Jumatatu, 24 Novemba 2014

KINANA AANZA ZIARA MKOANI MTWARA

 Vijana wa CCM wilaya ya Masasi wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili Nanganga wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ikiwa siku yake ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Mtwara baada ya kumaliza siku 8 za ziara mkoani Lindi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi wa CCM wilaya ya Masasi mara baada ya kuwasili mkoani humo ambapo anatarajiwa kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kubangua korosho cha Perfect Cashew Kernels Kate Kamba akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kwenye kiwanda chake cha kubangua korosho kilichopo Masasi mkoani Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya hatua mbalimbali za utayarishaji na ubanguaji korosho kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha Perfect Cashew Kernels Lydia Amuri

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mashine ya kubangua korosho yenye uwezo wa kubangua kilo 40 kwa saa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kubangua korosho cha Perfect Cashew Kernels Kate Kamba akizungumzia changamoto wanazopata wabanguaji wadogo wadogo wa korosho nchini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi na wafanyakazi cha kiwanda cha kubangua korosho cha Perfect Cashew Kernels na kuwaambia kuwa Korosho inaweza kubanguliwa nchini na kutoa ajira za kutosha kwani kiwanda cha korosho kinaajiri watu wengi sana hivyo ameitaka serikali kuwasaidia wananchi kuweza kumiliki viwanda vya korosho nakubangua hapa nchini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga kingo za barabara
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Masasi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano wa Fisi wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
 Wana CCM wakishangilia kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa fisi wilayani Masasi.
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Masasi kwenye uwanja wa Fisi na kuwataka Watanzania kukiamini chama chao .
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo mjini Masasi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara  Ndugu Mohamed Sinani(kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Masasi Mzee
Kazumari Malilo wakifuatilia makini mkutano unavyoendelea. 

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara  Ndugu Mohamed Sinani akitoa hotuba fupi kabla yakumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia.
 Katibu Mkuu wa CCM akivishwa mavazi ya Kimila na wazee wa jadi ambapo alisimikwa kuwa Mzee wa Jadi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Masasi ambapo aliwaambia viongozi wajenge utaratibu wa kuwaeleza wananchi maendeleo yao na yapi yamefanikiwa na wapi hawajafanikiwa, wapi yanakwamishwa.
Mbunge wa Jimbo la Masasi  Mariam Kasembe akieleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi unavyoelea kwenye jimbo lake ambapo huduma za msingi zimezidi kuimwarishwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Masasi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa viongozi wajifunze kujibu masuala ya msingi ya wananchi huku akitolea mfano wa umeme kukatika katika  hovyo.
Wananchi wakimsikiliza Kinana.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu