Unordered List


TAARIFA YA TUKIO LILILOTOKEA UBUNGO PLAZA KATIKA MKUTANO WA MWALIMU NYERERE FOUNDATION

IMG-20141102-WA0021
 Mkutano ulifanyika kuanzia saa 1520hrs ukiwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu mh. Joseph Sinde Warioba. Mkutano ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za kisiasa. Mkutano ulirushwa moja kwa moja na ITV na maudhui yake kimtazamo ulilenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya tume ya Warioba na ile ya Mh. Sitta na tume yake. Baada ya Mh. Warioba kuelezea kwamba Muungano sio tunu ila ni urithi ndipo wakereketwa w walipoinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya katiba ya Mh. Sitta ambayo wao wameshaikubali? Baada ya mabango yale kuinuliwa yakazua tafrani ambapo walishauriwa kutoyainua kwa sababu haukuwa mkutano wa kisiasa na wakanyang’anywa na kuyachana ndipo vurugu/kashfa/matusi yakaanza kutolewa dhidi ya meza kuu. Hali hii ilisababisha kushikana, kusukumana na kurushiana viti. Katika tafrani hiyo mh.WARIOBA ALIZOMEWA NA VINA WANADAIWA KUWA NI VIJANA WASOMI WANAOPENDA KATIBA INAYOPENDEKEZWA IANZE KUTUMIKA

Chapisha Maoni

0 Maoni