Unordered List


TAARIFA YA WAZIRI WA NISHANI NA MADINI PROF.MUHONGO KUHUSIANA NA SAKATA LA IPTL NA TEGETA ESCROW ALIYOIWASILISHA BUNGENI LEO

 
1
MAELEZO YA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI MAALUMKUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA
ESCROW
” YA
 TEGETA PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL1.
 
Historia ya Mradi
Mheshimiwa Spika 
,
Katika miaka ya tisini (1990s), Tanzaniailikuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hali iliyopelekea kuwepo kwa upungufu waumeme na kuathiri shughuli za maendeleo ya kiuchumi nakijamii nchini. Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali ilichukuahatua za dharura za kuanzisha mradi wa kufua umeme wenyeuwezo wa kuzalisha Megawati (MW) 100.
2.
 
Upatikanaji wa IPTL
Mheshimiwa Spika 
,
Mwaka 1994 Serikali ilitoa kazi yauwekezaji kwa Kampuni ya
Independent Power Tanzania Limited 
 (IPTL) iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni za
VIP Engineering andMarketing Ltd 
 ya Tanzania iliyokuwa na Asilimia 30 na
MECHMAR Corporation ya Malaysia 
 (MECHMAR) iliyokuwa naAsilimia 70. Kampuni ya IPTL ilipewa leseni ya kujenga, kumilikina kuendesha (
Build-Own-Operate 
) Mtambo wenye uwezo wakuzalisha umeme wa MW 100 kwa kutumia mafuta mazito eneola Tegeta-Salasala, Dar Es Salaam.
 
2
Katika
Ukurasa wa 52 Aya ya 2, ya Taarifa ya PAC,
 Kamatiimependekeza Mtambo huo utaifishwe.
Ufafanuzi:Mheshimiwa Spika,
Kulingana na Mkataba wa PPA kati yaTANESCO na IPTL, majukumu ya IPTL yalikuwa ni kujenga,kumiliki na kuendesha (Build, Own and Operate
– 
 BOO).Hivyo, kutaifisha Mtambo huo ni kukiuka makubalianokatika Mkataba wa PPA wa tarehe 26 Mei 1995, ukiukwajiwa aina hii ukitokea unaweza kuingiza Serikali katikamgogoro mkubwa ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kwenyeMahakama za kibiashara za kimataifa. Aidha utaifishaji wamiradi ya uwekezaji binafsi itakuwa ni njia ya kufukuzawawekezaji binafsi 
 
Mheshimiwa Spika 
,
 Tarehe 26 Mei, 1995, TANESCO na IPTLwalisaini Mkataba wa PPA kwa muda wa miaka ishirini (20), kwaajili ya kununua umeme utakaozalishwa na IPTL. Kwa mujibu waMkataba huo, IPTL ilitakiwa kuiuzia TANESCO umemeusiopungua Asilimia 85 ya uwezo wa Mtambo (
minimum off take 
).Hata hivyo, uzalishaji wa umeme haukuanza mara mojakutokana na mgogoro uliotokea kati ya TANESCO na IPTLkuhusu gharama halisi za uwekezaji na namna ya kukokotoa
Capacity Charges 
. Hivyo, IPTL ilianza kuzalisha umeme tarehe 15 Januari, 2002. Kutokana na hali hiyo muda wa miaka 20 ya
 
3
Mkataba ulianza kuhesabiwa tarehe 15 Januari, 2002 baada yakuanza uzalishaji (
Commercial Operation Date 
).
Mheshimiwa Spika 
,
Pamoja na mambo mengine muhimu yaliyokuwemo katika PPA, Kifungu Na. cha Mkataba huokinaipa TANESCO wajibu wa kulipa malipo yaliyotajwa hapo juuna kwamba endapo kutakuwa na mgogoro wowote kuhusiana namalipo hayo (
Disputed Amount) 
, itafunguliwa Akaunti maalum(
Escrow Account 
) ya kuhifadhi fedha hizo hadi pale pande mbilizitakapokubaliana juu ya uhalali wa malipo yanayobishaniwa.Aidha, chini ya PPA, migogoro yote kuhusiana na masuala yautekelezaji wa Mkataba huo ilitakiwa kuwasilishwa nakuamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi waMigogoro ya Uwekezaji (ICSID) ya London. Hivyo, ilikuwa ni jukumu la kila mhusika katika Mkataba huu kuwasilishamalalamiko yake ICSID yanapotokea.Katika Ukurasa wa 8 Aya ya 2 ya Taarifa ya PAC imeelezwakuwa mwaka 2004 TANESCO ilifungua shauri la ICSID 2kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya
Capacity Charge 
.
UfafanuziMheshimiwa Spika
,
Taarifa hiyo siyo kweli. TANESCOhaijawahi kufungua shauri lolote ICSID ya London auMahakama yo yote dhidi ya IPTL kupinga kiasi kikubwa cha

Chapisha Maoni

0 Maoni