Jumatatu, 10 Novemba 2014

UVCCM YAHITIMISHA BARAZA KUU LAKE DODOMA SALAMA

akisoma mapendekezo hayo,katibu mkuu wa uvccm taifa aliyasoma kama ifuatavyo

1..kuhakikisha ukawa wanapata mitaa 10 tu nchi nzima ktk uchaguzi mkuu ujao.

2.wapendekeza mchujo wa wagombea kabla ya kura za maoni 2015

3.wataka viongozi wa serikali ngazi zote  kufanya ziara kutatua migogoro ya ardhi,kutafuta masoko ya mazao kwa bei nzuri na marufuku mgambo kunyanyasa wafanya biashara ndogobdogo

4.serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali ktk kutatua tatizo la ajira

5.pongezi kwa katibu mkuu wa CCM ndugu kinana kwa uhodari wake kazini kukijenga chama

6.vijana kupambania fursa ili kujikwamua kiuchumi na halmashaur zitoe fedha asilimia 5 za vijana na wanawake haraka na kuwakopesha vijana haraka na ambazo hazijatoa ziwajibike

7.pongezi kwa bunge la katiba kupendekeza katiba bora na ni wajibu wa vijana kuiunga mkono

8.mchakato wa kumpata mgombea urais mwakani uanze mapema na wagombea wote wa CCM wapite kwenye midahalo nchi nzima ili kuwapa fursa watanzania na wanachama kupata usahihi wakujua ni mgombe yupi asimamishwe na chama

9.baadhi ya fedha za gesi zitumike kwa vyuo vya veta ili kuwapa elimu vijana wengi zaidi watakao jiajiri

pia akizungumza katika kulifunga baraza hilo la vijana BALOZI SIF ALI IDD ALISEMA;
1.vijana mkipata kazi kuweni waaminifu na acheni tamaa za haraka za utajiri,kama uongozi ni utajiri basi mzee kingunge na nyerere wangetajirika,watu wanajenga magorofa mikocheni kule ambayo hayalingani na mishahara yao,kule zanzibar tunawasughulikia watu hawa bila uoga

2.msifarakanishwe na wataka urais.
3.iungeni mkono katiba pendekezwa kwa kampeni za kisayansi
4.juzi maalim seif alitusema kuwa sie tunaiendesha znz kimabavu eti kisa kunamashehe wamekamatwa na sisi hatuwatetei,mtu huyu yaonyesha nae anahusika na mabomu ya watuhumiwa wanaliokamatwa maana hauwezi kuwatetea watu wanaotuhumiwa kulipua mabomu na kuua watu kama na wewe si muhusika ila atabambwa tu nae siku moja
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu