Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Alexander Rannkikh, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR
Jumatano, 31 Desemba 2014
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA MABALOZI WA URUSI, CANADA NA ALGERIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Alexander Rannkikh, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Picha na OMR
TAARIFA YA UFAFANUZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Katika gazeti la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari “Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya”. Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo:
Utendaji wa Wizara chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb)
Taarifa za gazeti hilo zilieleza kuwa utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini hasa katika uongozi wa Waziri Muhongo umekuwa ni wa kukatisha tamaa. Moja ya mifano iliyotolewa ni kuendelea kuwepo kwa wachimbaji madini wanaozidi kutorosha madini kwa nia ya kukwepa kodi. Hoja hii haina ukweli wowote kwani chini ya uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) utendaji wa Wizara umeimarika kwa kiasi kikubwa. Chini ya Uongozi wake kumekuwepo na uwajibikaji mkubwa kwa watumishi wa wizara ili kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi ipasavyo. Ni katika kipindi chake kumekuwepo na uanzishwaji wa madawati ya ukaguzi wa madini katika viwanja vikubwa vya ndege vya JNIA, KIA na Mwanza chini ya Wakala wa Ukaguzi wa madini (TMAA) ili kudhiditi wachimbaji madini na watu wengine wenye nia ya kutorosha madini nje ya nchi bila kuzingatia sheria. Kutokana na hatua hiyo madini mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15 yameweza kukamatwa. Madini yaliyokatwa bila kuwa na vibali halali
RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA SHEIKH ALI MZEE KOMORIAN KARIAKOO, DAR ES SALAAM
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu SheikhAli Mzee alipokwenda kuhani msiba huo jana Jumapili Desemba 29, 2014. Marehemu Sheikh Komorian
alifariki juzi Jumamosi Desemba 28, 2014 na kuzikwa jana Jumapili
Desemba 29, 2014
Jumanne, 30 Desemba 2014
MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MWENGE NA MATOPENI KATIKA WILAYA YA LINDI MJINI PIA AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa CCM wa Tawi la Kilimahewa lililoko katika Kata ya Mwenge Ndugu Mohammed Madodo mara baada ya kuwasili katika Tawi hilo kwa ajili ya mkutano na viongozi wa Tawi tarehe 28,12.2014.
MAAFISA, ASKARI NA WATUMISHI RAIA WA JESHI LA MAGEREZA WAPATIWA MAFUNZO YA JINSIA, ROMBO GREEN VIEW HOTEL - JIJINI DAR ES SALAAM
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Jinsia kwa Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza, leo Desemba 29, 2014 katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel. Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili ambapo yatafungwa rasmi kesho Desemba 30, 2014(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunura(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Augustino Mboje(kulia) ni Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi wa Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mbarak Semwenza.
Baadhi ya Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza wanaoshiriki Mafunzo ya Jinsia katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi. Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili ambapo yatafungwa rasmi kesho Desemba 30, 2014.
MBUNGE WA MOROGORO MJINI AZIZ ABOOD AENDELEA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KATIKA KATA MBALIMBALI
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akiwasikiliza Viongozi wa CCM wa Kata ya Konga wakati wa Ofisi ya kata hiyo Mara baada ya Mh Mbunge Kufanya Ukaguzi hiyo Na Kuahidi kutoa Msaada wa Bati 100 Kwajili ya Kumalizia Ujenzi wa Ofisi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akitoa maagizo kwa Mtendaji wa Kata ya Konga Kutafuta Eneo la Ujenzi wa Shule Hiyo haraka Iwezekanavyo.Mh Abood amemuagiza Mtendaji huyo ndani ya mwezi
Mmmoja wa amepata Eneo la Ujenzi wa Shule na Ujenzi Uanze Mara Moja Ambapo Mh Mbunge Amechangia Shilingi Milion 5 za Kuanza Ujenzi Huo .
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akiongea na Wato wa Kata ya Kauzeni mara baad ya Kuwasili katika Kata hiyo kwajili ya Kusikiliza Kero Zinazowakabili wakazi wa Kata Hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akitoa maagizo kwa Mtendaji wa Kata ya Konga Kutafuta Eneo la Ujenzi wa Shule Hiyo haraka Iwezekanavyo.Mh Abood amemuagiza Mtendaji huyo ndani ya mwezi
Mmmoja wa amepata Eneo la Ujenzi wa Shule na Ujenzi Uanze Mara Moja Ambapo Mh Mbunge Amechangia Shilingi Milion 5 za Kuanza Ujenzi Huo .
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akiongea na Wato wa Kata ya Kauzeni mara baad ya Kuwasili katika Kata hiyo kwajili ya Kusikiliza Kero Zinazowakabili wakazi wa Kata Hiyo.
Jumatatu, 29 Desemba 2014
NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo (Picha na Bashir Nkoromo)
MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MBANJA
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha
Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na vijana na wananchi mara baada
ya kuzindua rasmi shina la wakereketwa Zahanati Kempu lililoko katika
Kata ya Rasibura
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Mjini Mama
Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Tawi la CCM la Mbanja. Mama
Salma alitembelea tawi hilo jana kwa ajili ya kukagua kazi ya
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.
Baadhi
ya wajumbe wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Mabano katika Kata ya Mbanja
wakifurahia hotuba ya Mjumbe wa NEC Taifa wa Lindi Mjini Mama Salma
Kikwete wakati alipotembelea Tawi hilo.
Katibu
wa Shina la Wakereketwa Zahanati Kempu Ndugu Hidaya Chivi Ali
akikabidhi risala ya wanachama wa Shina hilo kwa Mjumbe wa NEC Taifa na
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
NAIBU WAZIRI MHE. JANUARY MAKAMBA AZINDUA KUNDI LA KAONE SANAA GROUP DAR LIVE
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba akiongea na wasanii....
Akiwa pamoja na wasanii
Jumapili, 28 Desemba 2014
TAARIFA KAMILI YA BOMU LILILOLIPULIWA SONGEA NA KUUA MLIPUAJI
maelezo kwa DCP Diwani Athumani ambaye aliwasili mkoani humo jana
kwaajiri ya bomu la kutengenezwa kienyeji ambalo askari wa doria
walinusurika kurushiwa na kumlipukia mlipuaji wa bomu hilo ambaye
alifariki papo hapo.
Askari WP Mariam mwenye namba 8616 akiwa amelazwa wodi ya
majeruhi hospitali ya Mkoa baada ya kujeruhiwa mkono wa kushoto kwenye
bega baada ya vipande vya bomu kumfikia akiwa na askari wenzake kwenye
doria siku ya sikukuu ya krisimas.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiuangalia mwili wa
mtuhumiwa wa ulipuaji wa bomu ambaye alitaka kuwarushua askari wa
doria wakati wa sikukuu ya krismas kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. (PICHA NA AMON MTEGA ,SONGEA)
Jumamosi, 27 Desemba 2014
FREDRICK SUMAYE: KUWENI NA HOFU YA MUNGU, NAYE ATASIKIA MAOMBI YENU KWA TAIFA
Upendo Kilahiro naye akafanya mabo makubwa mbele ya mashabiki wake wa muziki wa injili kama anavyoonekana jukwaani akiimba.
Mashabiki walishindwa kukaa chini wakati wote wa tamasha.
Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake jukwaani.
Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake jukwaani.
Mashabiki wakipata taswira kwa simu zao huku burudani ikiendelea.
Mwimbaji Emmanuel Mgogo naye amefanya mambo makubwa sana katika tamasha hilo.
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili.
Mwimbaji Joshua Mlelwa akikonga nyoyo za mashabiki wake kwa uchezaji wake na wacheza shoo wake huyu amekuwa pia akifanya maonesho kama haya Ulaya na Marekani ..
Edson Mwasabwite kulia ni Faraja Ntaboba kutoka DRC Congo wakionyesha vitu vikubwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mwimbaji kutoka Kenya Ritha Kisava ambaye ameshiriki Tamasha la Krismas kwa mara ya kwanza akiimba hii ilikuwa kama utabulisho wake kwa mashabiki wa muziki wa Injili nchini Tanzania.
LOWASSA AMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA ZAMANI, MH. ALI AMEIR MOHAMED
Ijumaa, 26 Desemba 2014
WAZIRI MUHONGO AANZA ZIARA YA SIKU 6 MKOANI MARA KUTEMBELEA MIRADI YA UMEME
Waziri wa Nishati na Madini akiulizia utekelezaji wa umeme katika kijiji cha Kamgendi katika siku yake ya kwanza ya siku 6 za ziara katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara
Meneja wa TANESCO mkoani Mara, Henry Byabato (kulia) akifafanua usambazaji wa umeme vijijini katika mkoa huo
Alhamisi, 25 Desemba 2014
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAAGA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA INDIA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Rais wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew Levi, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Jumatano, 24 Desemba 2014
PINDA AKUTANA NA KIONGOZI WA KAMPUNI YA GESI YA QATAR NA KUTEMBELEA ENEO LA UJENZI WA BANDARI MPYA YA QATAR
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bw. Otty Msuku ambaye ni Mtanzania , Mtalaamu wa upimaji ardhi katika mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Qatar wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa bandari hiyo akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 22, 2014. Katikati ni Mkurugenzi mwendeshaji wa Mradi huo, Don Morrison.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Qatar, Bw. Yusuf Ahmad Al Hammadi wakati alipotembelea eneo inapojengwa bandari hiyo kubwa na yakisasa akiwa katika ziara ya kikazi nPhini humo Desemba 22, 2014.