Unordered List


DK.BILAL KUWEKA JIWE LA MSINGI CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO

Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal (pichani) Desemba 2 anatarajiwa Kuwa mgeni
rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu Cha
Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Kijijini Kiromo,Bagamoyo Mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocheni Dar es
Salaam Ofisa Habari wa (UB), Happiness Katabazi alisema sherehe hizo
zitafanyika Kijijini Kilomo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na kwamba
uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha
Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao utaanza mapema Januari Mwaka 2015.

Katabazi alisema Dk. Bilal ndiye atakuwa mgeni rasmi katika sherehe
hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia
linatufundisha kuwa mji wa Bagamoyo ilikuwa ukikaliwa na watumwa.

” Sasa sisi UB tunaitambua hiyo historia na ndiyo maana tukaamua
kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la Bagamoyo.Na kwakuwa
kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, basi sasa kupitia UB ambayo
inajenga makazi yake ya kudumu katika mji huo, binadamu wote watakuwa
huru kwasababu tutapata elimu” alisema Katabazi.
Alisema UB
ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda
,Mikocheni ,Dar es Salaam na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB
kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo
hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu.

Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla
kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo. UB ilianzishwa rasmi Mwaka
2011.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Diama, Jumatatu, Desemba Mosi Mwaka 2014

Chapisha Maoni

0 Maoni