Jumatano, 3 Desemba 2014

HAYA NDIYO YALIYOJIRI SHINYANGA MKUTANO WA MWIGULU NI BAADA YA KUAPISHA MAKAMANDA

Baadhi ya makamanda wa vijana wa CCM mkoa wa Shinyanga wakila kiapo  baada ya kusimikwa  rasmi kushika wadhifa huo,kutoka kulia ni kamanda wa vijana mkoa Ahmed Salum ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Solwa akifuatiwa  na  Naibu  Kamanda wa vijana mkoa huo John Sukili aliyeshika  fimbo.
kamanda wa vijana Kahama Elias Kwandikwa akiwa na mbunge wa jimbo la Msalala  Ezekiel Maige wakila  kiapo mbele ya Naibu katibu  mkuu CCM  bara Mwigulu Nchemba .
Naibu katibu mkuu CCM bara ambaye pia  ni Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akizungumza  kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa manispaa ya Shinyanga katika  uwanja wa SHYCOM ,ambapo  alizindua rasmi kampeni za uchanguzi wa serikali  za mitaa na kusimika makamanda wa wilaya pamoja na mkoa.      Mwigulu alitumia fursa hiyo  kuwataka
 makamanda waliosimikwa kuhakikisha wanafanya kazi  kwa  uadilifu bila kuwafumbia macho watakao kwenda kinyume  na taratibu za chama, ili  kulinda  heshima iliyopo pamoja  na kusimamia  kikamilifu zoezi lililopo mbele yao ili washinde kwa kishindo.
Makamanda waliosimikwa wakiwa katika picha ya pamoja

Makamanda  wa  vijana CCM
Mbunge  wa jimbo la Kahama James  Lembeli akiwataka makamanda waliosimikwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia taratibu zote za chama na kuhakikisha hawasababishi makundi ndani ya chama kwa kuthamini walionacho na kuwabagua wengine.
Mbunge  wa jimbo  la Shinyanga Steven Masele ambaye pia ni Naibu waziri wa nishati na madini,akiwataka wananchi kuchagua viongozi wa serikali za mitaa wanaotokana na chama hicho ili kuleta ufanisi zaidi  katika kazi.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu