Katibu wa chama cha mapinduzi mkoani iringa HASSANI MTENGA akiwahutubia wananchi wa mataa wa semtema mjini iringa
Wananchi wa mtaa wa semtema wakimsikiliza katibu wa ccm mkoa HASSAN MTENGA
Na fredy mgunda, iringa
Katibu
wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Iringa HASSANI MTENGA, amefungua
rasmi kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa semtema
mkoani iringa.
Akiwahutubia
mamia ya wananchi wa mtaa wa semtema MTENGA aliwataka wananchi wa eneo
hilo kuwa makini wakati wa kuchagua kiongozi katika uchaguzi utakao
fanyika tarehe 14/12/2014.
MTENGA
alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu sana kwa maendeleo
ya nchi na watu binafsi kwa kuwa kila maendeleo yanaanzi chini ndio
yanaenda juu,hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini sana na kumchagua
kiongozi anayefaa.
aidha
MTENGA aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa kuacha kuiga
siasa chafu ambazo waiga kutoka kwa wapinzani wao kwa kuwa wanaiga kitu
ambacho hawakijua ambacho kitawaletea madhara baadae.
alisema
kuwa IRINGA ni ya watu wa iringa hivyo kuwaambia wanafunzi wa vyuo
vyote mkoani iringa kuwaachia siasa wana iringa na wao waendelee na
walicho kifuata hapa na sio isasa.
kwa
upande wake wanafunzi waliohudhuria mkutano huo walimsifu katibu huyo
wa chama cha mapinduzi kwa kuwa na sera zinazotekeleza na kuwaambia
ukweli vijana waliopo vyuoni kwqa kuwa wananfunzi wengi wamekuwa wakiiga
mambo mengi bila kujua nini kipo mbele yao.
lakini
wananchi waliojitokeza eneo hilo walimuita katibu huyo kwa jina dawa ya
muarobaini kwa maneno aliyoyatoa katika mkutano huo na kumsifu kiongozi
huyo kuwa ni kiongozi ayefaa kuigwa hapa mkoani iringa.
pia
kunabaadhi ya wananchi walisikika wakisema kwa sera za katibu MTENGA
mbunge wa jimbo la iringa mjini atake asitake ataondoka tu na kumwomba
aanze kukusanya kilicho chake.
0 Maoni