Unordered List


MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASMI MAJENGO YA TAASISI YA MAFUNZO YA UANASHERIA KWA VITENDO TANZANIA.

02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania kwa ajili ya kuzindua Taasisi hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2014.
Picha zote na OMR
01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2014.
09
010
03
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Desemba 22, 2014.

04 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi katika Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo hayo uliofanyika leo Desemba 22, 2014.
06
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la viwanja vya Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, baada ya kuzindua rasmi majengo hayo yaliyopo eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam leo Desemba 22, 2014.

Chapisha Maoni

0 Maoni