Unordered List


MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMUWAKILISHA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE MKUTANO WA MAZINGIRA LIMA PERU

unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wenzake wakati walipohudhuria katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo  alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrik zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMRunnamed1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru. Makamu wa Rais alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMR
unnamed3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru. Makamu wa Rais alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMRunnamed4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mjumbe maalum wa Marekani katika masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi, Todd Stern, baada ya kuhudhuria katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo  alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika
maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMR
unnamed5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Ujumbe wa China, katika mkutano wa Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Xie Zhenhua, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya kuhudhuria na kuhutubia katika mkutano huo unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo  alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrik zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi. Picha na OMRunnamed6Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Mawaziri wakati wakitoka katika chumba cha mkutano huo. Picha na OMRunnamed7Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Mawaziri wakati wakitoka katika chumba cha mkutano huo. Picha na OMRunnamed80Picha ya kumbukumbu na wadau wa masuala ya mazingira walipokutana katika viwanja vya kumbi hizo za mikutano. Picha na OMR
……………………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Desemba 09, 2014 amemuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, kwenye mkutano wa Kimataifa wa Mazingira Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, Peru.
 
Pamoja na shughuli nyingine ambazo zimemuhusisha Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika Mkutano huo ikiwa pamoja na kuwa eneo la Mazingira nchini liko chini ya Ofisi yake, Mheshimiwa Dkt, Bilal alipata fursa ya kutoa hotuba kwa niaba ya Wakuu wa Nchi za Afrika siku ya Ufunguzi wa Mkutano huo, huku akisisitiza katika hotuba hiyo umuhimu wa kila nchi kushiriki katika kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi na tena akaelezea kuwa, hakuna anayeweza kupona kwa kujificha ama kuachia kazi hii ifanywe na nchi baadhi na akaongeza kuwa, wanaochangia kwa kasi kubwa kuathiri mazingira wanatakiwa 
kutambua kwamba wanayoyafanya hayatawanufaisha milele hivyo nao washiriki kwa vitendo katika kukabiliana na janga hili kubwa linaloikumba dunia kwa sasa.
 
Awali akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alieleza kuwa yapo mabadiliko ya tabia nchi ambayo kimsingi yametengenezwa na binadamu wenyewe na kama binadamu wakiamua kukabiliana nayo 
wanaweza kabisa kuyatokomeza. Pia alifafanua kuhusu nadharia ya nchi kushirikiana kwa kuwa mabadiliko haya kwa sasa athari zake hazina mipaka na kwamba nchi zote lazima ziwe katika sehemu ya utatuzi wa tatizo hili kubwa linaloikabili dunia.
 
“Tutumie mapendekezo ya Lima kufungua njia mpya, tuwe na vipaumbele vinavyotekelezeka na kuonekana, Tutoke hapa Lima na twende kuandika historia mpya kwa dunia yetu,” alimalizia Ban Ki-moon.
 
Kwa upande wa Rais wa mkutano huo (Cop20) Manuel Pulgar-Vida ambaye pia ni Waziri wa Mazuingira wa Peru, alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha washiriki wa mkutano huo nchini Peru kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa Olanta Humala na kisha akafafanua kuwa nchi ya Peru imepitia masaibu kadhaa ya kimazingira na hivyo kupata nafasi ya kuandaa mkutano huu kwao ni heshima na wajibu katika dunia na kwamba anategemea maazimio ya Lima yasaidie dunia katika kukab iliana na tatizo hili 
linalokuwa la mabadiliko ya tabia nchi.
 
Kauli ya Mheshimiwa Manuel Pulgar inasadifu ile aliyoitoa pia  Christiana Fugueres, Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa wa Mkakati wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi ambaye aliuambia mkutano huo kuwa, wakati umefika kwa nchi zote kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi kwa pamoja kwa kuwa yanachangia kuongeza umaskini na ili jamii ipate ahueni, basi ni wajibu kwa kila binadanmu kuchukua nafasi yake katika kukabiliana na hali hii iliyopo.
 
Katika tukio jingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kukutana na Ujumbe kutoka Marekani uliongozwa na Mjumbe Maalum kutoka Serikali ya Marekani anayehusika na masuala ya Mabadiliko ya Tabia nchi Todd Stern, ambaye alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuhusu utayari wa serikali ya Marekani katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na kwamba nchi yake itashirikiana nan chi zinazoendelea ikiwemo Tanzania katika suala hilo. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata nafasi ya kukutana na ujumbe kutoka Jamhuri ya Watu wa China ulioongozwa na Mheshimiwa Xie Zhenhua ambaye alizungumzia kuhusu ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea katika suala la mabadiliko ya tabia nchi na akafafanua kuwa Tanzania na China zina uhusiano wa kindugu hivyo kama kutakuwa na jambo la kipekee baina ya nchi hizi mbili basi serikali ya China iko wazi kulipokea.
 
Mkutano huo pia umehudhuriwa na Rais wa Bolivia Evo Morales, Rais wa Nauru Baron Waqa, Waziri Mkuu wa Tuvalu Enele Sopoaga, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon. Mkutano huu unafanyika wakati dunia ikiwa imeanza kubadili fikra na misimamo kuhusu namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo nchi ambazo awali zilikuwa na misimamo mikali mfano Marekani na China sasa zimaeza kubadili fikra kuhusu suala hili na kwa sasa zinaanza kulipa uzito kutokana na athari yake pia kuzikabili nchi hizo.
Pamoja na Mheshimiwa Makamu wa Rais msafara wa Tanzia pia unawashirikisha Mawaziri Bilinith Mahenge (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira) Waziri Fatma Fereji (Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais SMZ), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim pamoja na wataalam wengine wa masuala ya Mazingira na Maliasili pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni