Jumatatu, 29 Desemba 2014

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MBANJA

Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na vijana na wananchi mara baada ya kuzindua rasmi shina la wakereketwa Zahanati Kempu lililoko katika Kata ya Rasibura 
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Tawi la CCM la Mbanja. Mama Salma alitembelea tawi hilo jana kwa ajili ya kukagua kazi ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.
Baadhi ya wajumbe wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Mabano katika Kata ya Mbanja wakifurahia hotuba ya Mjumbe wa NEC Taifa wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete wakati alipotembelea Tawi hilo.
Katibu wa Shina la Wakereketwa Zahanati Kempu Ndugu Hidaya Chivi Ali akikabidhi risala ya wanachama wa Shina hilo kwa Mjumbe wa NEC Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akisoma maelezo yaliyoko kwenye jiwe la msingi la shina la wakereketwa Zahanati Kempu mara baada ya kuzindua rasmi shina hilo. 
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na vijana na wananchi mara baada ya kuzindua rasmi shina la wakereketwa Zahanati Kempu lililoko katika Kata ya Rasibura.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanachama wa shina la wakereketwa Zahanati Kempu mara baada ya kulizindua rasmi.
Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya uanachama wa CCM Ndugu Nurdin Shaweji aliyejiunga na Chama hicho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tawi la Stendi lililoko katika Kata ya Rasibura. Picha na JOHN LUKUWI
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::

Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kushikamana kwa pamoja, kufanya kazi kwa bidii na kuzitumia rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo.
Rai hiyo imetolewa jana Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mitwero Stendi Kata ya Rasibura wilayani humo.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema mkoa wa Lindi umejaliwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na zao la korosho, ardhi yenye rutuba, bahari na gesi lakini bado kuna changamoto zinazowakabili wananchi na hivyo kukwamisha maendeleo yao.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na elimu kwani baadhi ya wanafunzi wafikapo darasa la tano wanaacha shule kwa ajili ya utoro, mimba za utotoni na vijana kutokufanya kazi kwa bidii.
“Kuna baadhi ya watoto wakifika darasa la tano wanaanza tabia ya utoro hakikisheni wanakwenda shule kusoma kwani elimu itawasaidia katika maisha yao, msikubali waache shule. Kutokana na umri wao mdogo wanaona raha kuacha shule na kwenda kucheza lakini wakifika umri wa utu uzima ndiyo watakapoona umuhimu wa elimu”. 
Maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana ikiwa kila mtu atapata elimu itakayomsaidia katika maisha yake, wakati shule za Sekondari za Kata zinajengwa kuna baadhi ya watu walitubeza na kuziita majina ya ajabu ikiwa ni pamoja na shule za Yeboyebo lakini shule hizi zimewasaidia watoto wengi kutoka familia maskini ambao wameweza kupata elimu”, alisema Mama Kikwete. 
Kuhusu tazizo la mimba za utotoni alisema ni hatari kwa maisha ya Mama na mtoto lakini kama kijana atasoma mimba zitaepukika, jukumu la wananchi ni kuhakikisha watoto wao wanasoma kwa bidii na kutokubali kupewa mimba ambazo zitawakatisha masomo. 
Kwa upande wa vijana MNEC huyo aliwahimiza kuangalia mstakabali wa maisha yao na kutumia muda wao kufanya kazi kwa bidii kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwani hizi sasa kuna baadhi ya vijana wakati wa asubuhi wanaacha kwenda shamba kulima na kucheza Pool kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata maendeleo. 
“Vijana wengine wanatumia madawa ya kulevya na kuvuta sigara wanajua kwa kufanya hivyo ndiyo ujanja kitendo ambacho siyo ukweli, bali unaharibu afya yako na kujirudisha nyuma kimaendeleo. Kama wewe kijana unahitaji kuwa na maisha bora ni lazima uachane na vitendo hivyo na kufanya kazi”, alisisitiza. 
Licha ya kufanya mkutano huo wa hadhara Mama Kikwete pia alifanya vikao na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM matawi ya Mbanja, Mabano na Mitwero Stendi na kuwataka wajumbe hao kuwapa vijana nafasi za uongozi pale watakapojitokeza kugombea nafasi hizo. 
Pia aliwahimiza wajumbe hao wakiwemo vijana, wanawake na wanaume kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani ili kuwe na ushindani wa kutosha ndani ya chama.

Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya shughuli za kichama na katika mkutano wa hadhara aligawa kadi kwa wanachama wapya 23 walijiunga na Chama Cha Mapinduzi.
CREDIT:SUFIANIMAFOTO
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu