Alhamisi, 18 Desemba 2014

MHE. DKT PINDI CHANA AZINDUA SEMINA YA KUDUMISHA AMANI NA KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI ROLYA, MARA

unnamed
Mheshimiwa Dkt.Pindi Chana (Mb.) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto tarehe 17/12/2014 alifungua rasmi semina maalum kuhusu masuala ya kukomesha vitendo vya Ukatili na kudumisha Amani Mkoani Mara. Semina hiyo iliyoandaliwa na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Rorya , Kanisa kuu Mt. Petro Kowak, kata ya Nyathorogo.
Wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo Mheshimiwa Naibu Waziri aliwasihi wadau mbalimbali wa maendeleo ya Jinsia kutekeleza kwa vitendo kauli Mbiu Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayosema “Maisha Yangu,Haki Yangu, Piga Vita Ndoa za Utotoni”

Alieleza kuwa Suala la ndoa za utotoni na ukeketaji linatia dosari
kubwa katika harakati za kumkomboa mtoto wa kike kwa vile taifa
linahitaji mchango wa kila mwananchi ili kufikia malengo yake ya
kujiletea maendeleo sambamba na utekelezaji wa Malengo ya Mpango wa
Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini( MKUKUTA), Dira ya
Maendeleo ya Taifa 2025 na Malengo ya Milenia, hivyo ndoa za utotoni
na ukeketaji zinapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote na jamii yote.
Aidha, akiwa Mkoani Mara, Mheshimiwa Dkt.Pindi Chana (Mb.) alitembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare, Musoma.
unnamed3
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu