• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Ijumaa, 30 Januari 2015

Waziri Mwakyembe tayari ndani ya Bunge la Afrika Mashariki

Waziri Harrison Mwakyembe akila kiapo ndani ya Bunge la Afrika Mashariki, Arusha.
Siku chache zimepita tangu yatangazwe mabadiliko madogo ndani ya Baraza la Mawaziri Tanzania.
Aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amehamishwa na kwa sasa ni Waziri wa Uchukuzi wakati Waziri Harrison Mwakyembe aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi kabadili kwenye nafasi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Leo kuna taarifa kwamba Waziri huyo ameapishwa katika Bunge hilo Arusha na kuahidi kushughulikia kero zote zinazoikabili Wizara hiyo kama ambavyo alifanya kwenye Wizara ya Uchukuzi.
Share:

KINANA AZURU KABURI LA DK.OMAR ALI JUMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi wengine wa CCM na ndugu wa aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hayati Dk.Omar Ali Juma wakiomba dua kwenye kaburi lake lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitia sahihi kitabu cha wageni kwenye kaburi la hayati Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hayati Dk.Omar Ali Juma  lililopo Wawi Mchekeni, Chake Chake ,Pemba
Share:

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE JIJINI PARISRais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Ikulu ya Ufaransamaarufu kama Champs L’Elysee jijini Paris Jumatano jioni Januari 28,2015 kuonana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande.
Share:

Alhamisi, 29 Januari 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MAJENGO YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA JIJINI PARIS

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Sallma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wafanyakazi wa ubalozi baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Sallma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
Share:

Jumatano, 28 Januari 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI CHARLES MWIJAGE WAANZA KAZI RASMI KWA KUTEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI

7
Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima (katikati) akielezea maendeleo ya mradi wa Kinyerezi I. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene. Kushoto kabisa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava.
Share:

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE LEO WILAYA YA WETE MKOA WA KASKAZINI PEMBA.

 Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba,Ndugu Kassim Mabrouk,mapema leo alipokuwa akiwasili mjini Wilayani Wete mkoa wa Kaskazini Pemba tayari kwa kuanza ziara ya siku tano mkoani humo.Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako Kisiwani Pemba kwa ziara ya Kuhimiza na Kukagua utekeleza wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinaa akisalimiana na baadhi ya Wanachama wa CCM Wilaya ya Wete,alipowasili katika ukumbi wa Jamhuri,ambapo Ndugu Kinana alipokea taarifa ya kazi ya chama na Utekelezaji wa Ilani na pia kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya.
Share:

NSSF, REAL MADRID KUZALISHA VIPAJI VYA SOKA TANZANIA.

3
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau  akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya shirika hilo na timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Dk. Dau alisema katika uendeshaji wa kituo hicho, Real Madrid itakua na dhamana ya kushughulikia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu.
2 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (aliyekaa kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (aliyekaa kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.
Share:

Jumanne, 27 Januari 2015

WAZIRI DKT. MAGUFULI AZINDUA UJENZI WA BARABARA ZA PETE JIJINI DAR ES SALAAM.


Waziri wa Ujenzi Mheshimkiwa Dkt.John Pombe Magufuli leo amezindua na kuweka  mawe ya msingi katika Ujenzi wa barabara za pete zitakazopunguza msongamano jijini Dar es salaam.
Barabara hizo zilizowekewa mawe ya msingi ni pamoja na ile ya  Kinyerezi –Kifuru hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilometa 14.0, Kigogo-Tabata Dampo yenye urefu wa kilometa 1.6, na Kimara Baruti-Msewe hadi Chuo Kikuu  cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 2.6. Barabara nyingine ni ile ya External –Kilungure hadi Kimara Korogwe kilometa 8.0, Wazo Hill-Goba hadi Mbezi mwisho kilometa 20 na Goba-Tangi bovu kilometa 9.0.
Akizungumza wakati akizindua ujenzi wa barabara hizo Waziri Magufuli amewataka wananchi kufuata sheria za barabarani kwa kutoingilia hifadhi za barabara na wale wenye nyumba pembeni mwa barabara kuzibomoa wenyewe ili kupisha ujenzi huo kwenda kwa wakati.
Share:

RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA MFALME WA SAUDI ARABIA, AWASILI BERLIN, UJERUMANI, KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25, 2015, alipofika kuhani kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari
yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Share:

DR SHEIN KUGOMBEA KWA MARA NYINGINE URAIS VISIWANI

Zanzibar. Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar imepitisha azimio la pamoja la kumtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kujitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais uchaguzi unaotarajia kufanyika mwaka huu,imefahamika Visiwani humo.
Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika Kongamano lililofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Fidel Castro na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, huko Pemba.
Share:

WAZIRI CHIZA AWASILI OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Christopher Chiza akipokea ua kutoka kwa mfanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Zubeda Ng'olongo kama ishara ya kumkaribisha ofisini hapo, leo Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na kuapishwa kushika wadhifa huo, awali Chiza alikuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
Share:

Jumatatu, 26 Januari 2015

MHE. ANGELLAH KAIRUKI AMKABIDHI OFISI MHE. UMMY MWALIMU

Naibu waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akikabidhiwa ua na mtumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Christina Nyenga wakati wa mapokezi ya Naibu Waziri jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki (kulia) akimkabidhi nyaraka mbalimbali Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu wakati akimkabidhi ofisi jijini Dar Es Salaam . kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri lililofanyika Jumamosi.
Share:

RAIS KIKWETE AWASILI RIYADH KUHANI KIFO CHA MFALME WA SAUDI ARABIA, KUFANYA ZIARA YA KIKAZI UJERUMANI NA UFARANSA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wan Kijeshi mjini Riyadh,
Saudi Arabia,  asubuhi ya Jumapili, Januari 25, kuhani kifo cha
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa
Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah,
Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na
Ufaransa kwa ziara za kikazi. unnamedjk 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Share:

Jumapili, 25 Januari 2015

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEINI AZINDUA SHEREHE ZA MIAKA 38 YA KUZALIWA CCM

 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzinzibar pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika uzinduzi wa kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM katika uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Pemba leo. 
Share:

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM,RAIS DKT SHEIN NA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE WAWASILI PEMBA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea  Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili mapema leo kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,ambayo Kitaifa zitaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma.
Makamu Mwenyeki wa CCM,Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, mara baada ya kuwasili mapema leo kwenye uwanja wa Ndege wa Pemba kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,ambayo Kitaifa zitaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma.Pichani Kati ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye pia amewasili leo na Ujumbe wake kwa ajili ya  ziara ya siku tano ya Kujenga na Kukiimarisha chama cha CCM.
Share:

Jumamosi, 24 Januari 2015

HAYA NDIO MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI YALIYOTANGAZWA NA RAIS KIKWETE JIONI HII

Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri,Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Ameliapisha jioni hii Ikulu,Jijini Dar es Salaam.
Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.
Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.
Share:

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA SIKU KUMI KISIWANI UNGUJA,KESHO KUWASILI KSIWANI PEMBA.

Pichani juu na chini ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Baadhi ya wakazi wa mji wa Kizimkazi waliofika katika uwanja wa Kizimkazi Mkunguni,Wilaya ya Kusini Unguja kumsikiliza.Ndugu Kinana ambaye leo anaikamilisha ziara yake ya siku kumi katika kisiwa cha Unguja akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,katika suala zima la kuimarisha uhai wa chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Share:

Ijumaa, 23 Januari 2015

UTIAJI SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA KUKIUNGANISHA CHAMA CHA SPLM CHA SUDAN KUSINI JIJINI ARUSHA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy waSudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek
Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakitia saini
mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha
Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari21, 2015 usiku. Nyuma yao ni mjane wa marehemu John Garang aliyekuwa
Mwenyekiti wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng de Mabior na Afisa wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Thobias Makoba. Nyuma
yao wakishuhudia utiaji saini huo ni Makamu wwa Rais Dkt Mohamed
Ghalib Bilali, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri Museveni wa
Uganda
Share:

Jumatano, 21 Januari 2015

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YAFURAHISHWA NA MIRADI YA VIJANA

unnamed (15)Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Siad Mtanda akizungumza na wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke kamati hiyo ilitofanya ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana vilivyonufaika na Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika manispaa hiyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Maabad S. Hoja na wamwisho kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw.P. Kagimbo  
Share:

Jumanne, 20 Januari 2015

KINANA AMALIZA ZIARA KATIKA JIMBO LA UZINI MKOA WA KUSINI UNGUJA

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Uzini na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha mapinduzi Mh. Mohamed  Seif Khatib mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Dunga wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2010, Katika mikutano mbalimbali ambayo Kinana amekuwa akihutubia na kuzungumza na wananchi na wana CCM amekuwa akihimiza viongozi kufuata maadili ya uongozi jambo ambalo ni muhimu na la lazima katika uongozi ili kuutumikia umma katika misingi mizuri na yenye tija,Katika ziara hiyo Kinana amewahimiza Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba mpya iliyopendekezwa kwakuwa inatatua kero nyingi za wanzanzibari  katika muungano na kuwafanya wawe na uhuru zaidi , kama vile Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iwapo Rais wa Jamhuri atatoka Bara, Zazibar kujiunga na jumuiya za kimataifa bila kikwazo, kuwa na uhuru wa kukopa na mambo mengine mengi yaliyomo katika katiba hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UZINI-ZANZIBAR)
Share:

Jumatatu, 19 Januari 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MAGHARIBI

1Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mti wa viungo aina ya Mdalasini wakati akipata maelezo kutoka kwa Othman Mohamed  mwenyekiti wa kikundi Kinachoendesha shamba la Spice Solution Farm lililopo Mwakaje  jimbo la Mfenesini Zanzibar  wakati aliposhiriki pia shughuli za upandaji wa miti katika shamba hilo, Katika ziara hiyo ambayo ni ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2010 Kinana Anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MFENESINI -ZANZIBAR)2Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la Spice Solution Farm Mwakaje Mfenesini.3Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia pilipili zilizolimwa katika shamba hilo huku akipata maelezo. 
Share:

MWIGULU NCHEMBA ATIKISA MKOA WA MOROGORO WOTE KWA SIKU MOJA

Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Gairo hii leo,Amesisitiza kuwatatulia swala la maji ambalo bajeti yake imeshaanza kufanyiwa kazi.Naibu katibu Mkuu akizungumza na wananchi wa Mvomero hii leo,Tatizo la Sukari ndio AGENDA kuu hapa Mvomero,Wananchi wanasumbuliwa na tatizo la soko la sukari na Migogoro ya Mashamba.Mwigulu Nchemba ameahidi kuchukua hatua kuhakikisha tatizo linapata dawa ya Kudumu.
Share:

Jumapili, 18 Januari 2015

PINDA AMTEMBELEA MBUNGE VITA KAWAWA HOSPITALI ALIKOLAZWA

Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akimpa pole Mbunge wa Namtumbo, MheshimiwaVita Kawawa ambaye amelazwa katika hospitali ya AMI jijini Dar es salaam kwa matibabu. Kushoto ni mke wa mbunge huyo, Siwa Kawawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Share:

KINANA AUNGURUMA WILAYA YA DIMANI MKOA WA MJINI MAGHARIBI ZANZIBAR

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara baada ya kupokelewa katika Ofisi kuu ya CCM mkoa wa Mjini Magharibi  wilaya ya Dimani Zanzibar akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba, Katibu Mkuu Kinana anaongozana na Nape Nauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama, Katika mkutano wa ndani akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu wa Halmashauri ya mkoa wa  mjini Magharibi  Kinana amesema katika mambo muhimu ambayo kamati za siasa zinatakiwa kuzingatia wakati wa kuteua wagombea mbalimbali ni Maadili ya viongozi, Ameongeza kwamba kama kuna kamati ya siasa itakiuka utaratibu huo na ikaonekana kubeba baadhi ya wagombea basi Kamati Kuu  haitasitakufuata utaratibu wa kikatiba na  kuteua kamati ya siasa nyingine ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea wote walioomba uongozi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DIMANI-MKOA WA MJINI MAGHARIBI -ZANZIBAR)

 Nape Nauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongozana na Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu Zanzibar mara baada ya kuwasili ofisi kuu ya CCM Kiembesamaki mkoa wa Mjini Magharibi.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu