Unordered List


DKT ALI MOHAMMED SHEIN AFUNGUA JENGO LA UPASUAJI VICHWA MAJI NA UTI WA MGONGO

  unnamed1x
Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman pamoja na Viongozi wengine alipofika katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
unnamed2x
Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa    Hospitali ya Mnanzi Mmoja Dk.Jamala Adam Taibu,alipofika   kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo  na Uti wa Mgongo leo (Neurosurgical Unit) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]

unnamed3x
Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kushoto) Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakili wa   taasisi ya NDkutoka Spein  sherehe hizo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
unnamed4x
Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Dk.Mohamed Ali Haji (ustadh) wa sehemu ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja wakati Rais alipowatembelea wagonjwa mbali mbali waliokwisha fanyiwa matibu na Kituo hicho baada ya kulifungua jengo hilo leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
unnamed5x
Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pilikushoto) na Makamo wa Kwanza wa Rais maalim Seif Sharif Hamad wakipata maelezo kutoka kwa Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakilishi  wa   taasisi ya ND kutoka Spain  wakati alipotembelea mashine za upasuaji baada ya kulifungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kulia)  Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dk.Jamala Adam Taibu pia  sherehe hizo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
unnamed6x
Wanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya wakiwa mbele ya jengo lajipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit)katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja baada ya kufunguliwa rasmi leo naRais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein likiwa la horofa mbili na uwezo wa vitanda 30 pamoja na vyumba (2)viwili vya upasuaji,[Picha na Ikulu.]
…………………………………………………………………………………
Na Miza Kona    –    Maelezo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amekemea tabia ya baadhi viongozi wa Taasisi  kuwazuia wafanyakazi wake kujiendeleza kielimu kwa lengo la kuongeza ujuzi na kuleta ufanisi.
Hayo ameyasema  Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja katika ufunguzi wa Jengo la Upasuaji Vichwa maji na Uti wa Mgongo ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya  miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema tabia hiyo haifai kwani inarejesha nyuma maendeleo ya wafanyakazi na kuanzisha majungu, fitna  na uhasama katika taasisi  kati ya wafanyakazi wa kawaida na viongozi wao.
Amefahamisha kuwa taaluma ndiyo inayopelekea ufanisi bora wa kazi na  kuleta mabadiliko kwa   kutoa huduma bora  na uhakika na kujenga taifa lililo imara.
“Mabadiliko hayaji   bila ya kuwa na taaluma  hasa katika sekta ya Afya hivyo viongozi  waruhusuni wafanyakzi wenu kupata elimu ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi”, alieleza Dkt. Shein.
Amesema lengo la  Serikali ni kuipa hadhi Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya rufaa kwa lengo la kuimarisha huduma bora lakini  kutokana upungufu wa vitendea kazi mabadiliko hayo yanakuja hatua kwa  hatua.
Dkt. Shein ameeleza lengo la  Serikali ni kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kutumia  wataalamu wenye elimu na vifaa  vya  uhakika kadiri ya uwezo uliopo ili kuimarisha afya za wananchi.
Aidha Dkt Shein amesema jitihada kubwa zinahitajika katika kuandaa mipango madhubuti itakayosimamia kuendeleza kitengo cha  upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo kwa kutafuta wataalamu na madaktari bingwa watakaoendesha matibabu hayo.
Amesema kitengo  cha huduma ya upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo ni cha pekee kwa Afrika Mashariki na Kati ambacho kitasaidia kupnguza gharama za usafirishaji wa wagonjwa wa matatizo hayo  nje ya nchi.
Amesisitiza madaktari kuwafanyia wagonjwa uchunguzi wa kina kabla ya kuwapa  matibabu ili waweze kutoa huduma ya uhakika na  kujiepusha kubahatisha.
Aidha ameutaka uongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja kukamilisha sheria na kuweka taratibu ili Hospitali hiyo iweze kujiendesha na kusimamia kazi bila kutegemea  Serikali kuu
“Nijukumu la uongozi wa Hospitali hii kuandaa mipango mizuri  itakayoweza kuiimarisha  ili lengo  la kujiendesha  liweze kufanikiwa”. Alisitiza Rais wa Zanzibar.
Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi, Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman alisema kupatikana kwa miundombinu katika kitengo hicho ni kuleta maendeleo katika sekta hiyo na ameeleza kitatoa huduma ya uhakika
 Jengo hilo lenye vyumba viwili vya upasuaji, wodi nne za kulaza wagonjwa na chumba cha mikutano  limejengwa kwa msaada wa Shirika moja la Hispania  na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  na limegharimu zaidi ya shilingi Mill 600 ambapo asilimia 60 zimetolewa na wafadhili.

Chapisha Maoni

0 Maoni