Jumatano, 28 Januari 2015

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE LEO WILAYA YA WETE MKOA WA KASKAZINI PEMBA.

 Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba,Ndugu Kassim Mabrouk,mapema leo alipokuwa akiwasili mjini Wilayani Wete mkoa wa Kaskazini Pemba tayari kwa kuanza ziara ya siku tano mkoani humo.Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako Kisiwani Pemba kwa ziara ya Kuhimiza na Kukagua utekeleza wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinaa akisalimiana na baadhi ya Wanachama wa CCM Wilaya ya Wete,alipowasili katika ukumbi wa Jamhuri,ambapo Ndugu Kinana alipokea taarifa ya kazi ya chama na Utekelezaji wa Ilani na pia kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya.
 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwa katika ukumbi wa Jamhuri wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo Utekelezaji wa Ilani.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM katika ukumbi wa Jamhuri mjini Wete mkoa wa Kaskazini Pemba mapema leo,Kinana alizungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo Utekelezaji wa Ilani.
Pichani kati ni Meneja Utawala wa shirika la Ununuzi wa Karafu (ZSTC),Bwa.Issa Hassani akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kulia alipokwenda kutembelea Ghala la Karafuu na kuona zoezi la ununuzi wa Karafuu katika Bandari ya Wete,Kaskazini Pemba.
 Katibu wa CCM,Ndugu Kinana akitoka kutembelea na kukagua bei ya karafuu katika ghala la Karufuu katika bandari ya Wete-Pemba.
 Ghala la Karafuu kama lionekanavyo pichani
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na wanachama wengine wa chama hicho,wakitoka kutembelea Kikundi cha Ushirika cha ufugaji wa samaki na uhifadhi wa Mazingira katika Jimbo la Gando,wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mshauri wa kikundi,Bwa.Mwinyjuma Hamad juu ya Kikundi cha Ushirika cha ufugaji wa samaki na uhifadhi wa Mazingira chenye idadi ya washirika wapatao 22,katika Jimbo la Gando,wilaya ya Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Mshauri wa kikundi (Organization for Gando Fishing, Farm & Enviromental Conservation) Bwa.Mwinyjuma Hamad akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana nama mabaki ya miti yanavyoweza kutengenezwa na kutumika kama mkaa ikiwa kama ni sehemu ya kusaidia kutunza mazingira.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki utengenezaji wa Maseredani (Majiko ya Mkaa) yanayotengenezwa  kwa kutumia udongo,Majiko jayo yanatengenezwa na Vijana wajasiliamali wapatao 21 katika kijiji cha Chanjaani,shehia ya Ukunjwi Jimbo la Gando,wilaya ya Wete mkoa wa kaskazini Pemba,ambapo mmoja wao alieleza kuwa wamekuwa wakifaidika na mradi huo kwa kiasi kikubwa,ikiwemo na kujiongezea kipato kwa kuuza kwa wingi majiko hayo,alisema kuwa asilimia 70 ya majiko yanatengenezwa Pemba,hivyo imepunguza uingizwaji wa majiko kutoka nje.
 Pichani shoto ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Zanzibar,Bwan Fakhi Othman Sharif akiwaongoza Katibu Mkuu wa CCM ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenda kupokea taarifa ya usambazaji wa Umeme na kushiriki kazi za Usambazaji umeme (kusimamisha nguzo za umeme),katika kijiji cha Chanjaani,jimbo la Tambwe,Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.Mradi huo una thamani ya shilingi milioni 84.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana katikati,Balozi Ali Karume kushoto na Dkt.Maua Daftari pichani kulia wakishiriki kufukia mabomba ya maji katika mradi wa usambazaji Maji katika Jimbo la Mtambwe,Wete mkoa Kaskazini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza na wanachama wa Tawi la Kigangani,jimbo la Ole,Wete,Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini Wete,mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia baadhi ya Wananchi waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini Wete,mkoa wa Kaskazini Pemba
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu