Jumanne, 20 Januari 2015

KINANA AMALIZA ZIARA KATIKA JIMBO LA UZINI MKOA WA KUSINI UNGUJA

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Uzini na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha mapinduzi Mh. Mohamed  Seif Khatib mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Dunga wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2010, Katika mikutano mbalimbali ambayo Kinana amekuwa akihutubia na kuzungumza na wananchi na wana CCM amekuwa akihimiza viongozi kufuata maadili ya uongozi jambo ambalo ni muhimu na la lazima katika uongozi ili kuutumikia umma katika misingi mizuri na yenye tija,Katika ziara hiyo Kinana amewahimiza Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba mpya iliyopendekezwa kwakuwa inatatua kero nyingi za wanzanzibari  katika muungano na kuwafanya wawe na uhuru zaidi , kama vile Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iwapo Rais wa Jamhuri atatoka Bara, Zazibar kujiunga na jumuiya za kimataifa bila kikwazo, kuwa na uhuru wa kukopa na mambo mengine mengi yaliyomo katika katiba hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UZINI-ZANZIBAR)

2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati alipowasili katika kijiji cha Dunga jimbo la Uzini mkoa wa Unguja Kusini leo.3Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana  wa pili kutoka kushoto akiwa katika mkutano wa ndani  pamoja na wawakilishi wenzake wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha Dunga. 4Ndugu Sauda Mpambalyoto Katibu wa CCM wilaya ya Kati mkoa wa Unguja Kusini akisoma taarifa ya utekelezaji ya chama cha mapinduzi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha Dunga leo.5Kutoka kulia ni Balozi Ali Karume na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakiwa katika mkutano huo.6Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa Unguja kusini.7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Vuai Ali Vuai kumwaga zenge la linta kwenye jengo la CCM Dunga.8Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa soko la samaki huko Unguja Ukuu jimbo la Koani.9Baadhi ya wana CCM wakifurahia wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika soko la Unguja Ukuuu jimbo la Koani.10Mwakilishi wa jimbo la Chwaka Mh. Issa Haji Gavu akizunguza wakati alipokabidhi misaada mbalimbali katika jimbo lake la Chwaka.11Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi jenzi kwa vijana wa jimbo la Chwaka.12Injinia Heri Tumaini Mkurugenzi wa kampuni ya CHECOTEC (T) LTD inayojenga barabara katika jimbo la Chwaka akishukuru na kuzungumza maneno yenye hisia ya furaha yake kwa kukutana na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.13Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kupanda miti katika shamba la viungo la Alis Spices &Fruits Farm wakati alipokagua shughuli zinazofanywa katika shamba hilo lililopo Kwabani jimbo la Koani Zanzibar.14Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia miche ya mikarafuu.15Mmiliki wa shamba hilo Bw. Ali akizingumza na kumshukuru  katibu mkuu wa CC kwa kutembelea shamba hilo.16Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na mmiliki wa shamba hili pamoja na wafanyakazi.17Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda kwenye tanki la maji wakati alipotembelea na kukagua mradi huo uliopo kijiji cha Michui jimbo la Koani Zanzibar.19Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni jimbo la Uzini.20Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono yao kuashiria kuiunga mkono na kuipitisha Katiba mpya iliyopendekezwa.21Mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib akiwahutubia wananchi wa jimbo la Uzini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni.2223Baadhi ya wawakilishi wa timu mbalimbali wakiwa na jenzi zao zilizokabidhiwa na mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib.24Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Tunduni wakati wa mkutano wa hadhara,25Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana  wa kwanza kutoka kushoto akiwa  na wawakilishi wenzake wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kijiji cha Tunduni.26Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu