Jumapili, 18 Januari 2015

KINANA AUNGURUMA WILAYA YA DIMANI MKOA WA MJINI MAGHARIBI ZANZIBAR

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara baada ya kupokelewa katika Ofisi kuu ya CCM mkoa wa Mjini Magharibi  wilaya ya Dimani Zanzibar akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba, Katibu Mkuu Kinana anaongozana na Nape Nauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama, Katika mkutano wa ndani akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu wa Halmashauri ya mkoa wa  mjini Magharibi  Kinana amesema katika mambo muhimu ambayo kamati za siasa zinatakiwa kuzingatia wakati wa kuteua wagombea mbalimbali ni Maadili ya viongozi, Ameongeza kwamba kama kuna kamati ya siasa itakiuka utaratibu huo na ikaonekana kubeba baadhi ya wagombea basi Kamati Kuu  haitasitakufuata utaratibu wa kikatiba na  kuteua kamati ya siasa nyingine ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea wote walioomba uongozi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DIMANI-MKOA WA MJINI MAGHARIBI -ZANZIBAR)

 Nape Nauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongozana na Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu Zanzibar mara baada ya kuwasili ofisi kuu ya CCM Kiembesamaki mkoa wa Mjini Magharibi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wajumbe mbalimbali na wa wana CCM wakati alipowasili wilaya ya Kiembesamaki wilaya ya Dimani mkoa wa Mjini Magharibi leo.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yusuf Mohamed Yusuf akimkaribisha Ndugu Abdulrahman Kinana ili kuongea na wajumbe wa halmashauri ya wilaya ya Dimani.
  Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, kulia Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na kushoto ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Bi. Khadija Abood wakiwa katika mkutano huo.
 Mjumbe wa Kamati kuu wa CCM Mh. Balozi Seif Ali Idd akizungumza katika mkutano huo wa ndani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe hao hawapo pichani.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Kirtkumar Dave Meneja wa Kiwanda cha maziwa cha Azam kilichopo Fumba Unguja wakati alipotembelea kiwanda hicho na kukagua shughuliza uzalishaji kiwandani hapo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya Meneja wa kiwanda cha maziwa cha Azam Bw.Kirtkumar Dave
 
 SEhemu ya mitambo ya uzalishaji wa kiwanda hicho
 Meneja wa kiwanda hicho Kirtimar Kumar akimueleza jambo Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uzalishaji wa kiwanda hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia baadhi ya maziwa yaliyozalishwa kiwandani hapo.
 
 Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akishiriki kupatkia katoni za maziwa kwenye kiwanda hicho.
 Meneja wa kiwanda hicho Kirtimar Kumar akimzawadia  katoni ya maziwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.akipokelewa na Profesa David Mfinaga Naibu wa Makamu Mkuu wa chuo cha UDSM wakati alipotembelea chuo Sayansi ya Bahari Shakani
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. akizungumza na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusafisha eneo la chuo hicho kinachoendelea kupanuliwa , kulia ni Profesa David Mfinaga Naibu wa Makamu Mkuu wa chuo cha UDSM na kushoto ni Ndugu Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua majengo ya chuo hicho huku akiongozwa na Profesa David Mfinaga Naibu wa Makamu Mkuu wa chuo cha UDSM katikati ni Desiderius Masalu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka chuoni hao.
 Msafara wa Katibu Mkuu ukikatiza katika msitu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mikoko huko Fumba kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Yusuf Mohamed Yusuf.
 Hapa akishiriki zoezi la uhifadhi wa Kaa
 Akizindua Gari la wagonjwa Ambulance
 Wananchi na wana CCM wakinyanyua mikono yao juu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Magereza..
 Balozi Ali Karume akiwahutubia wananchi katika mkutano huo
 Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kwenye viwanja vya  Magereza.
 Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Magereza Zanzibar
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaongoza wana CCM wapya kula kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi zao zauanachama
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu