Ijumaa, 2 Januari 2015

MAKACHERO KUTOKA DAR WATUA MWANZA KUMSAKA YULE MTOTO ALBINO ALIYETEKWA JUZI

Mwanza. Timu ya makachero wa polisi kutoka Dar es Saalm imewasili mkoani hapa juzi kuongeza nguvu ya kumsaka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Pendo Shilinde (4) ambaye anasadikiwa alitekwa  akiwa nyumbani kwao juzi.Tukio hilo lilitokea kwenye Kijiji cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba wilayani Kwimba saa 4:00 usiku, wakati mtoto huyo alipochukuliwa na watu wasiojulikana ambao walivunja mlango wa nyumba yao kwa kutumia jiwe kubwa, maarufu kwa jina la la “fatuma” na baadaye kutokomea naye.Polisi wametangaza dau la Sh3 milioni kwa mtu atakayesaidia kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watu waliohusika kumteka mtoto huyo.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilidai kuwa tayari watu sita wametiwa mbaroni wakihusishwa na utekaji huo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alisema ataiongoza timu hiyo inayowashirikisha pia makachero wa mkoani hapa.
Akitoa taarifa za kutekwa kwa mtoto huyo, Mlowola alisema mpaka sasa bado hawajafanikiwa kumpata licha ya kuendelea na mahojiano na watu wanne wanaowashikilia, akiwamo baba mzazi, Emmanuel Shilinde.
“Hatujafanikiwa kumpata mtoto huyu, lakini tumeomba timu ya makachero wa polisi kutoka Dar es Salaam iliyokuja kuongeza nguvu za kumtafuta na tayari wamewasili na kazi inaanza mara moja. Tutahakikisha wote waliohusika wanakamatwa,” alisema Mlowola.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu