Unordered List


RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA MFALME WA SAUDI ARABIA, AWASILI BERLIN, UJERUMANI, KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25, 2015, alipofika kuhani kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari
yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Fawzia Rasheed, Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani, leo Jumatatu 26, 2015 kuungana na viongozi mbali mbali duniani kujadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea. PICHA NA IKULU

Chapisha Maoni

0 Maoni