Unordered List


UTEUZI MWINGINE MAKINI WA JK BODI YA TANESCO..

2_57880.jpg

Ndugu zangu,
Juma lililomalizika zimetufikia tena habari kuwa Rais Jakaya Kikwete amemtua Dr. Mighanda Manyahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco.
Kwa mara nyingine tena, nauopongeza uteuzi huu wa Rais kwa kuachana na mazoea ya kuwaweka wanasiasa kwenye nafasi za uwenyekiti wa Bodi.
Kama alivyofanya kwa kumteua Mkurugenzi wa TPDC Dr Mataragio, safari hii tena Rais amemteua Mtanzania mwenye utaalamu kwenye eneo husika kuwa Mwenyekiti wa Bodi. Ndivyo Rais alivyofanya pia kwenye Bodi za Tiper na TPDC.
Ni kazi njema pia kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwateua wajumbe wa Bodi ya Tanesco kwa kuingiza Watanzania wenye taaluma zao badala ya wanasiasa.

Wanasiasa kwenye nafasi za uwenyekiti wa bodi , na hata kuwa wajumbe wa bodi imekuwa ni moja ya vyanzo vya kuanguka kwa mashirika yetu ya kizalendo. Ni kwa sababu moja kuu, wanasiasa wamekuwa na hulka ya kutanguliza maslahi yao binafsi, na ya kivyama hata kwenye mambo ya kimsingi ya kitaifa. Na kumekuwa na tatizo la migongano ya kimaslahi pia.
Ona mfano wa Victor Mwambalaswa, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Nishati na Madini na wakati huo huo akawa mjumbe wa Bodi ya Tanesco. Halafu tunashangaa kwanini mambo yalikuwa hayaendi Tanesco.
Kwa Rais kuwaweka kando wanasiasa kwenye nafasi za kuongoza bodi za mashirika anafungua ukurasa mpya utakaotoa fursa ya watendaji kwenye mashirika ku practice proffesional freedom kwa maana ya uhuru wa kitaaluma badala ya kuingiliwa na wanasiasa wenye kuendekeza bla bla za kisiasa zenye kutanguliza maslahi yao na ya vyama vyao.

Chapisha Maoni

0 Maoni