• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumatatu, 30 Machi 2015

ASENGA ABUBAKAR: TUMECHOKA NA MICHANGO YA DIWANI WA CHADEMA KILOMBERO

Komredi Asenga Abubakar akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kilombero, Ifakara.
 Komredi Asenga Abubakar akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kilombero, Ifakara.
 Komredi Asenga Abubakar akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Kilombero, Ifakara.
Komredi Asenga Abubakar akizungunguka mtaani Kilombero, Ifakara.

IFAKARA KILOMBERO,,,TUMECHOKA NA MICHANGO YA MAENDELEO TOKA DIWANI WA CHADEMA,,,,,,,walidanganya wakati wakampeni kuwa wataongoza na kuleta maendeleo bila micha...ngo sasa nini?
Geti la ushuru kero kubwa
baadhi ya watendaji wa kata hasa wa Mbingu,,,,amekuwa kero
CCM NI CHAMA CHA KUDEAL NA CHANGAMOTO ZA UMMA,,,TUTASHINDA PAMOJA

Share:

JENERALI MWAMUNYANGE: MAMLAKA ZA MISHENI ZA ULINZI WA AMANI ZIWE WAZI


Na Mwandishi Maalum, New York
Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, amelishauri   Baraza Kuu la  Usalama la Umoja wa Mataifa,   kuweka  bayana    na kwa uwazi mamlaka ( mandate) ambayo misheni ya kulinda Amani itapaswa kutelekeza  kule inakopangiwa kwenda.

Ametoa  ushauri huu   siku ya Alhamisi  wakati alipokuwa akitoa mchango wake kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi  ambao nchi zao zinachangia  katika operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.

Katika  mkutano huo uliokuwa wa siku moja, na kuhudhuriwa na  Wakuu wa Majeshi  na  Maafisa wa Ngazi za Juu ,kutoka nchi 108, Jenerali  Mwamunyage amesema;
“ Wakati wa utoaji wa idhini na mamlaka kwa   misheni ya   kulinda Amani,  Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  linatakiwa kumwita mbwa kwa  jina lake kama lilivyo.Mbwa aitwe kwa jina lake. Elezeni bayana na  kwa    uwazi  mamlaka na idhini  za utekelezaji za ya misheni ”

Na kuongeza, “ iwekwe wazi, kama ni misheni ya kulinda Amani, basi ielezwe ni ya kulinda Amani, na kama  ni  ya matumizi ya nguvu  basi na iwe hivyo”. Amesisitiza Mkuu wa Majeshi
Amesema kwamba, kwa kutamka  jina halisi /mamlaka  ya misheni  pale inapoundwa,  Baraza Kuu la Usalama  linakuwa linapeleka ujumbe ulio sahihi kwa pande zote zinazohusika  pamoja na nini wakitarajie.

Jenerali Mwamunyage ameuleza washiriki wa mkutano huo  mkutano wa kwanza wa aina yake  kuwakutanisha Wakuu wa Majeshi zaidi ya mia moja, wakati mmoja na mahali pamoja. Kwamba, uwazi huo pia utasaidia  kuweka bayana hatua za utekelezaji  zinazofanywa  na walinzi wa amani   kwenye eneo la utekelezaji.

Vile vile Mkuu wa Majeshi ya Tanzania ameshauri pia kuwa misheni  ambayo tangu  kuundwa kwake zilikuwa na mamlaka ya kutumia nguvu,   ni vema zisiendelee kutambuliwa hivyo pale mamlaka ya misheni hiyo  yanapobadilika  kutoka matumizi ya nguvu na kuwa misheni ya kulinda Amani au jina lolote lile.

Tanzania  inawanajeshi wake katika Misheni mbalimbali  ikiwa ni pamoja na   UNAMID ( Darfur) UNFIL, ( Lebanon) MONUSCO ( DRC) na katika maeneo mengine. Vile vile Tanzania ina Polisi na  Askari Magereza ambao nao wanahudumu katika misheni mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo ambao ulifunguliwa na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na  Ban Ki Moon na kufungwa na  Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson.  Jenerali Davis Mwamunyange amesema,  mkutano kama huo unapashwa kuitishwa mara kwa mara kwa kuwa unawawezesha  wakuu wa majeshi kubadilishana uzoefu wao katika utekelezaji wa  operesheni za ulinzi wa Amani na hasa kwa kuzingatia kwamba nchi wanachama ndio wanaotoa wanajeshi wao na ndio  haswa wanaokumbana na changamoto mbalimbmali za utekelezaji wa  dhamana hiyo.

Awali akifungua mkutano huo,   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon  pamoja na kuwashukuru  Wakuu hao wa Majeshi kwa mchango wao katika eneo hilo la  ulinzi wa Amani,  amesema   operesheni  ya kulinda Amani chini ya Umoja wa Mataifa,  licha kwa kwamba ni  dhamana inayohitajika sana  lakini pia inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Akazitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa  ni  upugufu wa raslimali fedha,  zana,  vifaa na teknolojia za kisasa lakini pia ugumu na hatari wanazokumbana nazo walinzi wa Amani, ambapo  hivi sasa mbinu za kigaidi na uvamizi kwa walinzi wa Amani ni baadhi ya changamoto na hatari wanazokumbana nazo.

Katibu Mkuu, amewataka wakuu hao wa majeshi kuongeza ushirikiano wao kwa  Umoja wa Mataifa na hasa katika kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto za kiulinzi na kiusalama ambazo duni hivi sasa inakabiliana nao.

Akaongeza kuwa   kujitokeza kwa idadi kubwa ya wakuu hao wa majeshi ya  ulinzi kushiriki mkutano  huo, kumeipa faraja kubwa  Umoja wa Mataifa.

Naye  Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson, akihitimisha mkutano huo, amewataka wakuu hao wa majeshi na serikali zao kuendelea na majadiliano  ya mchakaTo wa  kuundwa kwa majeshi ya ulinzi ya kikanda,  majadiliano ambayo  yanatakiwa kuendelea  kuelekea mkutano wa Operesheni ya Ulinzi wa Amani  utakaofanyika mwezi  Septemba mwaka huu.

     Wakuu hao wa Majeshi ya Ulinzi pamoja na kutoa mchango wa mawazo yao, pia walipata fursa ya kupata maelezo kutoka kwa  Viongozi wakuu waandamizi wanaoongoza    Idara zinazozohusu  Operesheni ya Ulinzi wa Amani.

-------------------------------------------------------
HABARI KATIKA PICHA
 " Mnatuwakilisha vema?" ndilo swali ambalo   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,  Jenerali Mwamunyange alilowauliza watanzania hawa wawili,  Afisa wa Usalama wa UN Bw. Jacob Mwashiozya na  Bw.  Joseph Msami, wa Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa walipokuwa  wakisalimiana naye na ujumbe wake  mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa majeshi ya ulinzi
 Jenerali Davis Mwamunyange (watatu kushoto), akiwa na ujumbe wake mbele ya bendera ya Tanzania, baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Majeshi ya  Ulinzi kutoka nchi 108. Kutoka kushoto ni  Kanali Adolf Mutta, Brigedia Jenerali Luwogo, Brigedia Jenerali Kamunde,  Meja Ngh'abi, na  Luten  Kanal Itang'are
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiingia kwa staii ya aina yake wakati alipokwenda kufungua mkutano wa kwanza wa aina yake  kufanyika  katika Umoja wa Mataifa,  ambapo Wakuu wa Majeshi  ya ulinzi kutoka  nchi zaidi ya 100 walikutana kwa wakati mmoja na mahali pamoja kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu operesheni za ulinzi wa amani za umoja wa mataifa.
Share:

KINANA AWATAKA WANANCHI WA VUCHAMA WILAYA YA MWANGA KUENDELEA KUSHIKAMANA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kikundi cha ngoma wakati akiwasili kwenye kata ya Kileo,wilaya ya Mwanga ,anayeongozana na Katibu Mkuu ni Mbunge wa Jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe.
 Kikundi cha utamaduni kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana alipotembelea kwenye kijiji cha Kileo,kata ya Kileo ambapo alijionea ujenzi wa nyumba za kisasa za walimu
Nyumba ya kisasa ya  Waalimu wa shule ya sekondari Kileo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Kileo ambapo alijionea ujenzi wa nyumba bora za walimu.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipita juu ya mfereji wa maji katika Skimu ya umwagiliaji Kivulini
Mbunge wa Jimbo la Mwanga ,Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe (katikati) akimpa maelezo ya mradi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) wakati alipotembelea skimu ya umagiliaji Kivulini ,mwingine pichani ni Katibu wa CCM Tawi la Kivulini Ndugu Nuru Juma Mwanga.
Skimu hii ya Umwagiliaji Kivulini hulimwa mpunga, mahindi,maharagwe na mboga mboga za majani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa mtaro wa maji katika skimu ya umwagiliaji Kivulini, kushoto ni Profesa Jumanne Maghembe Mbunge wa Jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kivulini wilaya ya Mwanga na kuwaambia wajitahidi kutafuta masoko nje zaidi ya mkaa maalumu unaotengenezwa pumba ya mchele pamoja na majani ya makuruwila.
Mkaa huo unatengenezwa na kikundi cha Mkombozi Kivulini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mara baada ya kuzungumza na wananchi wa kata ya Kivulini, Kileo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji Profesa Jumanne wakati wa kukagua mashine za kuvunia mpunga

 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Lembeni kijiji cha Mangara ambapo alihimiza waendelee kushikama na kuwa na umoja.
Mbunge wa Jimbo la Mwanga akizungumza na wananchi wa kijiji chaMangara ,kata ya Lembeni .
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Mwanga Ndugu Joseph Tadayo akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mangara
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM tawi la Mangara kata ya Lembeni
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti kama ishara ya kutunza mazingira nje ya jengo la ofisi ya CCM tawi la Mangara, Lembeni wilaya ya Mwanga.
Mbunge wa Jimbo la Mwanga ambaye pia ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe akicheza ngoma ya asili mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuingia kwenyekikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya.
Wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Mwanga wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha na kukijenga chama mkoa wa Kilimanjaro
 
 Mbunge wa Jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe akisalimiana na Ndugu Wildad Msuya mara baada ya kuwali kwenye kijiji cha Kifula.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye uwanja wa mikutano Vuchama akiongozana na kikundi cha ngoma ya asili ya mjungu
Mjumbe wa NEC ,Ndugu Joseph Tadayo akiwasalimu wananchi wa Vuchama wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanjani Vuchama wilaya ya Mwanga.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Vuchama kata ya Mwaniko ambapo aliwaambia wapinzani wameshapoteza dira.
Mzee akifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa chama.
Wazee wa Vuchama wakisikiliza hotuba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mwaniko kata ya Vuchama na kuwataka washkamane katika kusimamia haki na shughuli zao za kila siku za kuletea maendeleo.
Share:

RAIS ROBERT MUGABE AWASILI ARUSHA KUFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA VIONGOZI VIJANA AFRIKA-CHINA


 Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbambwe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kushiriki ufunguzi wa Kongamano la Viongozi Vijana Afrika-China .
  Rais Robert Mugabe akisalimiana  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa KIA
 Rais Robert Mugabe akizungumza jambo wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa KIA
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe akiwa na viongozi mbali mbali akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Share:

MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA BARAZA LA USHAURI WA KISIASA LA WATU WA CHINA AWASILI ARUSHA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa KIA.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China amewasili nchini kuja kushiriki kwenye ufunguzi wa Kongamano la Viongozi Vijana wa Afirka pamoja na China litakaloanza leo mjini Arusha.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.Wang Jiarui wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa KIA.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk.Wang Jiarui mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA ambapo atashiriki kwenye ufunguzi la Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Ushauri wa Kisiasa la Watu wa China pia Waziri wa Idara ya Kimataifa wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Dk. Wang Jiarui akizungumza  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Ndugu Daudi Felix Ntibenda kwenye hotel ya Ngurdoto,Arusha.

Share:

Jumamosi, 28 Machi 2015

ANNE KILANGO "CCM IMETEKELEZA ILANI YAKE KWA UKAMILIFU SAME"


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mashine ya kupasulia mbao wakati alipotembelea chuo cha ufundi  Maore kilichopo kata ya Muheza, Same Mashariki.
Chuo hicho kitachukua wanafunzi 300.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi katika chuo cha ufundi Maore kata ya Muheza jimbo la Same Mashariki ikiwa sehemu ya ziara ya kujenga na kuimarisha chama.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati alipotembelea chuo cha ufundi Maore,wengine pichani ni Padri Everest Abeid,Padri Japhet Njaule (kulia) na Padri Moses Mbwambo ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Anne Kilango Malecela
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo kwenye daraja la Mang'a katika kijiji cha Mang'a Myamba, Same Mashariki.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amesimama kwenye mto Mang'a.
  Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela akizungumza na vyombo vya habari kushukuru serikali ya Chama Cha Mapinduzi kujenga daraja la Mang'a katika kijiji cha Goha mbele ya  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiweka shada la maua pamoja na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Ndugu Anne Kilango Malecela(katikati) ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) kwenye makaburi ya watu waliofariki kwa mafuriko na maporomoko ya mawe yaliyotokea kiijiji cha Goha kitongoji cha Mang'a.
 Ujumbe wa kijijiwe kimoja kijiji cha Goha huko Same Mashariki.
 Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Ndugu Anne Kilango Malecela akielezea changamoto ya mtaji wa kukiwezesha kiwanda cha kusindika Tangawizi kuweza kufanya uzalishaji bora kwa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea kiwandani hapo Mang'a Myamba ,Same Mashariki.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Mang'a Myamba nje ya kiwanda cha kusindika Tangawizi ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia namna Tangawizi inavyoandaliwa kusindikwa kwenye kiwanda cha usindikaji tangawizi kilichopo Mang'a Myamba.
 Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela na Mbunge wa Viti Maalum Wanawake mkoa wa Kilimanjaro Betty Machangu wakiteta jambo na  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuingia kwenye mkutano Mkuu wa Jimbo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachi wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa mkutano Ndungu ,Same Mashariki.
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa hadhara.
 Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Ndugu Anne Kilango Malecela akihutubia wananchi wa Ndungu kwenye mkutano wa hadhara wa CCM
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape akihutubia wakazi wa Same Mashariki na kuwataka kuendelea kuamini Chama Cha Mapinduzi kwani vyama vingi vya upinzani havina uwezo wa kuongoza kutokana na kukosa sera mbadala kwa maendeleo ya wananchi.
 Wananchi wakifuatilia mkutano
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Same Mashariki ambapo alisema CCM itasimama imara kutetea haki za wanyonge nchi nzima na kuwataka viongozi na wana CCM kwa jumla wawe mstari wa mbele katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM 2010.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu