Ijumaa, 20 Machi 2015

KIKWETE ALIHUTUBIA BUNGE BURUNDI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya  Jumatano, Machi 18, 2015 amewasili nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo. 
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mji mkuu wa Burundi wa Bujumbura, Rais Kikwete amepokelewa na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunzinza na pamoja na mamia kwa mamia ya wananchi wa Burundi. 
Rais Kikwete ambaye amewasili Burundi akitokea Dodoma ambako alikuwa katika ziara ya kikazi pia leo Machi 19, 2015, atahutubia Bunge la Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki (EALA) katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) katika hotuba ya The State of the East African Community Address.
 Saa chache baada ya kuwasili Bujumbura, Rais Kikwete amehudhuria chakula cha jioni ambacho ameandaliwa na Rais Nkurunzinza kwenye Hoteli ya Panoramique. 
Wabunge wa Bunge la EALA pia wamehudhuria chakula hicho cha jioni. Rais Kikwete ataondoka Burundi mara baada ya kuhutubia EALA kurejea mjini Dodoma kuendelea na ziara yake.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Maua kutoka kwa watoto waliokuja kumlaki katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bujumbura ambapo alianza ziara ya kikazi ya siku mbili.
 Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bujumbura leo jioni.Rais Kikwete yupo nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 Rais Kikwete na mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipokea heshima wakati nyimbo za Taifa za nchi zao zikipigwa
 Rais Kikwete na mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakikagua gwaride liloandaliwa na jeshi la Burundi.
Rais Kikwete akiwa na Mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi jijini Bujumbura jana  jioni.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu