Ijumaa, 27 Machi 2015

KINANA AINGIA SAME MAGHARIBI Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk. David Mathayo David wakati wa mapokezi katika kata ya Njoro .
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ikiwa pamoja na kukagua,kusimamia na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa kata ya Njoro ikiwa ni kituo cha kwanza katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM jimbo la Same Magharibi.
 Wananchi wa kata ya Njoro wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwapongeza kwa uamuzi wao wa kujenga shule ya sekondari katika kata yao.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa vazi la heshima mara baada ya kusimikwa kuwa chifu wa wapare.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na silaha za jadi alizopewa baada ya kusimikwa kuwa chifu wa kabila la wapare.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda miti kwenye eneo la shule ya sekondari ya Njoro,jimbo la Same Magharibi ikiwa sehemu ya utunzaji mazingira.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi wakishiriki ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari ya kata ya Njoro.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Same Magharibi na kuwataka wajumbe hao kuhimiza umoja kati ya wana CCM na kuwapongeza kwa ushindi mzuri wa serikali za mitaa.
Katibu Mkuu pia alisisitiza kuwa kutokana na tatizo la maji kuwa kubwa nchi,CCM itahakikisha kwenye ilani yake mpya kuipa kipaumbele cha kwanza maji safi na salama kwa watanzania.
   Baadhi ya wajumbe wakifuatilia hotuba za  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano mkuu wa Jimbo la Same Magharibi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Makanya.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makanya ikiwa sehemu ya ziara yake katika jimbo la Same Magharibi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa wakati wa mkutano wa kuwasalimia wananchi kijiji cha Makanye ,jimbo la Same Magharibi.
 Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dk. David Mathayo David akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji kabla ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuzindua mradi wa maji safi na salama.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji ambapo aliwaambia CCM itaendelea kutekeleza yale ambayo imewaahidi wananchi wake.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufukia mabomba ya maji katika kijiji cha Gonjanza pamoja na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David wakinywa maji ya bomba mara baada ya Katibu Mkuu kuzindua mradi wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu baadhi ya changamoto za wananchi wa Hedaru waliomsomea kwenye risala yao, Katibu Mkuu alipita Hedaru kushiriki na kukagua ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Hedaru.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu