Jumamosi, 14 Machi 2015

KINANA;" CCM MONDULI ENDELEENI KUSHIKAMANA "


Friday, March 13, 2015

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Lolkisale ,Monduli Arusha .
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kukiimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha umeme kama ishara ya kuzindua umeme katika kijiji cha Lolkisale.
Mradi wa umeme vijijini (REA) ni mradi unaodhaminiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 100%.
Mbunge wa Jimbo la Monduli ,Waziri Mkuu Mstaafu Ndgu Edward Lowassa akiwasalimu wananchi wa Lolkisale mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuzindua rasmi umeme kijijini hapo.
Wananchi wa Lolkisale wakisikiliza hotuba za viongozi wao.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Nangole akihutubia wananchi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia wananchi hao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Lolkisale ambapo aliwapngeza kwa kuipa kura CCM kwenye chaguzi za serikali za mitaa.
Wananchi wa Lolkisale wakipiga makofi kushangilia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa hongera Mhandisi wa Tanesco mkoa wa Arusha Ndugu Seraphin Moshy mara baada ya zoezi la kuwasha umeme katika kijiji cha Lolkisale kukamilika.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na madaktari na wauguzi wa hospitali ya wilaya Monduli.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi jengo jipya la hospitali ya wilaya ya Monduli kwa kushirikiana Mbunge wa Monduli, Waziri Mkuu mstaafu Ndugu Edward Lowassa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanga mawe kwa ajili ya sakafu wakati alipotembelea kijionea maendeleo ya jengo la kisasa la hospitli ya Monduli.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia Viongozi na wananchi wa Monduli mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya majengo mapya ya hospitali ya wilaya ya Monduli.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Monduli mjini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa shukrani kwa vikundi vya burudani.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa Monduli mjini
Wananchi wa Monduli mjini kila mtu kwa nafasi yake akijaribu kupata kumbukumbu ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara mkoani Arusha.
Wananchi wa Monduli mjini wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya  kukiimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki palizi kwenye shamba la mpunga Mto wa Mbu,Monduli mkoani Arusha.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mto wa Mbu Arusha.
Vijana wa Mto wa Mbu wakishangilia CCM Oyee
Mbunge wa Viti Maalum Ndugu Namelok Sokoine akiwasalimu wananchi wa Mto wa Mbu na kuwaambia ni muhimu sana kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuwasihi kujitokeza kwa wingi mara tu baada ya tarehe ya kujiandikishwa kutangazwa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Waziri kuu mstaafu Edward Lowassa kwenye  viwanja vya mkutano Mto wa Mbu ,Monduli Arusha.
Wananchi wa Mto wa Mbu Arusha wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kuzunguka nchi nzima ya kuimarisha na kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010.

Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu