Jumamosi, 14 Machi 2015

WAZIRI SOFIA SIMBA AWAPONGEZA ASKARI WANAWAKE WANAOSHIRIKI ULINZI WA AMANI

 

Saturday, March 14, 2015
Na Mwandishi Maalum, New  York
Ushiriki wa askari wanawake   katika Operesheni za Ulinzi wa Amani za  Umoja wa Mataifa,  ni baadhi ya  mafanikio ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajivunia miaka 20 baada ya Mkutano wa Kihistoria wa wanawake uliofanyika Beijing, China mwaka 1995

Waziri wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na  Watoto, Mhe. Sophia Simba ( Mb) ameyasema hayo  leo ( alhamis) wakati alipokuwa akitoa tathmini na changamoto za utekelezaji wa  maazimio muhimu yaliyofikiwa katika mkutano huo wa  wanawake Beijing.

Mhe. Waziri Simba, anaongoza ujumbe wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  katika Mkutano wa Hadhi ya Wanawake ( CSW) unaoendelea hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  katika Ujumbe huo  wa Tanzania unajumuisha na washiriki kutoka  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwamo  Mhe. Zainab Omar Mohammed,  Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, vijana, wanawake na watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

“ Katika miaka  miaka  20 iliyopita, yapo  mambo mengi ambayo Tanzania tumepiga hatua za kuridhisha, katika maeneo ya uwezeshwaji  na fursa sawa kwa wanawake. Katiba za pande zote mbili za Muungano  zinaainisha vema kuhusu hadhi ya mwanamke. Na   Katika  katiba mpya inayopendekezwa  hivi sasa  kuna   eneo  ambalo linazungumzia kwa kina Usawa wa Jinsia na Uwezeshwaji wa wanawake.” anasema Waziri Simba

Vile vile ameeleza  baadhi ya sheria  ambazo ama zimefanyiwa marejeo au kutungwa kwa lengo la kuboresha usawa wa kijinsia. Amezitaja baadhi ya  sheria hizo kuwa ni sheria zinazohusu watoto,  sheria zinazohusu usafirishaji wa binadamu,  sheria ya ardhi, HIV/AIDS na sheria ya makosa ya kujamiana.

 Kuanzishwa kwa dawati la jinsia na watoto katika vituo vya Polisi,  vituo  vya kuhifadhi  watoto,  vituo kwaajili ya  wanawake wanaofanyiwa ukatili na mtandao wa viongozi wa madhehebu ya dini kuhusu ukatili dhidi ya wanawake. Ni baadhi ya mafanikio ambayo yameelezewa na Mhe. Waziri
Ameeleza  zaidi kwa kusema, Wanawake wengi sasa wanashiriki katika siasa ambapo  kwa mfano  asilimia 36 ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ni wanawake na   kwa upande wa Zanzibar asilimia 33 ya  Wawakilishi ni wanawake. Na  kwamba  kumekuwapo  pia ongezeko  la idadi ya  wanawake Majaji na Mahakimu na wanaoshika nafasi za uongozi.

Mhe. Simba amewaeleza wajumbe wanaoshiriki  mkutano huo  kwamba katika kuhakikisha  panakuwa na fursa sawa  katika  ajira  utumishi wa Umma,   kuna  kifungu   katika sheria za utumishi wa umma vinavyoainisha kwamba  pale  mwanamke na mwanaume wanapokuwa na sifa zinazolingana, basi mwanamke atafikiriwa kwanza.

Kwa upande wa elimu,  pamoja na  kuwa na  uwiano sawa kati ya wavulana na wasichana katika shule za msingi. Anasema elimu ya  msingi inatolewa bure katika shule za serikali   na kwamba utaratibu huo pia utafanyika katika  shule za  sekondari  za umma. Aidha  ameelezea ongezeko la wanafunzi wa kike wanaochukua masomo ya sayansi.

Kwa upande wa Afya,  Mhe. Waziri amesema  Tanzania imepiga hatua za kuridhidha katika upunguzaji wa  vifo vya wanawake wajawazitio na vya watoto wachanga.

Hata hivyo pamoja na  mafanikio  hayo na mengine mengi ambayo  Tanzania inajivunia kuhusu hadhi ya wanawake na watoto wa kike,  anasema kama ilivyo kwa mataifa mengi yanayoendelea, Tanzania pia bado inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwamo  za uhaba wa fedha kwa miradi inayohusu masuala  ya jinsia,  ndoa na mimba za utotoni,  umaskini wa kaya na ukatili dhidi ya wanawake.

Mhe. Waziri Simba, Tanzania imejifunza kutokana na changamoto hizo na nyinginezo na kwamba imejipanga vema kutekeleza baadhi  ya changamoto hizo  hususani  upunguzaji wa umaskini,  kupitia malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya  2015.
 Mhe. Asha-Rose Migiro ( Mb) wakati huo akiwa  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na  baadhi ya askari wanawake kutoka JWTZ wanaoshiriki katika  operesheni ya kulinda  amani kupitia Umoja wa Mataifa huko  Lebanon. Katika mchango wake,  Mhe. Simba  pamoja na mafanikio mengine ambayo  Tanzania imeyapata  katika miaka 20 tangu mkutano wa Beijing  ni pamoja na askari wanawake  kupata fursa za kushiriki katika operesheni za kulinza amani zinazoratibiwa  na Umoja wa Mataifa.> Picha ya Maktaba
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu