• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumapili, 19 Aprili 2015

UVCCM WALALA NA WAHANGA WAMAFURIKO WAKIITAKA SERIKALI ITIMIZE AHADI YAKE YA KUWAPA MAKAZI HARAKANdg Husna Sekiboko Mwenyekiti wa kamati ya maafa jana amewahani waathirika wa maafa ya mafuriko Kahama kwa niaba ya BARAZA KUU LA UVCCM TAIFA  kwa kushirikiana na katibu msaidizi mkuu Ndg Mpokwa, katibu wa mkoa wa Shinyanga Dada Teddy, Mjumbe wa baraza kuu Taifa anaepitia mkoa wa Shinyanga ndugu Zuber Bundara na mbaraza wa Kigoma Ndg Waziri Moris. wamekabidhi misaada mbalimbali ikiwemo unga, Maharage, chumvi na sabuni.

Wahanga wameishukuru sana UVCCM  na wameomba jamii iguswe na jambo hili kama UVCCM  ilivyokuswa kwa sababu bado misaada inahitajika sana kwa wahanga.

Bi Husna amewashukuru viongozi wote kwa ushirikiano hususani wote waliochangia.

Kidumu chama cha mapinduzi.
Uvccm mbele daima.

Share:

UCHUMI WA GESI UNA HATUA TATU

Njia 3 muhimu katika ujenzi wa uchumi wa gesi Tanzania

Ugunduzi huo mpya katika Kisima Piri-1 umefanyika katika eneo lenye kiwango kidogo cha mawe ya mchanga kama ilivyokuwa wakati ilipogunduliwa gesi katika Kisima cha Zafarani-1 mwaka 2012.PICHA|MAKTABA
Na Dk. A. Massawe
YA KWANZA
Mojawapo ya njia zitakazofanikisha matumizi ya gesi yetu asilia hapa chini yawe yenye tija zaidi ni ile ya kuisambaza maeneo yote nchini kwa kuanzia na miji mikuu ya kanda au mikoa kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani na kuzalisha umeme kwa ajili ya matumizi ya pale pale unapozalishwa.
Kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam itakakotumika kuzalishia umeme, majumbani na viwandani ni sahihi tu kama umeme wote utakaozalishwa utatumika ndani ya ukanda wa Dar es Salaam.
Yaani, ni sehemu kidogo tu ya gesi asilia inayowasili Dar es Salaam ingebaki hapo hapo kwa ajili ya kuzalisha umeme na matumizi ya majumbani na viwandani ndani ya ukanda wa Dar es Salaam na kitakachosalia kiendelee na safari yake hadi kanda nyingine za Tanzania kuzalisha umeme na kwa ajili ya matumizi mengine ya moja kwa moja majumbani na viwandani kuendana na mahitaji ya kila kanda.
Lengo ni kuondokana upotevu mkubwa wa umeme na gharama kubwa ya kuusafirisha umbali mkubwa kutoka kanda moja ya Tanzania hadi nyingine, pia ikizingatiwa kwamba, zaidi ya umeme, kila kanda hapa Tanzania pia inahitaji gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja majumbani na viwandani kama Dar es Salaam.
Hivyo ni kosa kuzalisha umeme wa megawati 3000 hapa Dar es Salaam kutokana na gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya matumizi ya ukanda wa Dar es Salaam na kanda nyingine zilizoko mbali na Dar es Salaam kwani njia sahihi ni kusambaza uzalishaji wa umeme utokanao na gesi asilia kote nchini kwa kusambaza gesi asilia kote nchini kwa njia ya mabomba na kufunga mitambo midogo midogo ya uzalishaji wa umeme wa gesi asilia kwenye kila kanda kuendana na mahitaji halisi ya kanda.
Hivyo, cha muhimu zaidi kwenye kufanikisha matumizi ya gesi asilia hapa nchini yawe yenye tija tosha ni kujenga miundo mbinu ya mabomba kwa ajili ya usambazaji gesi asilia kikanda kote nchini itakakozalisha umeme na kutumika moja kwa moja majumbani na viwandani kikanda kuendana na mahitaji halisi kikanda ili kukwepa upotevu mkubwa wa umeme na gharama kubwa za kuusafirisha umbali mkubwa kutoka kanda hadi kanda, huku ikizingatiwa kwamba, zaidi ya umeme, kanda zote pia zinahitaji gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja majumbani na viwandani kama Dar es Salaam.(P.T)
YA PILI
Njia ya pili itakayofanikisha matumizi yenye tija ya raslimali ya gesi asilia iliyogundulika hapa nchini ni kutumia hisa za Serikali kwenye raslimali hiyo iliyoko ardhini ikisubiria kuanza kuvunwa kama rehani kuchukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kuzalishia umeme wa maji huko Stigler's na wa makaa ya mawe huko Mchuchuma na kwingineko. Ni matumizi yanayowezesha kurudisha mikopo na kuleta faida hata kabla uchimbaji wa gesi asilia iliyotumiwa kama rehani haujaenda mbali sana, huku ikizingatiwa kwamba maelfu ya megwati za umeme wa maji ambazo hazijavunwa huko Stiglers na kwngineko hapa nchi huwa zikipotea kila saa miaka nenda rudi wakati gesi asilia na makaa ya mawe yanaweza kusubiri ardhini hadi uvunwaji wake kwa ajili ya uzalishaji wa umeme utakapoanza.
YA TATU
Njia ya tatu itakayofanikisha matumizi yenye tija tosha ya raslimali ya gesi asilia iliyogundulika hapa nchini ni kuwekeza mapato ya serikali yatokanayo na uvunwaji wa ralimali yake ya gesi asilia kwenye mfuko endelevu ''Sovereignity Fund''wa kutolea mikopo yenye riba nafuu kwa sekta za umma (kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi na uendelezaji wa miundo mbinu ya kitaifa na kwenye makampuni ya kimataifa yaliyo mihimili mikuu ya maendeleo ya uchumi wa dunia kisayansi na kiteknolojia (kuiwezesha Tanzania kuwa sehemu ya wahimili wakuu wa uchumi wa dunia kisayansi na kitknolojia na kuwa mmojawapo ya wanaonufaika sana), na kwa sekta binafsi (kuwezesha ukuwaji wa ujasiriamali hapa nchini).
Ni kuzingatia kwamba raslimali ya gesi asilia hapa nchini ni urithi usio endelevu wa vizazi vyote vya Tanzania, na njia ya kuhakikisha matumizi yake ni yenye manufaa makubwa zaidi kwa vizazi vyote vya Tanzania ni kutumia mapato ya serikali yatokanayo na uvunwaji wake kama kianzio endelevu cha mikopo yenye riba nafuu kwa sekta binafsi na za umma kote nchini.
Chanzo:wavuti.com
Share:

DAWA FEKI ZA KAMATWA MWANZAMaofisa zaidi ya 30 kutoka mamlaka ya chakula na dawa na baraza la Famasi Tanzania wamekamata ghala lenye dawa za serikali,zilizopigwa marufuku na zilizokwisha muda wake wa matumizi zenye thamani ya shilingi milioni 97 zikiwa zinamilikiwa na mfanyabiashara wa jijini mwanza CHARLES MBUSIRO kinyume cha sheria.
Ghala hilo lililopo eneo la ilemela jijini mwanza limekutwa likiwa limesheheni zaidi ya 120 za dawa ambazo ni sawa na tani 42 zikiwemo dawa za serikali za Kenya na Uganda, dawa za misaada, dawa zilizopigwa marufuku nchini kama vile klorokwini ya sindano, amodiaquine na gripe water -dawa nyingine zilizokutwa ndani ya ghala hilo na kwenye duka lake la dawa lililopo Natta barabara ya nyerere ni pamoja na ambazo hazijasajiliwa na TFDA na azisizoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka ya dawa.
Meneja wa usalama wa dawa wa TFDA Kissa Mwamwitwa ndiye aliyeongoza zoezi hilo liliendeshwa chini ya usimamizi mkali wa askari polisi wenye silaha za moto.
Baadhi ya maofisa wanaotekeleza operesheni hiyo, wakiwemo wanasheria kutoka TFDA na baraza la famasi tanzania pamoja na meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Florent Kyombo wakizungumzia tukio hilo wamesema taratibu za kisheria zinafanyika ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kahasa ilemela Richard Peter alikuwa shuhuda wakati maofisa hao wa TFDA, baraza la famasi tanzania na askari polisi walipokuwa wakitekeleza zoezi hilo kwenye ghala la dawa ambalo linasemekana bado halijasajiliwa na TFDA huku mmliki wake charles mbusiro akitoroka kwa kuruka ukuta na kutokomea kusikojulikana.(KILONGE)
Share:

Ijumaa, 17 Aprili 2015

LALA SALAMA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA


Friday, April 17, 2015

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali katika kumswalia aliyekuwa katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri katika Msikiti wa Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja kabla ya mazishi yake leo,[Picha na Ikulu.]
  Baadhi ya wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakilibeba jeneza la aliyekuwa katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja,[Picha na Ikulu.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,Makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sherif na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (katikati) wakiwa na Viongozi wengine na Wananchi katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo  kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitia udongo kufukia kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo  kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja,[Picha na Ikulu.]
Share:

AJALI SASA BASI

http://2.bp.blogspot.com/-06QFkzxMuDI/VSwTc6tHDeI/AAAAAAAHRAs/ssMrwjVZHGg/s1600/unnamed%2B(37).jpg
Share:

HALI YA UCHUMI TANZANIA SASA NI SHWARI

1
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akimsikiliza kwa makini Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier walipokutana katika mikutano hii ya kipupwe inayoendelea hapa Mjini Washington DC.Wengine ni ujumbe kutoka Tanzania pamoja na timu ya wataalam kutoka Benki ya Dunia.
2
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum akifuatilia kwa makini maswalialiyokuwa akiulizwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier hayupo kwenye picha. Kulia ni katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar.
3
Ujumbe wa Mkutano huo kutoka pande zote mbili yaani Tanzania na Benki ya Dunia, wakimsikiliza kwa makini Mchumi mwandamizi kutoka Benki ya Dunia.
4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akijadiliana jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier kabla ya kikao kuanza rasmi.
5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akiandika kwa makini hoja na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akijibu na kueleza kwa umakini hoja na mapendekezo yaliyokuwa yametolewa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.
Wakati Tanzania ikiendelea kupambana na umaskini , Benki ya Dunia imesema kuwa," tumefurahishwa sana na mwenendo mzuri wa usimamizi wa fedha na bajeti". Hayo yalisemwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier katika mkutano ambao waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum alikuwepo.
Mambo mbalimbali yalizungumziwa katika mkutano huo ambapo suala la upatikanaji wa fedha kusaidia bajeti ya serikali lilipewakipaumbele.Maboresho katika Sekta ya umeme nalo jambo mojawapo liliopewa uzito kwani Nchi wahisani wamepata moyo wakuachia misaada baada ya kuona Serikali imeweza kulishughulikia suala zima la IPTL.
" Nchi wahisani wamekubali kuendelea kutoa misaada kwa asilimia mia, hii ni kwa sababu tu! serikali yenu imekubali kuchukua hatua dhidi ya tatizo la IPTL", alisema Philippe.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhe. Mkuya alisema kuwa, suala la kuboresha Pension nalo lilizungumziwa na chombo hiki kitasaidia serikali katika kuboresha malipo ya uzeeni (pension) na kuwezesha mashirika ya "pension" ili yaweze kuwa na uwezo wa kusaidia wastaafu. Aidha tumekubaliana kuwa watatusaidia katika suala zima la kuboresha uwazi serikalini na mazingira ya biasha Tanzania.Aliongeza Mkuya.
Jambo lingine lililochukua uzito katika majadiliano hayo ni suala la kufanya ukaguzi Bandarini. Hili limejitokeza baada ya kubainika kuwa kuna baadhi ya wafanya biashara sio waaminifu hivyo benki ya Dunia imeitaka Serikali kuangalia upya maamuzi ya mwanzo ya serikali yakuto kagua mizigo, na kusema kuwa wanasubiri majibu juu ya kubadilisha utaratibu wa mwanzo. Tanzania imekubali kukaa kwa pamoja Wizara na Fedha na TRA ili kurudisha majibu na mkakati ambao kama serikali watakuwa wamekubaliana.
"Kumekuwa na madai mengi ambayo yanadaiwa na makandarasi na wafanyabiashara wadogo, tutajitahidi kuyalipa iliyaishe lakini kwa wale wenye nyaraka halali, tunaenda kupiga marufuku kwa Afisa masuuli wote kuwa kuanzia sasa hakuna kufanya malipo yoyote kama hakuna fedha kwa ajili ya shughuli hiyo".Alisema Mkuya.
" Hii itasaidia kupunguza madeni. Ninasema haya kwani ndicho kitu tulichokubaliana kwenye mkutano huu". Alisistiza Mkuya.
Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. Hali ya hewa ni baridi kiasi.(Muro)
Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha
Ingiahedi C.Mduma
Washington DC
16/04/2015
Share:

Jumamosi, 4 Aprili 2015

POLE SANA WANASIMBAZoezi la uokoaji wa watu waliokuwa ndani gari hilo ikiendelea.

Muonekano wa gari hilo baada ya ajali.
Ajali mbaya imetokea leo maeneo ya Makunganya, Barabara kuu ya kutoka Morogoro kwenye Dodoma baada ya gari iliyokuwa imewabeba washabiki wa Timu ya Simba Sports Club kupoteza muelekea na kuingia porini, watu nane wamepoteza maisa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya.
Hili ni pigo kubwa sana kwa Timu ya Simba, tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
Tunatoa pole wa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi kuwa kuondokewa na washabiki wake hao, na Mungu aziweke Roho za Marehemu hao mahala pema Peponi, Amin. (Muro)
Share:

Alhamisi, 2 Aprili 2015

KINANA ;MOSHI ACHENI USHABIKI WA KISIASA


Tuesday, March 31, 2015
 • Wafanyabiashara wafunga barabara
 • Walalamikia kufungiwa soko la kati kwa mwaka mzima
 • Kwa miaka 20 upinzani hamna walilofanya Moshi mjini
 • Nape awaambia stukeni wananchi,chagueni viongozi watakaowaletea maendeleo
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia vijana wa boda boda ,Stendi Kuu kata ya Mawenzi ambapo aliwaambia kuwa boda boda ni sehemu ya kupata kipato hivyo inabidi wafanye shughuli yao hiyo kwa umakini mkubwa ,ikiwa kudumisha umoja, kufuata sheria, kujisajiri na kutambulika na mamlaka husika ,kuaminika ili waweze kukopesheka.
 Katibu wa Umoja wa Boda Boda Moshi mjini akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano uliofanyika ,Stendi Kuu kata ya Mawenzi Moshi mjini.
 Wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini wakiwa wamefunga njia kuzuia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana usipite mpaka wawasilishe kero yao ya kufungiwa soko kwa mwaka mzima na uongozi wa halmashauri ya mji kwa maelezo ya kupisha ukarabati ambao haujafanyika.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye mabango na wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma risala ya wafanyabiashara wa soko la kati,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanya biashara ambao soko lao limefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuingia kwenye soko la kati, Moshi mjini mkoani Kilimanjaro ambalo lilifungwa kupisha ukarabati ambao mpaka sasa ni mwaka 1 hakuna kilichofanyika na wafanyabiashara wanaishi maisha magumu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa soko la kati ambalo limefungwa kwa mwaka mzima sasa.
 Ukuta wa soko la kati Moshi mjini ukiwa na matangazo yanayozuia kufanya biashara
 Katibu wa Vikoba kata ya Kongoroni Mariam Chawapoma akisoma risala ya kikundi chao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Wanachama wa Vikoba wakishangilia jambo wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wanachama wa Vikoba kata ya Makongoroni ambapo alishiriki kuzindua vikoba 11 vyenye wanachama 330,Kata ya Makongoroni,Moshi mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali baada ya kutembelea kikundi Vijana cha Kata ya Miembeni
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa akina mama Lishe wa Njoro,Moshi mjini.


 Wajasiriamali na mama lishe wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kata yao ya Njoro.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajasiriamali pamoja na mama lishe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ndugu Idd Juma
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatiza kwenye maji wakati akielekea kwenye eneo la mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Moshi mjini Ndugu Aggrey Marealle akihutubia wananchi wa Moshi mjini ambapo aliwaambia kuwa wakati umefika wa kufanya mabadiliko ya kweli kwa kuchagua CCM kuongoza mji wa Moshi.


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Moshi mjini mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambie wastuke sasa wasiendelee kukandamizwa na viongozi wasiojali maendeleo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Moshi mjini kwenye mkutano wa hadhara Bomambuzi viwanja vya shule ya msingi Mandela na kuwaambia kuwa wamekuwa na ushabiki kwa miaka 20 imefika wakati sasa kuamua kuchagua maendeleo kwa manufaa ya maisha yao
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia picha ya gari alilotumia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kabala halijafanyiwa ukarabati na Chuo cha Ufundi Veta, Moshi mjini.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu kuendesha gari alilotumia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kutafuta uhuru,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenye gari alilotumia Baba wa Taifa wakati wa harakati za kutafuta uhuru.


Wananchi wakiuaga msfara wa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya mkutano kumalizika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mandela,Bomambuzi, Moshi Mjini.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM