• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumapili, 10 Mei 2015

CCM YATANGAZA RATIBA YA VIKAO VYAKE VITAKAVYO FANYIKA DODOMA

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake wa Uenezi Ndugu Nape Nnauye watangaza ratiba za Vikao vya juu vya Chama hicho kuanzia tarehe 18 mpaka 23 Mjini Dodoma.

Tarehe 18 mpaka 19 Mei Kikao Cha Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana
Tarehe 20 Mei kutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Ndg Jakaya Kikwete.
...
Tarehe 21 mpaka 22 kutakuwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Ndg Jakaya Kikwete.

Vikao hivyo ambavyo vitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makao Makuu Dodoma maarufu kama "whitehouse" vinategemea kujadili ajenda zifuatazo.

1. Kuwasilisha na kujadili ripoti ya hali ya siasa nchini.

2. Ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge, urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3. Kupitia Rasimu ya Kwanza ya maboresho ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020.

4. Mapendekezo ya uboreshaji wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

5. Namna ya Ushiriki na Mkakati wa Ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.

Na Sufyan Omar
Share:

MAPACHA WENYE BABA TOFAUTI


1_d262e.jpg
Tukio limetokea New Jersey Marekani kwa mapacha waliozaliwa Januari 2013. Balaa lilianza pale mama mwenye mapacha alipoanza kumdai fedha za matunzo baba wa mapacha. Jambo hilo likafika mahakamani, na mahakama ilipotaka uthibitisho wa uzazi kwa kipimo cha DNA, ndipo ikagundulika, kuwa mama huyo alifanya tendo la ndoa na wanaume wawili tofauti katika wiki moja. Hivyo, kila pacha akawa na baba yake. Mahakama imepitisha hukumu ya baba huyo aliyedhaniwa ni baba wa mapacha, alipe gharama ya matunzo kwa pacha mmoja tu! Chanzo: http://www.dn.se
Share:

KAGAME ALIYAKATAA YA KIKWETE!!!!!, ILA YEYE ANAMHUSIA NKURUNZINZA usome ujumbe wake.

" It is not just about the third term, it is about delivery. If your own citizens tell you we don't want you to lead us, how do you say I am staying whether you want me or not?"- Paul Kagame ( The Citizen, Tanzania, Saturday, 9th May)
Share:

BAADA YA MASAA 48 WAANDAMANAJI KUANZA KUSHUGHULIKIWA BURUNDI


Burundi
Waandamanaji wawasha vizuizi vya barabara mjini Bujumbura
Serikali ya Burundi imewaagiza waandamanaji katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura kusitisha maandamano yao dhidi ya hatua ya rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwezi ujao.
Mamlaka imewapatia waandamanaji hao saa 48 kuondoa vizuizi walivyoweka katika barabara za mji huo.
Hakuna maandamano yanayoendelea leo kufuatia vifo vya waandamanaji wawili lakini waandalizi wake wamesema kuwa maandamano yataendelea siku ya jumapili.
Waandamanaji wawasha vizuizi vya barabara mjini BujumburaWaandalizi wanasema kuwa bwana Nkurunziza anakiuka katiba kwa kuwania muhula wa tatu,lakini mapema wiki hii mahakama ya kikatiba nchini Burundi iliamua kuwa rais Nkurunziza ana haki ya kuwania muhula wa tatu.
Takriban watu 18 wameuawa tangu maandamano hayo yaanze wiki mbili zilizopita.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako.(Muro)
Share:

UKAWA WA UINGEREZA WAJIUZURU BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI


Friday, May 8, 2015

Share:

Jumatano, 6 Mei 2015

NVUA KUENDELEA KUNYESHA HADI MWISHO WA MWEZI


Mkurugenzi Mtendaji wa TMA, Agnes Kijazi
Mkurugenzi Mtendaji wa TMA, Agnes Kijazi
MVUA za masika zinazoendelea kunyesha zinatarajiwa kukatika mwishoni mwa mwezi huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alisema hayo alipokuwa akizungumzia mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.
Alisema ndani ya msimu huu wa mvua kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua nyingi.
"Mfano mvua zilizonyesha Zanzibar zimenyesha kwa muda mfupi, lakini kwa wingi hadi kuleta mafuriko."Zanzibar mafuriko yaliyotokea juzi saa tatu asubuhi kituo cha mamlaka kilipima milimita 196.1. Mei tatu mwaka huu ilinyesha masaa machache kituo kilipima milimita 172.2. Hii ndiyo ilileta mafuriko," alisema Dk Kijazi.
Alitoa angalizo wananchi wajitahidi kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamlaka hiyo ili kuepuka kupata matatizo.CHANZO: HABARI LEO (Muro)
Share:

MEYA YUSUPH MWENDA WA KINONDONI DAR ES SALAAM NI KIBOKO YAO AFRIKA NZIMAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi cheti cha Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyo zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana.
Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora katika Bara la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji mengine mbalimbali.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United Cities and Local Government of Africa- UCLGA) na kupewa jina la Rais wa Angola 'President Jose Eduardo Dos Santos- Africa Mayors Award' ni za mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika.
Tofauti na Tuzo za Tanzania, Tuzo hizi za Afrika zinahusika na Mamlaka ya miji tu.
Tuzo hizi zilikuwa ni katika makundi matatu ambayo ni Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities), Tuzo za Majiji ya Kati (Medium Size Cities) na Tuzo za MajijiMadogo (Small Size Cities).
Tuzo za Majiji Makubwa (Large Size Cities) zimekwenda jijini Accra, Ghana wakati zile za Majiji madogo zimechukuliwa na Praia katika visiwa vya Cape Verde.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilishiriki mashindano ya Tuzo za Meya (Halmashauri Bora za Afrika baada ya kushinda Tuzo za Meya/ Halmashauri Bora Tanzania zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).
Miradi iliyoshindanishwa kutoka Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na ukusanyaji wa mapato na kituo cha Mabasi Sinza. Hata hivyo Manispaa ya Kinondoni ilipimwa katika vigezo vyote vilivyoanishwa na UCLGA.
Zawadi zilizotolewa ni kikombe, Cheti na Fedha tasilimu kiasi cha Dola za Kimarekani 100,000 ambazo sawa na shilingi milioni 200.
Majiji mengine yaliyoshinda yalipata Dola za Kimarekani 200,000 (Sawa na shilingi Milioni 400) kwa Miji Mikubwa na Dola za Kimarekani 50,000 (sawa na shilingi milioni 100 kwa Miji midogo.(Muro)
Share:

UCHAGUZI NI KESHO UINGEREZA


Wagombea nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza
Viongozi wa vyama na wagombea wanafanya kampeni zao za mwisho kuwashawishi wapiga kura wawapigie kura kabla ya kufunguliwa uchaguzi mkuu.
Waziri Mkuu David Cameron ataahidi "kuifanya Uingereza kuwa katika njia ya mafanikio", wakati ambapo kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband ataahidi kuwa na "serikali itakayowajali kwanza wafanyakazi".
Kiongozi wa Lib Dem,Nick Clegg ataahidi hali ya utulivu.
Kura ya maoni inaonyesha hakuna chama kitakachoweza kushinda moja kwa moja kwa wingi wa viti.
Naibu mhariri wa BBC James Landale amesema wanasiasa, wapiga kura na vyombo vya habari wanajaribu kufuatilia kwa kina uchaguzi huo, na kuwafanya wengi kufuatilia kile kitakachotokea iwapo matokeo yatakuwa kinyume na matarajio yao.
"Alhamisi, huenda isiwe mwisho wa mchakato huo wa uchaguzi," amesema.
"Huenda uchaguzi huo ukaenda katika hatua ya pili baada ya kushindwa kumpata mshindi wa moja kwa moja."
Katika habari nyingine za uchaguzi mkuu:
Mgombea wa chama cha UK Independence Party (UKIP) aliondolewa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo baada ya kupigwa picha akimtishia kumpiga risasi mpinzani wake kutoka chama cha Conservative.
Kiongozi wa Labour Ed Miliband amesema haamini kama chama chake kitakopa zaidi ya ilivyokuwa mipango ya chama cha Conservative iwapo kitashinda uchaguzi.CHANZO: BBC (Muro)
Share:

BUMBULI WABARIKI URAIS WA JANUARY MAKAMBA,WASEMA NI SHUJAA WAO


Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia, January Makamba akipokelewa na wazee mara baada ya kuwasili jimboni kwake.
Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia, January Makamba akipokelewa na akina mama na kupewa baraka zake.
Na Raisa Said, Bumbuli.
Wakazi mbalimbali wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoani Tanga wamesema kuwa wapo tayari kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba kama ataamua kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa Uraisi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu. Wakazi hao ambao walionyesha nia yao hiyo katika sehemu mbalimbali alizopita Mbunge huyo katika ziara yake ya siku sita kutembelea jimbo lake iliyoanza Machi 30. Makamba ni mmojawapo wa watu wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ya Urais.
Alipokuwa katika kata ya Tamota, viongozi wa dini walimfanyia maombi maalum ambayo yaliongozwa na Mchungaji Amasia Mweta na Sheikh Amiri Yahaya Shekibula mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutumbiwa na Mbunge huyo kijana. Akihutubia mamia ya wakazi wa Bumbuli katika maeneo yote aliyopita kwenye ziara yake, Makamba aliwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kusema kama sio wao asingeweza kuonekana na kutajwa katika kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa CCM.
Makamba, huku akishangiliwa na wakazi hao wa maeneo hayo, alisema kuwa hakuna namna ambayo unaweza kutengeneza watu kukutaja katika nafasi za juu bila kupitia kwa wananchi kukuchagua katika nafasi ya kuwawakilisha. "Kutajwa si dhambi na kwa kuwa fomu za uchaguzi sio sumu si dhambi pia kuchukua na kuingia katika kinyang'anyiro hicho," alisema na kuongeza kuwa sasa hivi kuna kiu kubwa ya uongozi wa aina mpya na kuna watu wamemuona na kumtaja yeye jambo ambalo si baya.
Nao wananchi , wakiwemo vijana, kina mama na wazee katika maeneo mbalimbali aliyopitia Makamba, walimhakikishia Mbunge huyo kuwa hivi sasa hawatampokea mtu yeyote ambaye atakuja kujipitisha katika jimbo hilo hadi hapo watakapojua hatma ya utekelezaji wa nia ya Mbunge huyo kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM. Nao waumini wa Usharika wa Bumbuli walimtaja Mbunge huyo kuwa jasiri, mweledi na mwenye maono mapana na wakasema wanaahidi kuwa bega kwa bega katika harakati hiyo ya kuwania kuwa mgombea wa CCM.(Muro)
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMATANO

MAGAZETI LEO JUMATANO

Na Awadh Ibrahim

.

Share:

SIXTUS MAPUNDA AMALIZA UKAWA IRINGA VIJIJINI

Tukiwa katika Kata ya Idodi kijiji cha Mapogolo, Jimbo la Isimani, Wilaya ya Iringa Vijijini. Tumepata wanachama wapya 592 kutoka kwenye jamii ya kimasai na ya kimang'ati. Aidha UVCCM itaweka kambi mara baada ya kufunga shule ya sekondari ya Idodi ili tufyatue matofali na kujenga mabweni 12 yaliyo athirika na ajali ya moto. Aluta continua!!
Share:

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI MPYA


Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Rais Jakaya Kikwete amemteua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula (Pichani), kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Pia Rais Kikwete amemteua Mkurugebzi waIdara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Hassan Simba Yahya kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema uteuzi huo umeanza jana.

Taarifa hiyo imesema, Rais amemteua Mzee Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, huku akimteua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga,  Daudi Maayeji kuwa Mkurugenzi wa Jiji la mkoa huo wa Tanga.
Share:

HUYU NDIE MWENYEKITI WA VIJANA WA MKOA ANAE INYIMA UKAWA USINGIZI MBEYA


Tuesday, May 5, 2015
Mwenyekiti  wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UVCCM) Mkoa wa Mbeya , Amani Kajuna, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi katika eneo la Sogea Tunduma wilayani mombaMei 4 mwaka huu.
Wanachama wa ccm na wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Uvccm Mkoa wa mbeya Amani Kajuna katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Sogea Tunduma Wilayani Momba.

Mwenyekiti Kajuna akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika mkutano huo uliofanyika katika eneo la Sogea Tunduma Momba Mkoani Mbeya Mei 4 mwaka huu.


Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa Hasani Nyalile akizungumza katika mkutano huo.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Adia Mamu akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi walifika katika mkutano huo eneo la sogea Tunduma Momba Mkoani Mbeya Mei 4 mwaka huu.
Msanii wa Nyimbo za Asili Awilo akitumbuiza katika mkutano huo.

Mkutano ukiendelea

Kikundi cha sanaa cha Makirikiri kikitoa burudani katika Mkutano huo ulioandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mbeya chini ya Mwenyekiti Amani Kajuna Mei4 mwaka huu.Picha Emanuel Madafa
Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Mbeya(uvccm) umetoa siku tatu kwa Mbunge wa jimbo la momba David Sillinde kuziwasilisha fedha za mfuko wa jimbo kiasi cha shilingi milioni 46 anazodaiwa kuzihafadhi kwa ajili ya kumsaidia kwenye kampeni yake ili zifanyie maendeleo
Akizungumzia hilo, mwenyekiti wa umoja huo, amani kajuna, katika mkutano wa wananchi katika eneo la sogea tunduma wilayani momba, amesema sillinde anapaswa kuziwasilisha fedha hizo kwenye mamlaka husika ili zifanyie shughuli za maendeleo.
''Kiasi hiki cha fedha cha shilingi milioni 46 kinatokana na kodi za wananchi na ni kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo hivyo kitendo cha mbunge kuzikumbatia ni ukiukwaji wa sheria, umoja wa vijana tunamtaka kuziwasilisha fedha hizo ndani ya siku tatu,"
Aidha, mwenyekiti huyo, amechangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika eneo la sogea mjini tunduma.
Mwisho.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu