Jumapili, 10 Mei 2015

CCM YATANGAZA RATIBA YA VIKAO VYAKE VITAKAVYO FANYIKA DODOMA

Chama Cha Mapinduzi kupitia Katibu wake wa Uenezi Ndugu Nape Nnauye watangaza ratiba za Vikao vya juu vya Chama hicho kuanzia tarehe 18 mpaka 23 Mjini Dodoma.

Tarehe 18 mpaka 19 Mei Kikao Cha Sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana
Tarehe 20 Mei kutakuwa na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Ndg Jakaya Kikwete.
...
Tarehe 21 mpaka 22 kutakuwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Ndg Jakaya Kikwete.

Vikao hivyo ambavyo vitafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makao Makuu Dodoma maarufu kama "whitehouse" vinategemea kujadili ajenda zifuatazo.

1. Kuwasilisha na kujadili ripoti ya hali ya siasa nchini.

2. Ratiba ya mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge, urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3. Kupitia Rasimu ya Kwanza ya maboresho ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020.

4. Mapendekezo ya uboreshaji wa mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

5. Namna ya Ushiriki na Mkakati wa Ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu.

Na Sufyan Omar
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu