Unordered List


MAPACHA WENYE BABA TOFAUTI


1_d262e.jpg
Tukio limetokea New Jersey Marekani kwa mapacha waliozaliwa Januari 2013. Balaa lilianza pale mama mwenye mapacha alipoanza kumdai fedha za matunzo baba wa mapacha. Jambo hilo likafika mahakamani, na mahakama ilipotaka uthibitisho wa uzazi kwa kipimo cha DNA, ndipo ikagundulika, kuwa mama huyo alifanya tendo la ndoa na wanaume wawili tofauti katika wiki moja. Hivyo, kila pacha akawa na baba yake. Mahakama imepitisha hukumu ya baba huyo aliyedhaniwa ni baba wa mapacha, alipe gharama ya matunzo kwa pacha mmoja tu! Chanzo: http://www.dn.se

Chapisha Maoni

0 Maoni