Jumatatu, 15 Juni 2015

KATIBU MKUU WA CCM, KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA, NI KWA KUTEMBELA WILAYA YA BIHARAMULO


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdlrahman Kinana akikagua chanzo cha maji cha mradi wa maji wa Nyakahura wilayni Biharamulo, mwishoni mwa ziara yake mkoani Kagera.
Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itiadi na Uenezi Nape Nnauye.

Katibu Mkuuu wa CCM Abdulrahman Kinana amehitimisha ziara yake hiyo ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Kagera kwa mafanikio makubwa.

Katika ziara hiyo Kinana amemaliza  ziara hiyo leo Julai 14, 2015, baada ya kutembea jumla ya kilometa 3374, akiwa ametembelea majimbo yote tisa katika wilaya zote nane za mkoa huo.

Ziara hiyo imeonyesha kuwa na mafanikio makubwa kwa kuingiza CCM wanachama wapya  5678 kati ya wanachama 488 wakiwa wamehama kutoka vyama vya upinzani vikiwemo Chadema, CUF na NCCR Mageuzi.

Katika ziara ya mkoa wa Kagera, ambako amesafiri kwa gari nchi kavu na mitumbwi kwenda katika visiwa vitano, amefanya mikutano 74 kati yake ikiwemo mikutano 63 ya hadhara na kuzindua miradi 46, 41 ikiwa ni yamaendeleo ya wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa maji wa Nyakahura wilayani Biharamulo,  mwishoni mwa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, mkoani Kagera leo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongera. Akikagua mradi huo wa maji Kinana ameonyesha kukerwa baada ya kubaini kwamba mradi huo umefanywa vibaya na kutosaidia wananchi kupata maji kama ilivyotarajiwa kutokana na sababu nyingi ikiwemo ramani ya mradi huo kuchorwa vibaya licha ya kutengewa sh. bilioni 1.4.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katikamkutano wa hadhara uliofanyika leo Juni katika Biharamulo mjini, mwishoni mwa ziara yake katika mkoa wa Kagera.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano huowa wa Kinana, Biharamulo mjini.
 Wananchi wa Biharamulo mjini wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara Biharamulo mjini.
 Vijana wakitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika Biharamulo mjini mwishoni mwa ziara yake mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi baada ya mapokezi yaliofanyika katika kijiji cha Nyabugombea, wakataai akiingia katka wilaya ya Biharamulo mwishoni mwa ziara yake mkoani Kagera.
 Mamia ya wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyakahura wilayani Biharamulo mwishoni mwa ziara yake mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara aliofanya katikakijiji cha Nyabungombea wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi waliomsimamisha njiani wakati msafara wake ukitona Nyabungombe kwenda Biharamulo mjini mkoani Kagera.
 Meneja wa mradi wa Umeme wilayani Biharamulo, Ernest Milyango akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipokagua mradi huo mwishoni mwa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na Uhai wa Chama mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimhoji jambo meneja wa mradi wa umeme wilayani Biharamulo mkoani Kagera, Ernest Milyango alipokagua mradi wa umeme wa wilaya hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiagana na Meneja wa Mradi wa umemewa Biharamulo Elnest Milyango baada ya kukagua mradi huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitzama chumba cha kupumzikia kina mama waliojifungua, alipotembelea ujenzi wawodi ya wazazi ya katika kituo cha afya cha Rukaragata, wilayani Biharamulo mkoani Kagera, leo Juni 14, 2015, akia katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Kagera. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupachipa dirisha kwenye shule ya msingi ya Kiislamya Al Rahman katika wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua shule ya msingi ya Kiislam ya Al Rahman mjini Biharamulo mkoani Kagera. Kulia ni Mkurugenzi wa shule hiyo, Sheikh  Masoud Saadan
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki kuomba dua baada ya kuzindua shuke ya msingi ya Kiislam ya Ar Rahman wilayani Biharamulo mwishoni mwa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCMna uhai wa Chama mkoani Kagera. 
 
 na Sufyan Omar
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM