Jumatano, 15 Julai 2015

MAGUFULI AITEKA DAR ES SALAAM MAELFU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA


 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam akimpokea Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji hilo.
 Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam.

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM ,Ndugu Nape Nnauye akizungumza na wakazi wa Dar es salaam waliojitokeza kwenye uwanja wa ndege kumpokea mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar Es Salaam Ramadhan Madabida akizungumza na wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kumpokea mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli.
 Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.

 Mgombea Mwenza wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wakazi wa Dar es Salaam waliokuja kuwapokea uwanja wa ndege Dar es Salaam.
 
Wakazi wa Mbagala wakiwa wamejipanga barabarani kumuona mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli .
 
Katibu wa Itikadi na uenezi Nape Nnauye akiwasili kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala akiwa kwenye usafiri wa Boda boda.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Mbagala Zakheem tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa Dar es Salaam.
 
Dk. John Pombe Magufuli mgombea wa Urais kupitia CCM akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Idd Azzan wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano Zakheem Mbagala.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Dar es Salaam.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwatambulisha viongozi mbali mbali waliomsindikiza mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli kwenye viwanja vya mikutano vya Mbagala Zakheem.


 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kabla ya kumkaribisha mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kujitambulisha na kuwasalimia wakazi wa Dar es Salaam.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala kwenye mkutano wake wa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo aliahidi kuwatumikia wananchi na kutenda haki.
 Mgombea Mwenza wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtemvu kwenye mkutano wa hadhara wa kumtambulisha mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais Mhe. john Pombe Magufuli
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam. 

 Ndugu, Jamaa na wafanyakazi wenzake Dk. John Pombe Magufuli wakisikiliza kwa makini hotuba kwenye mkutano huo.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za tumba pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye kwenye jukwaa la bendi ya TOT mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuhutubia  wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye mkutano wa Dk. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam 
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu