Unordered List


NAPE AITAJA TANO BORA YA WAGOMBEA URAISI CCM



Katibu wa NEC itikadi na uwenezi wa CCM ndugu NAPE NNAUYE, azungumza na waandishi wa habari  leo asubuhi, kwa kutoa taarifa sahihi za wagombea walioteuliwa katika katika tano bora, ndugu Nape aliwataja wagombea hao kuwa ni Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ndugu Bernard Membe, Dk Asha Rose Migiro, Amina salumu, Mh: January Makamba na Dk: John Magufuli. Majina hayo yatapelekwa kwenye halmashauri kuu ya taifa ya CCM kujadiliwa na kupata 3 bora ya wagombea,ambayo yatapelekwa katika mkutano mkuu wa Taifa kwa kumpata mmoja atakae kuwa mgombea uraisi kwa CCM

Chapisha Maoni

0 Maoni