Jumapili, 9 Agosti 2015

ASENGA ABUBAKAR ASHINDA KWA KISHINDO UBUNGE WA KILOMBERO

 
Matokeo ya kura za maoni kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi kwa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge yameendelea kuwa mwiba mkali kwa waliokuwa wakitetea nafasi hizo 
Mbunge wa Kilombero Abdu Mteketa
Wilayani kilombero aliyekua mbunge wa jimbo hilo Abdul Mteketa amelazimika kuyakimbia matokeo baada ya kubaini ameangushwa katika kutetea nafasi hiyo.

Hali hiyo imejitokeza wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ndani ya CCM, wa kuwatafuta wawakilishi wa ubunge na udiwani watakaopeperusha bendera ya CCM, katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu,

Mbunge wa Kilombero Abdu Mteketa alilazimika kususia zoezi hilo baada ya kubaini nafasi aliyokuwa akiwania kuitetea, kuchukuliwa na kijana mdogo, Abubakar Asenga aliyetumia nafasi hiyo kuwaomba wana ccm kuvunja makundi yaliyojitokeza wakati wa kura za maoni na kuwa wamoja ili kufanikisha ushindi na maendeleo ya chama hicho na taifa kwa ujumla
Abubakar Asenga ameshinda kura hizo za maoni za kuwania ubunge kilombero kwa kupata kura 9629,dhidi ya mpinzani wake wa karibu Abdalah Lyana aliyepata kura 3999 huku mteketa aliyekuwa akiwania nafasi hiyo akishika nafasi ya tatu kwa kuambulia kura 2646 na alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi iliita bila majibu,

Katibu wa CCM, wilaya ya kilombero Bakari Mfaume pamoja na kushukuru zoezi hilo kumalizika salama,amesema ofisi yake ipo tayari kupokea malalamiko ya wanaodhani wameonewa katika uchaguzi huo ili wafanyie kazi.

Katika maeneo mengine ya uchaguzi ndani ya ccm mkoani Morogoro,baadhi ya waliokuwa wabunge wamefañikiwa kutetea nafasi zao kwa kushinda kura za maoni,akiwemo aliyewahi kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Haji Mponda aliyeshinda jimbo la ulanga magharibi,Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa umma,Celina Kombani akishinda ulanga mashariki,Ahmed Shabiby akishinda jimbo la Gairo na Abdulaziz Abood akishinda Morogoro mjini,huku jimbo wazi la kilosa ambalo awali lilishikiliwa na Mustafa Mkulo ambaye hakugombea tena akishinda Mbaraka Bawaziri.

Walioangushwa ni pamoja na naibu waziri wa maji na mbunge wa mvomero amos makala na nafasi hiyo kuchukuliwa na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo suleiman Sadiq Murrad,aliyewàhi kuwa Naibu Waziri wa afya Dkt. Lucy Nkya akianguka jimbo la Morogoro kusini Mashariki na nafasi yake kuchukuliwa na Mgumba,

Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Morogoro Innocent Kalogores akiangushwa jimbo la Morogoro kusini na nafasi yake kuchukuliwa na Mbena na aliyekuwa mbunge wa mikumi Abdusalam Ameir akiangushwa jimbo la Mikumi na nafasi hiyo kuchukuliwa na Jonas Estomih nkya.

CHANZO EATV
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu