Jumatano, 26 Agosti 2015

MAGUFULI ASIMAMIA SHOW PEKE YAKE TUNDUMA

  •  Wananchi wamkubali kwa uwezo wake wa kujieleza, sera ,ilani na mipango ya kuleta maendeleo huku akiwa yeye mweyewe bila kuwa na msururu wa watu wa kutanguliza kuhutubia.
  •  Ahutubia mikutano mikubwa  Laela, Tunduma,Isongile,Vwawa
  •  Asema ataondoa urasimu mwingi serikalini
  •  Elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne
  •  Kuboresha huduma za afya haswa upatikanaji wa madawa
  •  Kuboresha malipo pamoja na haki za walimu
  • Anaamini kwa anachokisema kwani amekuwa mfano katika kutimiza wajibu wake.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa shule ya msingi Tunduma tayari kuhutubia mkutano wa kampeni.
 Wananchi wa Tunduma wakizingira gari la mgombea wa urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati akiwasili kwenye uwanja wa mkutano Tunduma.
 Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoa wa Mbeya Ndugu Bashiru Madodi akizungumza kabla mgombea wa urais kupitia CCM Dk.John pombe magufuli hajahutubia wakazi wa Tunduma.
 Wakazi wa Tunduma wakiwa wamefurika kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli
 Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji mdogo wa Tunduma .
 Ni shamra shamra kila kona Tunduma
 Hivi ndivyo Tunduma ilivyofurika
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la tunduma kupitia CCM Frank Sichalwe akitaja mambo ya msingi muhimu ambayo angependa wananchi wa Tunduma wayapate, alisema wananchi hao wanahitaji huduma bora ya afya, magari ya wagonjwa, zimamoto, kiwanja cha michezo, kushoto ni mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiandika hayo mahitaji.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akionyesha msisitizo wa yale anayoyasema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Tunduma.
 Hii ni Barabara kuu inayounganisha Tunduma na Rukwa ambayo ni moja ya barabara nyingi nchini zilizojengwa chini ya usimamizi wa Dk. John Pombe Magufuli
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa, Mhe. William Lukuvi akihutubia wakazi wa Laela kabla ya kumkaribisha mgombea wa urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kuhutubia kwenye uwanja wa Laela A.
 Wananchi wa Laela wakimsikiliza mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kwa kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisali sala maalum na watawa wa kanisa katoliki waliofika kwenye mkutano wake Laela, kulia ni Sister Christiana na kushoto ni Emiciliana, mwingine pichani ni Mhe.William Lukuvi.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na kijana mwenye ulemavu Joseph mkazi wa Laela mara baada ya kumaliza mkutano.
 Dk. John Pombe Magufuli akiwapa mikono ya heri madiwani wanaogombea udiwani la KwelaShare:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu