• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Alhamisi, 24 Septemba 2015

MAMA SAMIA ACHANJA MBUGA KUPIGA KAMPENI HANDENI, KILINDI, KITETO NA NCHEMBA

                       

 Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, alipohutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la  Handeni mkoa wa Tanga.
                                                Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Handeni katika mkutano wa hadhara uliofanyika Handeni mkoani Tanga.
 Wagombea Udiwani katika kata mbalimbali jimbo la Handeni, wakinyoosha mikono, waliponadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo la Handeni mkoani Tanga. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Angella Kizigha.
 Mwandishi wa habari aliyeko katika msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wa kampeni za CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Handeni mkoa wa Tanga.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akionyesha ilani ya CCM, kabla ya kumkabidhi Mgombea Ubunge jimbo la Handeni Vijijini, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga. 
 Aliyekuwa Muomba ridhaa ya CCM, kugombea Ubunge jimbo la Handeni Vijijini, John Sallu, akimnadi Mgombea aliyepitishwa na CCM katika kura za Maoni, Mboni Mhita, katika mkutano wa  kampeni uliofanyika katika jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga.
 Mgombea Ubunge jimbo la Handeni Vijijini, Mboni Mhita akihutubia mkutano wa kampeni katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgombea Ubunge jimbo la Handeni Vijijini, Mboni Mhita, katika mkutano wa kampeni uliofanyika, katika jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga leo.
 Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipopita katika kijiji cha Msente, akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Kilindi mkoani Tanga. 
 Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipopita katika kijiji cha Kwediboma, akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Kilindi mkoani Tanga. 
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgombea Ubunge jimbo la Kilindi, Omar Kigua, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Tanga.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika  katika jimbo la Kilindi mkoa wa Tanga.
 Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kibirashi leo katika jimbo la Kilindi mkoa wa Tanga.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizmnadi Mgombea Ubunge jimbo la Kilindi mkoani Tanga, Omari Kigua katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi waliozuia msafara wake wakati akitoka Kilindi kwenda Kiteto kuhutubia mkutano wa kampeni.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi waliozuia msafara wake wakati akitoka Kilindi kwenda Kiteto kuhutubia mkutano wa kampeni.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Kiteto kabla ya kwenda Uwanjani kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Kiteto
 Wananchi wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kiteto
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Kiteto mkoani Manyara.
 Wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara.
 Vijana wakijitahidi kukaa popote kuhakikisha wanamuona Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi Mama Samia, uliofanyika leo katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara.
 Mgombea Mwenza a Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Emmanuel Papian John, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo.
 Wagombea wa Udiwani katika jimbo la Kiteto wakinyoosha mikono baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanyika.
 Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara.
 Mbunge wa Nchemba, Juma Nkamia akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Dodoma
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Nchemba mkoani Dodoma.
Baadhi ya wagombea Udiwani jimbo la Nchemba, wakinyoosha mikono, baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoa wa Dodoma. 

Na Sufyan Omar
Share:

Jumatano, 23 Septemba 2015

JANUARY MAKAMBA AZUNGUMZIA MWENENDO WA KAMPENI 2015


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Mapinduzi kinapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa.

Mwenendo wa Kampeni

Kwa kifupi, Mgombea Urais, Ndugu John Pombe Magufuli na Mgombea-Mwenza Ndugu Samia Suluhu Hassan, wanaendelea vizuri na kampeni. Kila mmoja anafanya mikutano na wananchi kati ya 8 hadi 11 kwa siku na kukutana na maelfu kwa maelfu ya wananchi. Tunawashukuru wananchi wanaokuja kwenye mikutano yetu. Tunawashukuru pia makada wa CCM wanaojitolea kwa hali na mali kukipigania Chama cha Mapinduzi na kumtafutia kura Ndugu Magufuli.

Tunaridhika sana na mwenendo wa kampeni yetu. Katika nusu hii ya pili ya kampeni tutaongeza kasi na msukumo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mbinu na mikakati mipya.

Midahalo ya Wagombea

Tumeshangazwa na kauli ya Ndugu Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania kwamba CCM haijathibitisha kushiriki mdahalo. CCM ilipokea mwaliko wa MCT na kuijibu kwa barua ya tarehe 13 Septemba 2015 yenye kumbukumbu CMM/OND/M/190/132 iliyosainiwa na Ndugu Stephen Msami, Msaidizi wa Katibu Mkuu. Barua hiyo ilipelekwa na kupokelewa kwa dispatch ambayo nakala yake tunayo. Baada ya hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, alifanya kikao na wawakilishi wa MCT katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba ili kutaka kujua zaidi na kutoa maoni ya CCM kuhusu utaratibu mzima wa mdahalo. Katika kikao hicho, ambapo MCT iliwakilishwa na Afisa wake, Ndugu Allan Lawa, pamoja na Ndugu Tido Mhando, CCM ilithibitisha tena kushiriki mdahalo. Tatu, tarehe 16 Septemba 2015, CCM ilitoa kauli rasmi, iliyosainiwa, ikithibitisha kushiriki mdahalo. Kauli ya Ndugu Mukajanga inalenga kuwasaidia kisiasa wale ambao hawajathibitisha au hawana nia ya kuthibitisha kushiriki. Kwa msingi huu, tunaamini ni vyema mdahalo huu ukaandaliwa na ushirika wa taasisi mbalimbali zilizokuwa na nia ya kuandaa midahalo, (kama vile CEO Roundtable, UDASA, Twaweza) ili kuiondolea uwezo taasisi moja, au kikundi cha watu wachache, kuhodhi na kuwa na ukiritimba kwenye jambo hili kubwa na muhimu.

CCM inapenda kusisitiza yafuatayo:

1. Ndugu Magufuli amekubali kushiriki mdahalo wa wagombea Urais
 2. Mdahalo uwashirikishe wagombea wenyewe na sio wawakilishi wao.
 3. Wagombea wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki.

Tunapozungumzia mabadiliko katika nchi maana yake ni utayari wa kufanya mambo mapya yenye tija ambayo hayajawahi kufanyika, ikiwemo mdahalo wa wagombea Urais. Wanaohubiri mabadiliko huku wakiogopa kushiriki mdahalo wanahubiri mabadiliko hewa.

Utafiti wa TWAWEZA

CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoa ushindi wa asilimia 65 kwa Ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya asilimia 25 za Mgombea wa UKAWA. Hatukushangazwa na matokeo ya utafiti huu kwasababu tano:

1. Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM hatukumteua kwasababu tuliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi watamchagua.

2. Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM tunafanya utafiti wetu wa ndani wa kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu tuanze utafiti wetu mwishoni mwa mwezi Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.

3. Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda. Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao wanawaelewa.

4. Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.

5. Tunaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha uchaguzi iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye, kutokana na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa viongozi wa muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na Dr. Wilbrod Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya yamepunguza imani ya wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.

Lakini vilevile matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumkabidhi nchi.

Sisi kama CCM kuna baadhi ya mambo tumeyachukua katika utafiti huu na tutayafanyia kazi ili kujihakikishia ushindi.

Tumeshangazwa na taharuki, hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huu. CCM ilitegemea kwamba jamii ya wasomi na wanaharakati ingefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa unaoanza kujitokeza hapa nchini ili siku zijazo tujikite katika kurekebishana kwenye kanuni za utafiti na ithibati na uhakiki wa ubora. Tunasikitika kwamba yanawekwa mazingira ya kutisha na kukatisha tamaa (atmosphere of intimidation) kwa watu wanaotaka kufanya tafiti za kisiasa nchini.

Utafiti ni sayansi. Matokeo ya utafiti hupingwa kwa matokeo ya utafiti mwingine, sio kwa kuponda tu au kwa matusi na vitisho. Ni vyema tukajifunza kupokea habari mbaya bila taharuki.

Itakumbukwa kwamba, mwezi Agosti 2010, taasisi ya utafiti ya kimataifa ya Synovate ilitoa utafiti ikionyesha kwamba CCM itashinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa asilimia 61. Baadhi ya wana-CCM hawakufurahishwa na matokeo ya utafiiti huo kwasababu waliamini kwamba ushindi wetu ulikuwa ni mkubwa zaidi. Wapinzani waliwalaani, kuwatukana na hata kutaka kuwashtaki Synovate. Kwenye matokeo halisi ya kura, CCM ilipata asilimia zilezile 61 zilizotabiriwa na Synovate.

Ni vyema kuweka akiba ya maneno kwenye masuala haya.

Imetolewa na:


 January Makamba
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni

Na Sufyan Omar
Share:

MAGUFULI ALIVYOISIMAMISHA GEITA

Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Karangalala tayari kuhutubia wakazi wa Geita mjini.

 Umati ukiwa umefurika kumsikiliza mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Karangalala,Geita mjini.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Geita mjini kwenye uwanja wa Karangalala ambapo aliwaeleza wakazi wa mji huo kuwa atahakikisha viwanda vinajengwa , wacimbaji wadogo wadogo wanapata maeneo ya kuchimba, ataboresha maslahi ya wafanyakazi , kuhakikisha madawa na huduma za afya zinakuwa bora zaidi na elimu bure kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha nne.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake wa kampeni.
           Bbbbb.       
Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge wa Jimbo la Geita mjini Ndugu Costantine John Kanyansu kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Karangalala mjini Geita.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliakiwa jukwaani na wanachama waliohamia CCM.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa jukwaani wakati Mwana F.A akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Geita.
 Wasanii wa Bongo flava wakipiga push up kumuunga mkono Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufulikwenye uwanja wa Karangalala.
 Mabango ya Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli yakiwa yametanda kila kona ya mji wa Geita.


 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Musukuma pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dk. Anthony Diallo kabla ya kuanza kuhutubia wakazi wa mji wa geita waliofurika kwenye uwanja wa Karangalala.
 Burudani kutoka kikundi cha Geita zilivutia sana.

 Yamoto Bendi wakitumbuiza kwenye mkutano wa Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli,Geita mjini.

 Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia wakazi wa Geita mjini kwenye mkutano wa kumnadi Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia wakazi wa Geita mjini ambao aliwahimiza wananchi hao kumpigia kura Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufulina wabunge na madiwani wote kutoka CCM.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaji Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa Geita kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiondoka uwanjani mara baada ya kumaliza kuhutubia wakazi wa Geita mjini.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wapenzi na mashabikia wa CCM walioitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Vijana wakiondolewa uwanjani na polisi baada ya kubainika wanaleta fujo.

Na Sufyan Omar
Share:

MAGUFULI AUSTUA ULIMWENGU BAADA YA KUPIGA PUSH UP KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KARAGWE


 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgombea ubunge jimbo la Nkenge kupitia CCM Balozi Dk. Deodorus Kamara mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mkutano maarufu kama uwanja wa Chakaza ,Bunazi wilaya ya Misenye.
 Baadhi ya wagombea wa udiwani wakiwa tayari kujinadi kwenye mkutano wa kampenii za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa maarufu kama Chakaza,Bunazi wilaya ya Misenye.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Alhaji Abdallah Bulembo akimtambulisha mgombea wa ubunge jimbo la Nkenge
Balozi Dk. Deodorus Kamara kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa maarufu kama Chakaza.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bunazi wilaya ya Misenye ambapo aliwaahidi kuondoa kodi zote zisizokuwa na maana kwa mkulima wa kahawa.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihtubia wakazi wa Misenye na kuwaahidi kuwa ataondoa vikwazo kwa wafanya biashara ili waweze kufanya biashara vizuri.
 Wakazi wa Bunazi wakiwa wengi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo pia ulihutubiwa na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Sheikh wa Wilaya ya Misenye Alhaj Abdul Chagulani akimuombea dua njema Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipokea dua ya sheikh mkuu wa wilaya ya Misenye Alhaj Abdul Chagulani.
 Wakazi wa Karagwe wakimsubiri Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kuwahutubia kwenye viwanja vya Changarawe Kayanga wilayani Karagwe.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Karagwe ambapo aliwaahidi kutekeleza anayo ahidi ikiwemo ukamilishwaji wa ujenzi wa barabra kwa kiwango cha Lami.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga push up mbele ya maelfu ya wakazi wa Karagwe kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Changarawe,Kayanga.


 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu Alhaji Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa Kyerwa kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Rumanyika kata ya Nkwenda wilaya ya Kyerwa.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kyerwa kwenye mkutano wa kuomba kura kwa wananchi.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Kyerwa Ndugu Innocent Balikwate kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Rumanyika.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
 Wakazi wa Benako wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati akielekea kwenye mkutano wa kampeni Ngara.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Alhaj Abdallah Majura Bulembo akihutubia wakazi wa Ngara kwenye uwanja wa posta ya zamani.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ngara mjini
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubiawakazi wa Ngara ambapo aliwaahidi wakazi hao kuwa atashughulikia kupunguza kodi zinazo mkandamiza mkulima.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimndadi mgombea wa ubunge jimbo la Ngara Ndugu Alex Raphael Gashaza .


 Mbunge Mteule anayewakilizsha Wazazi Oliva Semguruka akihutubia kwenye mkutano wa Kampeni za CCM kulia ni Halima Bulembo Mbunge mteule kupitia vijana 
 Mbunge Mteule anayewakilizsha Wazazi Oliva Semguruka akihutubia wakazi wa Ngara ambapo aliwaambia wakina mama kushikana na kuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo na kuitunza amani iliyopo.
 Mbunge mteule atakayewakilisha vijana Ndugu Halima Bulembo akihutubia wakazi wa Ngara kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea ubunge wa jimbo la Ngara Ndugu Alex Raphael Gashazaakihutubia wakazi 
wa Ngara mjini wakati wa mkutano za CCM za kumnadi Dk.John Pombe Magufuli.


Na Sufyan Omar
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu