Jumapili, 20 Septemba 2015

SHAKA: SUMAYE na Lowassa kama “pwagu na pwaguzi”

Na Mwandishi Wetu,Mtwara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye  uamuzi wake wa kusaidia  kumfanyia kampeni mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa ni sawa na pwagu kumfanyia kampeni  pwaguzi.

Shaka alitoa matamshi hayo jana katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni za ubunge na madiwani  jimbo la Mtawara vijijini  wakati akimdani mgombea wa jimbo hilo kupitia CCM Hawa Abdulrahaman Ghasia uloiofanyika katika kijiji cha Mo Pacha Nne Mkoani hapa.

Alisema ni kituko kwa viongozi hao  ambao waliwahi  kukabidhiwa dhamana za uongozi wa juu na serikali ya CCM na kushindwa kuleta ufanisi na matokeo chanya na  sasa wakiwa Chadema  waghilibu wananchi  wakidai  wana ubavu wa kuleta  mabadiliko na maendeleo.

“Sumaye anapomfanyia kampeni  Lowassa awe Rais ni sawa na pwagu  kumfanyia kampeni pwaguzi, hawajui wafanyalo , hawatambui   kama majina yao hayaheshimiki mbele ya jamii ,walipewa nafasi za juu wakashindwa kuisukuma  nchi kimaendeleo na sasa wanachokifanya ni upekepeke na utapitapi ” Alisema Shaka huku akishangiliwa.

Alisema Sumaye akiwa Waziri Mkuu wa Serikali chini ya Rais Benjamni Mkapa  usimamizi wake alizisibabishia halmashauri nyingi za wilaya nchini kupata hati chafu kwa mujibu wa ripoti za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali.

Aidha shaka alifichua  siri ya jina la Lowassa kukatwa na vikao vya  CCM katika mbio za urais  huku akisema halikuwa jambo la bahati mbaya ila uamuzi huo ulifanyika kwa lengo la kukipa  hadhi na heshima Chama Cha Mapinduzi mbele ya wananchi na jamii ya kimataifa.

“CCM ni chama kinachoheshimika kitaifa, kikanda na kimataifa, hakiwezi kusimamisha  mgombea anayetiliwa shaka ,anayetazamwa kwa jicho la hofu ndani ya nje ya mipaka yetu, tuliamua, tulikusudia, tukalikata jina lake si kwa  bahati mbaya bali tulikusudia” Alisisitiza Shaka.

AlisisitizaTanzania haiwezi kupata  alama ya Rais ila inahitaji Rais mwenye viwango, anayeheshimu  miiko ya uongozi , mwenye kuzingataia maadili na  aliyeshiba uzalendo ambaye akishiakuwa na utayari wa  kulitumikia Taifa na watu wake kwa uadilifu na utii.

Katibu Mkuu huyo wa UVCCM alisema  CCM ilijua Lowassa akitemwa  hatabaki ila atakwenda upinzani   ili kukamilisha  kwa lengo la kuusambaratisha , kuumaliza ,kuudhofisha na kuuzika usiwepo kama inavyotokea sasa .

Alisema kuhamia Chadema kumezuia tafran kati ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Wilbroad Slaa, mwanzo wa kuhasimiana kwa Profesa Lipumba na Maalim Seif Sharif Hamad huku Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi James Mbatia akitu na Katibu Mkuu wake Mosena Nyambabe.

“Hesabu zetu zimetoa majibu chanya, mwaka huu ndiyo mwanzo na mwisho wa kelele za upinzani uchwara, tumewatupia makapi wakafikiri  wamepata malighafi, hii ndiyo CCM aliotokana na TANU na ASP”Alijigamba Shaka

Shaka aliwataka wananchi wa jimbo la Mtwara vijijini kumchagua Hawa Ghasia awe mbunge wao  kutokana na uwezo mkubwa aliouyesha alipopewa dhamana  ya kusimamia Tawala za mikao na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) huku akikomesha vitendo vya wizi ,ufujaji wa fedha za umma pia  Halmashaugi  zikipata hati safi.

“Huyu ni mwananmke wa shoka, hodari na makini, msikubali kupoteza hazina inayotegemewa na Taifa, mpeni kura  ni muaminifu, muadilifu anayependa ushirikiano, habagui wala hachagui ”Alisisitiza Shaka.

Akimnadi mgombea urais wa CCM Dk John Magufuli , Shaka alisema ni kiongozi wa  dhamira, mchapaka kazi , msimamiaji wa sera, malengo na mipango endelevu hivyo anastahili kumrithi Rais Jakaya Kikwete na kuwa Rais wa awamu ya tano ifikapo oktoba 25 mwaka huu akisema watanzania hawatajuta uamuzi wa kumpa dhamana hiyo.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu