• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumamosi, 31 Desemba 2016

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN ATOA SALAMU YA MWAKA MPYA 2017

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa salamu za mwaka mpya wa 2017 kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla,   ambapo Dkt Shein ameuombea 2017 kuwa mwaka wa mafanikio na amani katika salamu hizo alizotoa alipokuwa akifanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Bi. Imane O.Duwe leo katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.  Picha na IKULU
Share:

Ijumaa, 30 Desemba 2016

UVCCM CUP YAIVA, KAIRUKI AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA VIJANA WA SAMETukiwa tunaelekea katika michuano ya  LIGI YA VIJANA CUP itakayo anza kurindima katika ngazi za Wilaya,Mkoa,Kanda hadi kufikia kilele chake Taifa Mnamo tareh 5/02/2017.

Mapema ya leo Mh Angellah Kairuki Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi ambae pia ni kamanda wa Uvccm Wilaya ya Same akiwa ndiye mzamini rasmi wa ligi Wilayani humo amekabidhi vifaa vya Michezo kwa timu 49 zitakazoshiriki ligi ya mpira wa miguu Wilayani Same.

    Akizungumza mara baada ya kugawa vifaa ivyo Mh Angellah Kairuki Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi ambae pia ni kamanda wa Uvccm Wilayani humo akizungumza na viongozi na wachezaji wa timu hizo pamoja na kuwatakia maandalizi mema ya michuano hiyo  amewaeleza yakuwa  ''Ufunguzi wa ligi hii unarajiwa kufanyika tar 3/01/2017 ambapo Mgeni Rasmi atakuwa ni  Mh Anastanzia Wambura Naibu waziri Vijana, Habari, Utamaduni na Michezo''.

 Mh Angellah Kairuki Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi ambae pia ni kamanda wa Uvccm Wilaya. Na ndie mdhamini wa ligi hii Wilayani humo wa tatu kushoto akikabidhi jezi mbalimbali kwa viongozi wa kamati ya ligi wilayani Same.
  Mh Angellah Kairuki Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi ambae pia ni kamanda wa Uvccm Wilaya. Na ndie mdhamini wa ligi hii wilayan Same wa nne kushoto akikabidhi vifaa vya kingo za uwanja kwa viongozi wa kamati ya ligi wilayan same.
  Mh Angellah Kairuki Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi ambae pia ni kamanda wa Uvccm Wilaya. Na ndie mdhamini wa ligi hii wa Nne kushoto akikabidhi Vibendera kwa malefa watakao ongoza Vijana Cup Wilayan Same.
Jezi na Vifaa mbali mbali vya michezo vilivyo tolewa leo na  Mh Angellah Kairuki Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi ambae pia ni kamanda wa Uvccm Wilaya. Na ndie mdhamini wa ligi wilayani Same itakayo funguliwa na  Mh:Anastanzia Wambura Naibu waziri Vijana, Habari, Utamaduni na Michezo Tareh 3mwezi 1mwaka2017.


Share:

Alhamisi, 29 Desemba 2016

UVCCM WAMFARIJI MSANII BEN WA BONGO MOVIE

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa (MCC/MB) Leo ameongoza  ujumbe wa viongozi wa UVCCM kumfariji na kumpa pole msanii wa maigizo ndg Abdul Ahmad jina la Usanii Ben Serengo nyumban kwao Kigogo Jijini  Dar Es Salam, aliyepata ajali ya gari tareh 25 siku ya  skukuu ya Christmas


 '' UVCCM inathamini sana mchango wa wasanii wa ndani na  inaguswa na  changamoto na matatizo mbali mbali yanayopata  wasanii hivyo Jumuiya itaendelea kuwa nao karibu kwa kuzingatia umuhimu wao katika jamii na Chama Cha Mapinduzi. Alisema Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Mhe:Sadifa Juma Khamisi(MCC/MB) alipokwenda Kumjulia Hali Msanii wa Bongo Movie Abdul Ahmad jina maarufu Ben Serengo wa pili kulia  na wa tatu kulia ni Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Sadifa Juma Khamisi(MCC/MB)  wa nne kulia akitizama picha mbali mbali za tukio la ajali Msanii wa Bongo Movie Abdul Ahmad jina maarufu Ben  Serengo wa Tatu kulia iliyotokea tareh 25 Siku ya Skukuu ya Christmas.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa  Sadifa Juma Khamisi(MCC/MB) wa Tatu kushoto akizungumza na mama wa msanii Bi Jasmin Rajabu Hatia Mara baada ya kutoka kumuona mgonjwa.
Share:

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MAARUFU WA CHATO ADMIRABILIS MBABE MANYAMA (82) CHATO MKOANI GEITA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole   Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita
 Mdogo wa Marehemu Deodatus Manyama kimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapa pole na  kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani mara baada ya kutoa pole. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi akitokea katika msiba huo Chato mkoani Geita.
PICHA NA IKULU
Share:

Jumatano, 28 Desemba 2016

KHATIB: APITISHWA KUWANIA UMEYA WA MANISPAA YA MJINI Z'BAR

 

Na Is-haka Omar,  Zanzibar
MADIWANI wa Manispaa ya Mjini, wamempitisha Khatib Abdulrahman Khatib , kugombea nafasi ya umeya wa manispaa hiyo.

Uchaguzi huo ulimpendekeza meya huyo na kumpitisha baada ya kupata kura 27 za madiwani wote, hatua ambayo itamfanya kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa Meya kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Khatib alipitishwa kuwania nafasi hiyo katika Mkutano uliofanyika  Ukumbi wa CCM Mkoa Mjini Amani Unguja ambapo mgombea huyo atachaguliwa kwa kuwa hakuna chama kingine chenye Madiwani ukiachia CCM na inatarajiwa atashika nafasi hiyo kwa mara ya pili. Kwa sasa Khatib ndie Meya wa Manispaa ya Mjini.

Madiwani hao pia walipitisha majina ya Naibu Meya ambaye ni Bimkubwa Said Sukwa aliepata kura 15, akimshinda mpinzani wake , Saleh Fasihi Saleh aliepata kura 12.

Kwa mujibu wa miongozo ya uchaguzi huo Majina hayo ya Meya na Naibu Meya yatapigiwa kura na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Mjini.

Kupitia Uchaguzi huo nafasi nyingine zilipigiwa kura ni Mwenyekiti wa Madiwani wa CCM katika manispaa hiyo na kupatikana Omar Mwalimu Juma , aliepata kura 13 na nafasi ya Katibu wa Kamati ya Madiwani iliyochukuliwa na Makame Khamis aliepata kura 27.

Mapema Akifungua Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai aliwataka Madiwani hao kuwachagua viongozi makini na wenye sifa za kujituma  kiutendaji.

“ Endelelezeni utamaduni wa Chama Chetu katika kufanya uchaguzi huru na wa haki ili kupata viongozi watakaoweza kusimamia shughuli za manispaa yetu kwa ufanisi.

Pia epukeni makundi na badala yake kuweni wamoja katika kufanya kazi za maendeleo ili wananchi waweze kunufaika na uwepo wenu katika Manispaa ya Mjini.”, aliwasihi Vuai na kuongeza kuwa Manispaa ya Mjini ndiyo kioo cha Mjini wa Zanzibar hivyo lazima pafanyike kazi ya ziada kuhakikisha panakuwa safi na kung’ara muda wote kama ilivyo Miji mingine Duniani.

Naibu Katibu Mkuu huyo aliwasisitiza Madiwani hao kuwa Chachu ya kuleta maendeleo katika Wadi zao na kubuni miradi inayoendana na matakwa halisi ya wananchi ili kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa vitendo.

Akizungumza na Gazeti hili mara baada ya Uchaguzi huo Meya Mteule wa Manispaa hiyo Khatib Abdulrahman Khatib aliwashukru Madiwani hao kwa kumuamini na kumpitisha tena ili aweze kuendelea kuongoza Manispaa hiyo kwa awamu ya pili.

Aliahidi kuendeleza mikakati ya kimaendeleo ndani ya Manispaa hiyo ikiwemo kushirikiana na viongozi wengine na wananchi kwa ujumla kuhakikisha Manispaa hiyo inakuwa na hadhi inayoendana na historia ya Zanzibar kimataifa.

Aliwakumbusha wananchi kudumisha usafi na utunzaji wa miundombinu mbali mbali iliyomo katika Manispaa hiyo ili kuepuka kuingia katika mikono ya kisheria.
Share:

Jumanne, 27 Desemba 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI KATIKA WILAYA YA RUANGWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa lindi  Alli Mohamed Mtopa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa Nachingwea (DED) Bakari Mohamedi Bakari katika kiwanja cha ndege cha Nachingwea wakati wa mapokezi ya waziri mkuu wilayani hapo waziri mkuu amefika kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa mkoani lindi
 Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT  843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo katika mapokezi ya Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Nachingwea 
Share:

Alhamisi, 22 Desemba 2016

ZIARA YA SHAKA MISENYI NA BUKOBA MJINI YAFANA


 Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka Mapema ya leo Ameikamilisha Ziara yake ya Kikazi katika Wilaya ya Misenyi na Bukoba Mjini yenye dhamira ya Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020 na Kuimarisha Uhai Wa Chama na Jumuiya  Mkoani kagera.


 Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka Alipo tembezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyelwa Kuona Athari zilizo tokana  na Mvua ya Mawe  Zilizo Wakumba Wananchi wa kijiji Kangenyi Kata ya Kieluwa Wilayani Kyelwa

 Mhandisi wa maji wilaya Misenyi ABdallah Gendaheka wa tatu kutoka kushoto akitoa maelezo mbele ya kaimu katibu mkuu wa UVCCM na msafara wake walipoutembelea mradi huo wa maji ambao kati ya vituo 15 ni vituo vi8tu vinavyotoa na saba kwa mwaka mmoja na miezi miwili sasa vimeharibika.
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM  Shaka Hamdu Shaka akipata maelezo toka kwa Afisa Mfawidhi wa Mpaka wa Mutukula Bw.Samwel Mori wilayani Misenyi Mkoani Kagera alipotembelea katika mpaka huo kuangalia shughuli za kihuduma katika mpaka huo.
 Mapokezi ya Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka  alipo Wasili Bukoba Mjini
 Watendaji na wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Manispa ya mji wa Bukoba wakimsikiliza Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka alipotembelea Manispaa hiyo
 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Ndg:Yahya kateme wa tatu toka kushoto alipoingia na mgeni wake Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka wa pili kushoto katika  kiwanda cha uzalishaji maji safi  Bunena Spring Water katika manispaa ya mji wa bukoba wa nne kulia ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya bukoba mjini Ashraf kazinja
 Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kagera  Dismas Zimbihire wa kwanza kulia akiongoza msafara na kumfikisha Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka katika eneo la uzakishaji Maji na ufungaji wa chupa katika kiwanda cha  Bunena Spring Water kilichopo katika manispaa ya mji wa bukoba.
 Makundi ya Vijana wajasiriamali wakiwemo Mamalishe,bodaboda,na machinga walipompokea kwa shangwe na hoihoi  Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka alipokwenda kuwatembelea katika soko la machinjioni kwenye manispaa ya mji wa bukoba.
 Kaimu katibu wa Idara ya Hamasa,Sera,Utafiti na Mawasiliana UVCCM Mtemi Slyvester yaredi akizungumza na makundi ya wajasiriamali katika manispaa ya mji wa bukoba kabla ya kumkaribisha Kaimu katibu mkuu UVCCM
 ''Nimefarijika saana na ziara ya mkoa wa Kagera,nimefurahi kuwakuta viongozi wa chama,Serikali kuu na Halmashauri za wilaya wakifanya kazi bega kwa bega kwa lengo la kuhudumia wananchi na kutekeleza matakwa ya sera za CCM zilizoainishwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020''Shaka alimueleza mkuu wa mkoa wa Kagera Meja jenerali Salum kijuu alipomtembelea ofisini kwake
''Nimekua nikifuatilia ziara zenu kwa karibu sana,nimeridhika na uibuwaji wenu wa maswala yenye manfaa,kuzindua miradi ya kimaendeleo lakini pia kuzungumza na wanachama wenu katika vikao vya ndani vya kisiasa.Changamoto mlizoziona serikali itaendelea kuzifanyia kazi na kupata utatuzi,tutasiliba na kuziba mianyayote inayopitisha wahamiaji haramu na kukomesha vitendo vya uhalifu,hatutashindwa kwa jambo lolote''Meja jenerali Kijuu alimueleza kaimu katibu mkuu UVCCM
Share:

SHAKA VIJANA FICHUENI WAHAMIAJI HARAMU.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akipokea Salaam za Shukrani Kwa niaba ya Rais  kwa mama MjaneAGRIPINA ANGERO ambaye alie jengewa Nyumba Mpya na Ya kisasa na Mhe : Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuri.

.................................................................................

 Kaimu katibu mkuu uvccm taifa Ndg Shaka H Shaka  tarehe 20 aliendelea na ziara yake mkoani Kagera wilayani KYERWA .Akiwa njiani kuelekea Wilayan Kielwa aliongozana pamoja na  viongozi   mbalimbali kumtembelea Mjane mama AGRIPINA ANGERO ambaye alie jengewa Nyumba Mpya na Ya kisasa na Mhe : Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuri mara baada ya nyumba aliokua akiishi mjane huyo kubomoka tokana na Tetemeko.

Akiwa hapo kaimu Katibu mkuu alipokea salamu za Shukrani kutoka kwa Mama Mjane AGRIPINA ANGERO  kwenda kwa mhe Rais kwa kumjali na kuguswa na Shida za wanyonge.Kaimu katibu mkuu amewaagiza UVCCM wilaya ya Karagwe ndani ya siku 3 kwenda kwenye eneo hilo kufanya Usafi  ili kumsaidia mama mjane. 

Pia akiwa Wilayani Karangwe kuelekea Wilayani Kielwa Kaimu katibu mkuu uvccm taifa Ndg Shaka H Shaka  alishiriki zoezi la kugawa vifaa vya ujenzi kwa familia 10 Wahanga wa Tetemeko vifaa hivyo vimetolewa na Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera usharika wa Karagwe akigawa vifaa hivyo kaimu katibu mkuu amelishukuru kanisa la Anglican kwa kuendelea kuguswa na maafa ya tetemeko.

Mara baada ya kupokelewa kijiji cha Changa akiwa kijijini hapo alipata fursa ya kukagua tenki la maji linalo tumiwa na wananchi katika kijiji hicho
Pia amepata fursa ya kutembelea mradi wa nyumba wa Uvccm tawi la Nkwenda akiwa hapo aliwataka vijana kuacha ulalamishi wajitume katika kazi za ujasiliamali na kuwekeza kwenye miradi ya kiuchumi.

Ukaguzi  Wa Utekelezaji wa ilani ulimfikisha Kaimu katibu mkuu uvccm taifa Ndg Shaka H Shaka  kuona pia ujenzi wa barabara ya Nkwenda-Mabira yenye urefu wa Km 31 iliyogharimu Tsh bil 2.

 Mara Baada ya zoezi hilo kaimu katibu mkuu alifika kijiji cha Kakanja sanjari na kutembelea mradi wa ufugaji nyuki akiwa hapo aliwapongeza wananchi kwa kuweza kuwekeza kwenye ufugaji nyuki na pia alitoa kadi kwa wanachama wapya 59 Uvccm na CCM.

Hatimaye Msafara wa kaimu katibu mkuu ulifika ofisi ya Mkuu wa wilaya Kyerwa Kanali mst Lissu kusomewa taarifa ya Serikali. na Mara Baada ya Kupokea Taarifa hiyo  alihudhuria baraza la Vijana wilaya akihutubia baraza hilo Kaimu katibu mkuu amewataka vijana kuacha kuwaficha wahamiaji haramu badala yake washirikiane na serikali katika kulinda mipaka na Wahamiaji haramu kutokana na wilaya kupakana na nchi za Rwanda na Uganda.
 Alisema"Hakikisheni mnawafichua wahamiaji haramu wote bila uoga hawa ni hatari kwa usalama wa nchi yetu" hali kadharika Tuache kupenda vya dezo kwa kuwafanya Vibarua katika Mashamba yetu ilhali tunajikaanga wenyewe pia'' Alisema Shaka.

Pia Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka ameitaka halmashauri wilaya Kielwa kuendelea kutoa mikopo kwa vijana  kwa kuzingatia 5%  ya mikopo ya vijana Wilayani humo Alisema'' Viongozi wa Halmashauri ifikie hatua Tuwajali Vijana kwa kuwapatia Mikopo ili waweze kujikwamua kiuchmi hawa ndio wapiga kura wetu Uvccm italala Mbele na Halmashauri itakayo kaidi Utoaji wa Fedha za Mikopo kwa Vijana''
Eneo la Nyumba ya Nyumba Mpya na Ya Mama MjaneAGRIPINA ANGERO  kisasa na Mhe: Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuri iliyopo katika Kijiji cha Kayanga Wilayani Karagwe.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa  Ndg:Shaka Hamdu Shaka wa Tatu Kulia akigawa Vifaa Vya Ujenzi Vilivyo tolewa kwa Hisani ya  Kanisa la Anglican Dayosisi ya Kagera usharika wa Karagwe kwa Familia nane Maskini zilizo kubwa na Tetemeko.
 •  Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe  Godfrey Ayub  Mheluka Mwenye Suti Nyeusi akiagana na kaimu katibu Mkuu Shaka Mara baada ya Kumfikisha Wilayani Kielwa.

kaimu katibu Mkuu Shaka akikagua Ukaguzi  Wa Utekelezaji wa ilani  Wilayani Kielwa ulimfikisha Kaimu katibu mkuu uvccm taifa Ndg Shaka H Shaka  kuona pia ujenzi wa barabara ya Nkwenda-Mabira yenye urefu wa Km 31 iliyogharimu Tsh bil 2.

 Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akiambatana na Mkuu wa wilaya Kanal Mstaafu Shaaban Lissu  na Viongozi Mbali mbali wa Chama na Serikali  akikagua Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wiliya iliyopo katika kijiji cha Rubwera Kagenyi Wilayani Kielwa.
  Mkuu wa wilaya Kyerwa Kanal Mstaafu Shaaban Lissu  akimsomea Kaimu katibu Mkuu Taarifa ya Serikali juu ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020.
Mwenyekiti wa Uvccm Yahya Kateme akimkaribisha Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Kuzungumza na Baraza la Vijana Wilayani Kielwa.
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka Akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM Wilaya ya Kielwa.
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akigawa kadi kwa Mmoja kati ya Wanachama  Wapya 173 Wilayani Kielwa Mkoa wa Kagera
Wanachama wapya wakila Kiapo na Yamini ya Chama Mara baada ya kupokea kadi ikiwa ni Ishara ya Kujiunga Rasmi na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi.
Share:

Jumanne, 20 Desemba 2016

SHAKA AZINDUA RASMI KAMPENI YA JOGGING UVCCM MKOANI KAGERA

Kaimu katibu mkuu Uvccm Taifa ndg Shaka H.Shaka leo amezindua rasmi kampeni ya Jogging UVCCM yenye kauli mbiu ya 'MAZOEZI KWA AFYA' iliyozinduliwa Kitaifa Wilayani Karagwe.

Katika Mazozi hayo Kaimu katibu mkuu ameshiriki jogging na Mazoezi Viungo akiongozwa na Mwenyekiti  Uvccm mkoa wa Kagera ndg YAHYA KATEME,Mkuu wa Wilaya Karagwe  Mhe. Godfrey Ayub  Mheluka pamoja na vijana na viongozi mbalimbali  Wa Chama na Serikali Wilayani humo.  

Akiongea  mara baada ya Mazoezi hayo Ndg: kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka amewataka Makatibu wa UVCCM Ngazi za Wilaya Nchini kote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa tangu Mnamo tarehe 24 Mwezi Oktoba 2016 la kuanzisha jogging Club alisema "nitumie fursa hii kuwapongeza sana kwa kutambua umuhimu wa mazoezi, sasa Vijana lazima wawe wakakamavu na tayari muda wote hatuwezi kuwa na taifa la vijana goigoi wasio jiweza kama ambavyo  hata makamu wa Rais alivyounga mkono katika swala hili la mazoezi " Pia amewataka vijana wote kushiriki ipasavyo Zoezi hili amesema '' Jogging ni swala muhimu sana kwa vijana kwani pamoja na kujenga miili yetu jogging itatufanya tuwe wamoja t wenye ushirikiano wa kudumu haswa katika mambo mbali mbali ya kijamii''.

 Kaimu katibu mkuu yupo katika ziara ya siku nane mkoani Kagera ambapo atatembelea wilaya zote 8 za mkoa wa Kagera.


 Kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (Mnec)  wa tatu kulia akiongoza zoezi la jogging wilaya karagwe pamoja na Viongozi Mbali mbali wa chama na Serikali
  Kaimu katibu mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wa katikati akiendeleza zoezi la jogging pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM  Wa Uvccm Mkoa wa Karagwe Ndg Yahaya Kateme wa kwanza kushoto.
 Kaimu katibu Mkuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Taifa Shaka Hamdu Shaka akiruka Mchaka mchaka katika viwanja vya CCM Wilaya ya karangwe leo.
 Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akiendelea na Zoezi la Unyooshaji wa Viungo pamoja na Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe. Godfrey Ayub  Mheluka
 Katibu UVCCM Mkoa wa Kagera Ndg:Didas Zimbile akiongoza Zoezi la Unyooshaji wa Viungo katika Viwanja vya CCM Wilaya ya Karagwe mapema leo.
 Kijasho chembamba kikimtiririka Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Ndg:Yahya Kamteme katika zoezi la unyooshaji wa Viungo Vya Mwili katika Viwanja Vya CCM Wilaya ya Karagwe.
Kaimu katibu Idara ya Hamasa,Sera,Utafiti na Mawasiliano Ndg Mtemi Slyvester Yaredi akiendelea na zoezi la kunyoosha viungo.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu