• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Alhamisi, 31 Machi 2016

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM-BARA, RAJAB LUHWAVI ATUA MBEYA KUANZA ZIARA YA KIKAZI LEO

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara, Rajab Luhwavi, akiwasalimia baadhi ya viongozi wa CCM wa mkoa baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya leo asubuhi. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangwi Kundya, Katibu wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Lobe Zongo na Katibu msaidizi Mkuu wa mkoa, Adallah Mayomba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwai akiwa na mwenyeji wake, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Mwangwi Kundya (kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani Mbeya.
Share:

Jumanne, 29 Machi 2016

Dk. Shein amteua Balozi Idd Makamu wa Rais Zanzibar


Balozi Seif Ali Idd  
  
Zanzibar. Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa visiwa hivyo.

Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk Shein amemteua Balozi Idd ambaye alikuwa na wadhifa huo hata kipindi kilichopita.

Uteuzi wa Balozi Idd aliyezaliwa Februari 23, mwaka 1942, ulianza jana ikiwa ni siku nne tangu kuapishwa kwa Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Balozi Idd anakuwa mtu wa pili kuteuliwa na Dk Shein baada ya kuteuliwa kwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said mwishoni mwa wiki.

Dk Shein sasa atakuwa na wakati mgumu wa ama kumteua au kutomteua Makamu wa Kwanza wa Rais ili kukidhi matakwa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani hakuna chama cha upinzani kilichokidhi vigezo vya kushirikishwa katika kuunda Serikali.    
Share:

Jumatatu, 28 Machi 2016

COMRADE JAPHARI MGHAMBA; ATOA POLE KWA UVCCM MKOA WA IRINGA

Mwenyekiti wa UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mwanga, Mkoa was Kilimanjaro Ndugu Japhari Kubecha Mghamba.
Kwa niaba ya Vijana wa CCM Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. napenda kutuma salam zangu za pole kwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini kwa niaba ya wana Uvccm wote waliko Iringa kwa kuondokewa na Ndugu yetu kipenzi Makaa Omari.

Binafsi nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Ndugu Makaa Omari, aliyekuwa mtia nia wa kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa Mgombea wa Uenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa.

Kama wanavyosema wahenga kwamba Kazi ya Mungu haina makosa lakini kiubinaadam nilazima tuumie,tusikitike,tuhuzunike na kulia kifo hiki kimetuumiza sana, Ndugu Omar ameondoka wakati Uvccm, Ccmm na Taifa likiwa linamuhitaji sana.

 Hakuna namna nyingine zaidi ya kukuombea kwa Mungu akupe furaha ya milele na Mwanga wa milele akuangazie lakini nasi tukiendelea kutafakari kifo chako tukiamini kuwa kila nafsi itaonja umauti.

Mimi pamoja na Vijana wenzangu wa Wilaya ya Mwanga tutaendelea kukuishi kwa kuyafuata Yale yote mema uliyokuwa ukiyafanya kwa ajili ya Chama na Taifa letu.

Poleni sana ndugu, jamaa, Rafiki, Wazazi wa Marehemu Makaa Omari na Wana Iringa wote kwa msiba huu mzito. Daima tupo pamoja katika kipindi chote cha majonzi, mazishi na maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wetu.

By.
Japhari Kubecha Mghamba
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Wilaya ya Mwanga.
Share:

Jumapili, 27 Machi 2016

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA PASAKA KANISA LA KKKT LA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa alipowasili kwa Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Mama Magufuli wakishiriki na waumini wengine Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini huku akisikilizwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa na Mchungaji Chalres Mzinga baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Mama Rebecca Malasusa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa baada ya Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akiwapungia waumini baada ya  Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akisalimiana na mtoto Javiera Lyimo (9) anayesoma darasa la tano shule ya Genesis jijini  baada ya  Ibada ya Pasaka katika Kanisa la KKKT la Azania Front jijini Dar es salaam leo Machi 27, 2016. 
Share:

ZUBEIR MAULID ACHUKUA FOMU YA KUWANIA USPIKA BARAZA LA WAWAKILISHI, ZANZIBAR

KATIBU wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dk. Yahya Khamis Hamad (kushoto) akimkabidhi fomu ya kugombea uspika, mgombea wa nafasi hiyo kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Zubeir Ali Maulid , ambapo uchaguzi wa spika unatarajiwa kufanyika tarehe Machi 30 , 2016, fomu hiyo alikabidhiwa katika ofisi ya katibu wa baraza ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.
KATIBU wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dk. Yahya Khamis Hamad (kushoto) akisalimiana na mgombea wa nafasi ya Uspika wa Baraza hilo kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Zubeir Ali Maulid wakati alipofika kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo katika ofisi ya katibu wa baraza ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.
MGOMBEA wa Nafasi ya Uspika kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) Zubeir Ali Maulid akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika wa Baraza la Wawakilishi katika ofisi za Baraza hilo ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.Picha na Haroub Hussein
Share:

UVCCM TAIFA INAWATAKIA PASAKA NJEMA

Kwa niaba ya Jumuiya ya Vijana wa CCM(UVCCM)

Tuwatakia Sikukuu njema kwenu nyote,

Nawatakia heri ya Sikukuu ya Pasaka, nikiwa nimekaa Kariakoo, maeneo ya Jangwani na Watoto sita wa Mtaani.

Mmoja wa Watoto hawa nilimjua wiki tatu hivi zilizopita.

Nikiwa na Vijana Wenzangu nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, mbele yetu jirani kabisa na lami ya Lumumba road alilala kijana mdogo wa miaka 13.

Akiwa hana ndala na nguo chafu sana, nyuso yake iliashiria njaa Kali sana.

Nikiwa nataka kuendesha Pikipiki kutoka eneo hilo nafsi ilikataa, nilimuamsha kijana huyo alielala juani.

Kijana amka njoo hapa, unaitwa nani? umetoka wapi? Kwanini umelala hapa?

Kijana : Njaa inauma Kaka kaninunulie chakula,
Nilitokea Mwanza Kuja kumtafuta Mama yangu Hortesia niliambiwa yupo Dar Es Salaam, Sina simu yake wala chochote nimekuwa nikilala Mitaani Kariakoo miezi Sita Sasa.

Maswali nilimuuliza mengi sana,
Kifupi majibu ni hayo alionijibu ili ujaribu kupata picha wewe ambae unakula bata Sikukuu hii ama umepanga kula bata.

Nilimpima kijana huyu kwa kumpa pesa ya kula na kumwambia akanunue Ndala, Shati, Suruali na kunyoa Nywele na kesho yake anitafte kwa kutafta simu yeyote ile ata alipie atume ujumbe nitamuona(Nilimpa Business Card yangu).

Kijana alikuwa mtiifu kweli kwa mara ya kwanza ndani ya Miezi Sita alibadili Nguo.

Leo siku ya Pasaka nimekuja kumuona yeye na wenzake sita na kila Mmoja wao ana Historia yake.

Huruma ilikuja Zaidi baada ya wengine kusema wanafanyiwa vitendo vya liwati usiku na watu wazima na wamelia wakiomba wapande gari warudi kijijini wakakae tu na bibi, kwani hawajui wazazi wao walipo.

Mimi na Marafiki zangu tutawasaidia hawa ikibidi waende na Shule kabisa na baada ya Mwaka Mmoja tutatoa Taarifa rasmi ya Maendeleo yao.

Wakati tunakula bata za Sikukuu ujumbe wangu na Ushauri wangu.

Wakati umefika kwa Serikali kuweka Sheria na utaratibu rasmi kwa watu wote wanaozaa ama wanaotaka kuzaa.

Ndugu zangu tatizo hili ni kubwa sana na Dunia tuendayo sasa si ya kuendelea kuzalisha watu tegemezi, wakutegemea wengine kuishi
Wakati wapo vijana wakike na wakiume ambao kazi yao wao kuzaa tu bila kulea.

Binti anashika Mimba lazima amtaje aliempa na wote waandikishwe wata wajibika kumlea Mtoto mhusika ikibidi Serikali imlee Mtoto ila  Baba na Mama wakae Gerezani kama wameshindwa kulea Mtoto wao.

Hii itakomesha kuzaa ovyo na kutelekeza ovyo Watoto mtaani.

Itasaidia pia kukuza kizazi kinacho eleweka katika kujitaftia Ajira na kukipa Elimu ya Bure.

Elimu ya Bure isiwe ndio tiketi ya kufyatua Watoto Vijijini na kuwatelekeza.

Wito wangu kwa Rais.... Iwe wanaotelekeza watoto kwabibi zao, mtaani huku wakipata shida watu hao ni Majipu lazima watumbulie haraka sana.

Tunawatakia pasaka Njema.

Imetolewa leo Machi 27, 2016 na;
Abubakar Asenga,
Mtoto wa Fundi Cherahani,
Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano.
Meseji 0715429738.
Share:

Jumamosi, 26 Machi 2016

MBUNGE KIJANA MHE. ZAINAB KATIMBA AKUTANA NA ASASI ZA VIJANA

Katibu wa Organization na  Siasa UVCCM TAIFA na MBUNGE wa Viti Maalum kupitia kundi LA Vijana, Mhe. Zainab Katimba akiwa katika picha ya pamoja na Vijana.

Katibu wa Organization na  Siasa UVCCM TAIFA na MBUNGE wa Viti Maalum kupitia kundi LA Vijana, Mhe. Zainab Katimba akiwa katika Meza ya Majadiliano na Vijana.


apema leo TYVA ilipokea ugeni wa Mbunge wa Vita Maalum (CCM), Mhe.Zainab Katimba na Mjumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, ambaye pia anawakilisha kundi la vijana.

Pia kulikuwa na uwakilishi wa asasi ya NA ikiwakilisha na mjumbe wa kamati ya utendaji Arafat.

kaimu Katibu Mtendaji wa TYVA Bw. Sadam Khalfan akiwa na Makamu Mwenyekiti Bw.Dickson Kamala na Afisa Mahusiano wa Mradi wa YEID Bi.Emiliana Muchu, wamemhakikishia ushirikiano mbunge huyu katika kusukuma ajenda ya Vijana mjengoni(bungeni).

Pamoja na mambo Mengine Mbunge kijana Mhe.Zainab Katimba amekubali kuifikisha ajenda ya vijana bungeni na kupigania maslahi ya vijana kwa ujumla akiwa mjengoni.

TYVA imeunda kikosi kazi cha Vijana kwa ajili ya shughuli za bungeni yaani Parliamentary Youth Working Group ambayo mwaka 2015 April kikosi kazi hicho kilisaidia kuboresha muswada wa sheria ya Baraza la Vijana Tanzania.

Kikosi kazi hicho kinachoundwa na asasi mbalimbali za vijana kitakutana mapema April ili kuja na maoni juu ya Bajeti ya Wizara inayohusika na vijana kwa mwaka wa fedha 2016/2017.


M

Share:

MH. HALIMA DENDEGU ATEKELEZA AHADI YAKE, AWAPA VIJANA 600 BIMA YA AFYA

Mwenyekiti wa UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara ndugu Nestory Chilumba akiwa Meza kuu na Mh. Halima Dendegu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Mwenyekiti wa UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara ndugu Nestory Chilumba akiwa Meza kuu na Mh. Halima Dendegu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Wanachama wa UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara, waliojitokeza kuja kuchukua kadi zao za Bima.

Wanachama wa UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara, waliojitokeza kuja kuchukua kadi zao za Bima.

Wanachama wa UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara, waliojitokeza kuja kuchukua kadi zao za Bima.

Kwa niaba ya UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Mtwara, nikiwa kama Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa natoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu kwa kutekeleza ahadi yake ya kutoa kadi za Bima ya Afya kwa vijana 600 ambao walishiriki Kambi ya Vijana Mkoa mwaka jana.

 Leo hii vijana hao wanafuraha sana kupata Kadi za Bima ya Afya ambazo zimelipiwa Mwaka mzima. Mungu akubariki sana Mh. Halima Dendegu kwa kutimiza ahadi yako kwa vijana wako wa Chama Cha Mapinduzi. CCM oyeeeeeee√®eeee
Share:

Ijumaa, 25 Machi 2016

ZUBERI ALI MAULID KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM KINYANG'ANYIRO CHA SPIKA WA BARAZA

Picha ya Ndugu Zuberi Ali Maulid amechaguliwa kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Spika wa Baraza.
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi watokanao na Chama Cha Mapinduzi Zanzibar leo wamefanya Uchaguzi wa kumpata mjumbe atakaye peperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Spika wa Baraza hilo, kwa kipindi cha mwaka 2015 - 2020.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi  Mhe. Waride Bakari Jabu, amesema uchaguzi huo ulioendeshwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, ulifanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Unguja.

Mwenyekiti wa Uchaguzi huo, uliojumuisha wajumbe 72, alimtangaza Zubeir Ali Maulid kuwa mshindi baada ya kupata kura 55 na kuwashinda wapinzani wake wawili aliyemaliza muda wake Pandu Ameir Kificho aliyepata kura 11 na Jaji Janeth Nora Sekihola aliyepata 4, na kura mbili (2) ziliharibika.

Jumla ya wanachama wa tisa (9) walijitokeza kuomba ridhaa ya CCM ili wagombee nafasi hiyo ya Spika .

Katika kikao cha Kamati Maalum kilichofanyika Machi 24, mwaka huu, Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, ilipitisha majina matatu ikiwa ni pamoja na Pandu Ameir, Zubeir Ali Maulid na Janeth Nora Sekihola, ambapo uchaguzi wake umefanyika leo.

Akitoa neno la shukrani, Zubeir Ali Maulid, aliwashukuru wajumbe hao kwa imani yao kwake na kuwataka wampe kila aina ya mashirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Naye aliyekuwa Spika wa Baraza hilo Pandu Ameir Kificho, amekubali kushindwa na kumuahidi kumpa msaada wowote atakaohitaji, iwapo atatakiwa kufanya hivyo.

Uchaguzi huo wa Spika unatarajiwa kufanyika mara tu baada ya kuitishwa kwa Baraza jipya la Wawakilishi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

 Sgd
…………….
 (Waride B. Jabu),
Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM,
ZANZIBAR.
25/03/2016.
Share:

KATIBU WA UVCCM NYAMAGANA AFANYA ZIARA KATA YA ISAMILO

Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndugu Odilia Abraham Batimayo akizungumza na Vijana wa Kata ya Isamilo Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza.

Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndugu Odilia Abraham Batimayo (katikati) na Katibu Hamasa wa Wilaya (Kulia) wakielekea katika kikao na Vijana wa Kata ya Isamilo Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza.

Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndugu Odilia Abraham Batimayo(wa pili kushoto) akiwa Meza Kuu wakati anatambulishwa na Katibu Hamasa wa Wilaya katika kikao na Vijana wa Kata ya Isamilo Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza.

Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana Ndugu Odilia Abraham Batimayo, aendeleza ziara yake ya kuimalisha jumuiya katika Kata ya Isamilo.

Akiambatana na Katibu Hamasa wa Wilaya, katibu Odilia amezungumza na kuwa hamasisha vijana juu ya uhai wa jumuiya na kuwahimiza vijana kuwa wazalendo katika kukitumikia chama na kuwa na umoja na mshikamano, lakini pia katika ziara yake hiyo amebaini changamoto mbali mbali zinazo wakabili vijana na kuzitolea ufafanuzi namna gani ya kuzitatua, moja ya changamoto kubwa ikiwa ni swala la ajira kwa vijana aliwaomba na kuwa hamasisha kwa haraka zaidi vijana waweze kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kujikwamua kiuchumi na Kuwaahidi atakua nao bega kwa bega ili vijana kuweza kujiondoa katika hali ya kuwa tegemezi na kutafta fursa za kujikomboa kiuchumi.
 #HapaKaziTu
Share:

KAMATI KUU MAALUM YAKUTANA ZANZIBAR

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua kikao cha Kamati Kuu Maalum kilichofanyika kwenye Afisi Kuu za CCM Zanzibar,Kikao hicho kiliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ,Rais wa Srikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ai Mohamed Shein (kulia) wengine pichani ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu CCM (Zanzibar) Mhe. Vuai Ali Vuai.
 Spika wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Pandu Kificho akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakipitia agenda muhimu ya kikao hicho cha Kamati Kuu Maalum ambacho kililenga kupendekeza jina la Spika la Baraza la Wawakilishi.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Jerry Silaa muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu Maalum mjini Zanzibar.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai wakipitia ajenda ya kikao hicho cha Kamati Kuu Maalum, kulia ni Mhe. Pandu Ameir Kificho mjini Zanzibar.
Share:

Alhamisi, 24 Machi 2016

SHEREHE YA KUAPISHWA RAIS MTEULE WA ZANZIBAR KATIKA UWANJA WA AMANI LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamanda wakati alipokuwa akikagua gwaride la Vikosi vya Brass Band leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,baada ya kuapishwa rasmi kwa kuongoza Zanzibar katika kipindi cha Pili cha Awamu ya saba.
Rais Mteule wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akitia saini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu Mhe,Omar Othman Makungu baadanya kumalizikika kwa zoezi hilo lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee. 
Viongozi mbali mbali wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa leo katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi baada ya zoezi la kuapishwa pamoja na kukagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa unaoashiria mwanzo wa Uongozi wake kwa kipindi cha pili katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa rasmi leo. 

Waaandishi wa Habari Wapigapicha wakijaribu kufanikisha kazi yao kupata matukio mbali mbali wakati wa Sherehe za kumuapisha kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Mkuu wa KMKM Hassan Mussa Komodoo wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Kaimu Mkuu wa JKU Kanali Ali Mtumweni Hamadi wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
WanaChama cha Mapinduzi na Wananchi wakiwa pamoja wakisherehekea kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,pia wakiwepo Waandishi wa Habari kushuhudia mambo mbali mbali yanayoendelea katika zoezi la kuapishwa kwa Rais.
[Picha na Ikulu.]
Share:

COMRADE ASENGA ABUBAKAR; WANACUF MATUSI HAITASAIDIA KUZUIA RAIS ASIAPISHWE

Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano UVCCM TAIFA, Ndugu Abubakar D. Asenga akizungumza na Vijana wa Hamasa Zanzibar.
Tunaomba mpuuze kwa mara nyingine uzushi unaosambazwa juu ya Umoja wa Vijana CCM na Kaimu Katibu Mkuu wake Ndugu Shaka Hamdu kwenye mitandao ya kijamii.

Tupo  Zanzibar Pemba na Unguja tunaendelea na hamasa ya vijana kushiriki kwa wingi Uwanja wa AMANI kesho kuhakikisha Rais Mteule Dr. Ally Mohammed Shein anaapishwa kwa salama na amani.

Tunajua kwa siasa za huku Zanzibar matusi ni ya kawaida kutoka kwa wapinzani Ila yamewapa taabu baadhi ya watu wabara.

WanaCUF hii ya matusi kwa Ndugu Shaka Hamdu hayatawasaidia kuzuia Rais asiapishwe.

Najua Salam za Jana za matembezi makubwa yalioongozwa Kaimu Katibu Mkuu UVCCM kwa kushirikiana na Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano UVCCM TAIFA Pemba na unguja bado zinawapa kiwewe. Hamkuamini kuwa mmechokwa na malaki ya watu.

Tutawajibu vizuri baada ya kumaliza agenda ya kesho uwanja wa AMANI. Sasa hatoki mtu kwenye agenda
Masalaaam
Abubakar D. Asenga
Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano UVCCM TAIFA
Niulize kwa 0715429738
HAPA KAZI TU
Share:

Jumatano, 23 Machi 2016

MWENYEKITI WA UVCCM KILIMANJARO, AENDELEA NA ZIARA WILAYA YA MOSHI VIJIJINIMwenyekiti UVCCM mkoa wa Kilimanjaro ameendelea na ziara ya kuimarisha Jumuiya wilayani Moshi vijijini.

Akiwa wilayani hapo amekutana na Kamati ya utekelezaji ya wilaya na kupewa taarifa ya hali ya kisiasa na kichumi ya Jumuiya.

Alitumia ziara hiyo kuzindua mashina matatu ya kereketwa ya vijana Kata ya Makuyuni.

M/kiti wa Uvccm mkoa kili, Ndg. Juma Raibu aliweza kukagua eneo la Jumuiya lililovamiwa na Bw. Mafole na kuamua kulima eneo hilo bila kufata utaratibu. Ametoa onyo kali kwa kitendo hicho na amemtaka kufuata taratibu za msingi.

Alitumia ziara hiyo kutembelea Mamlaka ya Mji mdogo wa HIMO kupewa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kisikiliza changamoto zao na kuahidi kuzifikisha kwa wakati kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Said Mecky Sadiq.

Baada ya hapo alifanya mkutano wa hadhara wa wananchi Kata ya Kahe Mashariki na baada ya kusikiliza kero mbalimbali ziliwasilishwa na Mh. Diwani Mmbando wa CCM. M/kiti wa uvccm mkoa amempatia BATI 10 ili ziweze kwenda kukamilisha ujenzi wa CHOO unaoutumika na shule mbili za msingi ya Mabirango na Ghona.

Sambamba na hilo amewataka vijana na wanawake kuunda vikundi kwa ajili ya kukopesheka. Pia, amewaahidi jezi na mipira kwa ajili ya michezo kata hiyo.

Baada ya Mkutano wa hadhara Uvccm mkoa wa kilimanjaro ulimtembelea Ndg. Halid Shekoloa kada wa CCM ambaye jana usiku nyumba yao iliungua yote na kumfariji pamoja na kumpatia pole ya Jumuiya.

Ziara ya Uvccm mkoa kilimanjaro itaendelea kesho wilayani HAI.
@Uvccm Kilimanjaro, 2016.
Share:

Jumatatu, 21 Machi 2016

WANANCHI WASHEREKEA USHINDI WA CCM KWA KISHINDO KIKUU, ZANZIBAR YASIMAMA!


Taarifa kutoka Zanzibar zinasema kuwa Wananchi wameandamana kwa wingi ili kusherekea Ushindi wa Rais Mteule Dr. Ali Mohammed Shein, Unguja na Pemba shughuli zimesimama kwa muda ili kushiriki katika msafara huo, ambao unaelezwa kuwa na waendesha pikipiki wengi na magari pamoja na Wananchi wengi walijitokeza Leo jioni kila kona ya Zanzibar ilitawala rangi nyeusi na kijani.

Taarifa kutoka Zanzibar zinasema kuwa Wananchi wameandamana kwa wingi ili kusherekea Ushindi wa Rais Mteule Dr. Ali Mohammed Shein, Unguja na Pemba shughuli zimesimama kwa muda ili kushiriki katika msafara huo, ambao unaelezwa kuwa na waendesha pikipiki wengi na magari pamoja na Wananchi wengi walijitokeza Leo jioni kila kona ya Zanzibar ilitawala rangi nyeusi na kijani.

Taarifa kutoka Zanzibar zinasema kuwa Wananchi wameandamana kwa wingi ili kusherekea Ushindi wa Rais Mteule Dr. Ali Mohammed Shein, Unguja na Pemba shughuli zimesimama kwa muda ili kushiriki katika msafara huo, ambao unaelezwa kuwa na waendesha pikipiki wengi na magari pamoja na Wananchi wengi walijitokeza Leo jioni kila kona ya Zanzibar ilitawala rangi nyeusi na kijani.

Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu