Jumatatu, 14 Machi 2016

CHAMA CHA MAPINDUZI SINGIDA KUUNDA KAMATI YAKUFUAILIA MIRADI YAKE

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimewaagiza wenyeviti wa chama wa wilaya zote Mkoani Singida kuunda kamati za kufuatilia mali za chama za wilaya zao pamoja na miradi yake yote iliyopo kwenye maeneo yao na taarifa za kamati hizo zitumwe makao makuu ya mkoa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Marther Mosses Mlata alitoa agizo hilo alipokuwa aakiongea na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Manyoni,uliokuwa na lengo la kuwashukuru kwa kumchagua kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Akizungumza na wanachama wa chama hichco,wa wilaya ya Manyoni,Mwenyekiti huyo alisema kwamba iwapo miradi ya chama hicho itafahamika na kutambulika kikamilifu uzalishaji wake,utasaidia kuondokana na tabia ya kuwategemea madiwani kusaidia kwa kila jambo linalojitokeza kwenye maeneo yao.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata akisisitiza jambo kwenye mkutano wa kuwashukuru wajumbe wa wilaya ya Manyoni.

“Mwenyekiti ninaomba uunde kamati maana mimi nitaunda hivi leo ninamalizia halafu nitatangaza kamati yangu,hivyo unda kamati itakayofuatilia mali za chama za wilaya na miradi yake yote ije pale makao makuu ya mkoa”alisisitiza huku akishangiliwa na wanachama wa chama hicho waliohudhuria mkutano huo.

“Nimesema mali za wilaya,mali si mnazo,miradi mnayo,mapatoo,mapatoo… mnasomewa,mwenyekiti wenu anasema?alihoji mwenyekiti huyo mbele ya wanachama hao ambao kwa kauli moja walipinga kutosomewa taarifa za mapato na matumizi ya chama chao.

Kwa mujibu wa Mlata hata hivyo alitumia mkutano huo pia kuwaagiza watendaji wa ngazi za matawi na kata kwenda kuunda kamati hizo kwa madhumuni kama hayo ya kutambua mali za wanachama wa chama hicho na kutuma taarifa zao wilayani na kusisitiza pia kwamba kwa kata na matawi yasiyokuwa na miradi ikabuni haraka ili vyanzo vya mapato viweze kuwepo kwenye maeneo husika.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata akivishwa skafu muda mfpi tu mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za chama mjini Manyoni.

Naye Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki(CCM), Emanueli Mtuka alisema kuwa ili fedha zilizoahidiwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano,Dk.John Pombe Magufuli kwa kila Kijiji kupatiwa shilingi milioni hamsini,ni vyema vikundi vyote vilivyoundwa wilayani hapa kutosubiri fedha hizo na badala yake vifungue akaunti benki,kuchagua viongozi pamoja na kuanza kufanyakazi mara moja na hiyo ndiyo sifa pekee ya kupata fedha hizo.

“Tuliimba sana kipindi kile kuna milioni hamsini inakuja kweli si kweli…ile milioni hamsini haitagawiwa kama njugu,bali ni kwenye vikundi kama vile kikundi cha Kaloleni kimekaa vizuri nadhani mama atakisemea vizuri sana sitaki kukisemea”alifafanua Mtuka.

Kwa mujibu wa mbunge Mtuka kikundi cha Kaloleni kimekaa kisayansi,kina viongozi,kina mikakati na wameshaanza kazi kwa kufungua akaunti,kuchagua viongozi na waanze kufanyakazi mara moja hata kama kwa kuchechemea.
Mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki,Bwana Emmanueli Mtuka akifafanua juu ya upatikanaji wa shilingi milioni 50 za JPM.


Hata hivyo mbunge huyo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa vikundi vya vijana pamoja na akina mama vya Manyoni waige mfano ulioonyeshwa na kikundi cha Kaloleni ili navyo visisubiri kuwezeshwa na badala yake vianze kufanyakazi haraka iwezekanavyo kwani ndiyo sifa pekee ya kupata fedha hizo.

Awali katika taarifa ya wanakikundi cha umoja wa vijana wa CCM(UVCCM) ilieleza mafanikio waliyopata kuwa ni pamoja na cherehani nne,jora tano za vitambaa na mashsine mbili za kufyatulia matofali na akiba benki ya shilingi 150,000/=.
Kuhusu changamoto wanakikundi hao walisema kwamba licha ya mafanikio hayo lakini kikundi hicho kinakabiliwa pia na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa fedha za kununulia vitendeakazi  vya kikundi hicho.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu