Jumatatu, 28 Machi 2016

COMRADE JAPHARI MGHAMBA; ATOA POLE KWA UVCCM MKOA WA IRINGA

Mwenyekiti wa UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mwanga, Mkoa was Kilimanjaro Ndugu Japhari Kubecha Mghamba.
Kwa niaba ya Vijana wa CCM Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. napenda kutuma salam zangu za pole kwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini kwa niaba ya wana Uvccm wote waliko Iringa kwa kuondokewa na Ndugu yetu kipenzi Makaa Omari.

Binafsi nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Ndugu Makaa Omari, aliyekuwa mtia nia wa kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa Mgombea wa Uenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa.

Kama wanavyosema wahenga kwamba Kazi ya Mungu haina makosa lakini kiubinaadam nilazima tuumie,tusikitike,tuhuzunike na kulia kifo hiki kimetuumiza sana, Ndugu Omar ameondoka wakati Uvccm, Ccmm na Taifa likiwa linamuhitaji sana.

 Hakuna namna nyingine zaidi ya kukuombea kwa Mungu akupe furaha ya milele na Mwanga wa milele akuangazie lakini nasi tukiendelea kutafakari kifo chako tukiamini kuwa kila nafsi itaonja umauti.

Mimi pamoja na Vijana wenzangu wa Wilaya ya Mwanga tutaendelea kukuishi kwa kuyafuata Yale yote mema uliyokuwa ukiyafanya kwa ajili ya Chama na Taifa letu.

Poleni sana ndugu, jamaa, Rafiki, Wazazi wa Marehemu Makaa Omari na Wana Iringa wote kwa msiba huu mzito. Daima tupo pamoja katika kipindi chote cha majonzi, mazishi na maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wetu.

By.
Japhari Kubecha Mghamba
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Wilaya ya Mwanga.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu