Unordered List


MAKA OMARY; NATAKA KUWEKA HISTORIA NDANI YA UVCCM IRINGA

Mgombea nafasi ya Uenyekiti UVCCM Mkoa wa Iringa Ndugu Maka Omary, akiwa ofisi za CCM Mkoa wa Iringa akisubiri kuhojiwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa.

Mgombea nafasi ya Uenyekiti UVCCM Mkoa wa Iringa Ndugu Maka Omary, akiwa ofisi za CCM Mkoa wa Iringa akisubiri kuhojiwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa.

Akizungumza na Blog ya Uvccm Taifa, Ndugu Maka Omari amejinadi kuwa yeye ndiye anastahili kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa kwani anazosifa zote.

Binafsi Mimi ni Mdau wa Vijana ndani ya Mkoa wetu(Iringa), nilijitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti was UVCCM Mkoa wa Iringa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti kujiuzulu(Dada tumaini Msowoya)".

Aliendelea kusema, "Mimi ni mkazi wa Iringa Mjini, kwa sasa ni Mwenyekiti wa Uvccm tawi la Ngeleli, nimekuwa mwamasishaji wa nyimbo za Chama na nimekuwa nikishirikiana na Marehemu Kapteni John Komba. Ni mwasisi wa programu ya kitaifa ya kuzuia ujangili inayojulikana kama SIMAMA TANZANIA TOKOMEZA UJANGILI".


alimalizia kwa kusema "Nataka kuweka historia katika jumuiya ya Vijana so nawaomba vijana waniombe na Mungu atajibu Maombi Yetu".



Chapisha Maoni

0 Maoni