Jumatano, 23 Machi 2016

MWENYEKITI WA UVCCM KILIMANJARO, AENDELEA NA ZIARA WILAYA YA MOSHI VIJIJINIMwenyekiti UVCCM mkoa wa Kilimanjaro ameendelea na ziara ya kuimarisha Jumuiya wilayani Moshi vijijini.

Akiwa wilayani hapo amekutana na Kamati ya utekelezaji ya wilaya na kupewa taarifa ya hali ya kisiasa na kichumi ya Jumuiya.

Alitumia ziara hiyo kuzindua mashina matatu ya kereketwa ya vijana Kata ya Makuyuni.

M/kiti wa Uvccm mkoa kili, Ndg. Juma Raibu aliweza kukagua eneo la Jumuiya lililovamiwa na Bw. Mafole na kuamua kulima eneo hilo bila kufata utaratibu. Ametoa onyo kali kwa kitendo hicho na amemtaka kufuata taratibu za msingi.

Alitumia ziara hiyo kutembelea Mamlaka ya Mji mdogo wa HIMO kupewa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kisikiliza changamoto zao na kuahidi kuzifikisha kwa wakati kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh. Said Mecky Sadiq.

Baada ya hapo alifanya mkutano wa hadhara wa wananchi Kata ya Kahe Mashariki na baada ya kusikiliza kero mbalimbali ziliwasilishwa na Mh. Diwani Mmbando wa CCM. M/kiti wa uvccm mkoa amempatia BATI 10 ili ziweze kwenda kukamilisha ujenzi wa CHOO unaoutumika na shule mbili za msingi ya Mabirango na Ghona.

Sambamba na hilo amewataka vijana na wanawake kuunda vikundi kwa ajili ya kukopesheka. Pia, amewaahidi jezi na mipira kwa ajili ya michezo kata hiyo.

Baada ya Mkutano wa hadhara Uvccm mkoa wa kilimanjaro ulimtembelea Ndg. Halid Shekoloa kada wa CCM ambaye jana usiku nyumba yao iliungua yote na kumfariji pamoja na kumpatia pole ya Jumuiya.

Ziara ya Uvccm mkoa kilimanjaro itaendelea kesho wilayani HAI.
@Uvccm Kilimanjaro, 2016.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu