Alhamisi, 24 Machi 2016

SHEREHE YA KUAPISHWA RAIS MTEULE WA ZANZIBAR KATIKA UWANJA WA AMANI LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamanda wakati alipokuwa akikagua gwaride la Vikosi vya Brass Band leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,baada ya kuapishwa rasmi kwa kuongoza Zanzibar katika kipindi cha Pili cha Awamu ya saba.
Rais Mteule wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omar Othman Makungu katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akitia saini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu Mhe,Omar Othman Makungu baadanya kumalizikika kwa zoezi hilo lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee. 
Viongozi mbali mbali wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa leo katika sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi baada ya zoezi la kuapishwa pamoja na kukagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa unaoashiria mwanzo wa Uongozi wake kwa kipindi cha pili katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa rasmi leo. 

Waaandishi wa Habari Wapigapicha wakijaribu kufanikisha kazi yao kupata matukio mbali mbali wakati wa Sherehe za kumuapisha kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Mkuu wa KMKM Hassan Mussa Komodoo wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana mkono na Kaimu Mkuu wa JKU Kanali Ali Mtumweni Hamadi wakati aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
WanaChama cha Mapinduzi na Wananchi wakiwa pamoja wakisherehekea kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,pia wakiwepo Waandishi wa Habari kushuhudia mambo mbali mbali yanayoendelea katika zoezi la kuapishwa kwa Rais.
[Picha na Ikulu.]
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu