Jumatano, 9 Machi 2016

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM KWA UMMA

Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano, Ndugu Aboubakary Asenga akizungumza na Wananchi (Hawapo Pichani).

Tunapenda kuwajuilisha kwa masikitiko makubwa kuwa  Leo  alasiri kupitia mtandano mmoja wa kijamii ilisambazwa taarifa ya kihuni na upotoshaji  ikiihusisha Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa  (UVCCM)dhidi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano Mheshimiwa  January Yussuf Makamba.

Tungependa ifahamike kuwa UVCCM  haijawahi kuandika wala kujiwa na wazo  la kuandika mambo ya kipuuzi na uzushi  yaliyoandikwa kwenye taarifa ya mtandao huo na kutoa shutuma zenye taaswira ya unafiki na uzandiki na upotoshaji kwa  lengo la kuipaka matope jumuiya yetu mbele ya jamii.

UVCCM haijawahi kufanya kikao chochote cha kikatiba na kujadili suala lolote kuhusu mwenendo wa Waziri yeyote katika Serikali ya awamu ya tano au  kushindikiza Serikali imchukulie hatua zozote waziri mhusika. 

Aidha Kaimu  katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka hajawahi kutoa tamko lolote linalohusisha jina la Waziri January na tuhuma yoyote ya kutunga uongo, kuamini hatimaye kuueneza katika jamii. 

Kutwa nzima   Leo  Kaimu Katibu Mkuu Shaka amekuwa  akishiriki maziko ya marehemu Mzee Seleman Khalifan Kikwete katika kijiji cha  Msoga jimbo la Chalinze hadi jioni alipoona taarifa hiyo ilioandikwa na kundi la wahuni na kusambazwa. 
Tunatambua zipo juhudi na wapo mamluki majeruhi  wachache wanaopania kila uchao  kutaka aidha  kuwagawa wana jumuiya , kuivunjia heshima taasisi yetu na viongozi wenye staha mbele ya jamii na   mpasuko na kugombanisha watu kwa sababu wanazozijua wao  na mabwana wanaowatumikia. 

Nichukue nafasi hii kukanusha kwa sauti ya juu kwamba UVCCM wala ofisi ya Kaimu Katibu Mkuu haihusiani na taarifa inayosambazwa na maadui ambao muda si mrefu watajulikana na kuchukuliwa hatua za kisheria.

UVCCM  tunawaonya na kuwatahadharisha wale wote wenye fikra za kutukwamisha , wajue kuwa mradi wao wa kuwa mawakala wa mafisadi hautafanikiwa wala hautawasaidia kwa wakati huu. Tunawahakikishia UVCCM ni taasisi kubwa hivyo hili na jengine la kutaka kutuchafua tutalikomesha muda mfupi toka leo kwa mujibu sheria.

Imetolewa na
Aboubakary Asenga 
Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano.
Na Sufyan Omar.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu