Kaimu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Shaka Hamdu Shaka. |
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM ) umesema uchaguzi wa marudio utakaofanyika kesho machi 2o mwaka huu ndiyo utakaotatua na kuhitimisha mvutano uliopo kufuatia Tume ya Uchaguzi Zanzbar (ZEC) kufuta matokeo kwa mujibu wa sheria.
Umesema wananchi watakaopiga kura na kutumia haki ya kuchagua nani awe Rais kwa mujibu wa sheria, ndiyo hatua itakayokwamua kile kinachoitwa mkwamo wa kisiasa zanzibar.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu shaka amewaeleza waandishi wa habari jana katika Afisi kuu ya UVCCM huko Gymkhana mjini Unguja.
Shaka alisema wale wanaosema Zanzibar kuna mgogoro au tatizo linalohitaji kupatiwa suluhu bado hawajatambua kiini cha tatizo na ufumbuzi wake ila wanajifurahisha .
Alisema kiini cha tatizo au kukithiri kwa mivutano ya kisiasa iliopo inasababishwa na chama cha CUF kukidi utii wa matakwa ya sheria na kutaka hata kuipuuza katiba ya Zanzibar.
"Zanzibar ina katiba na sheria zake,vipi sheria na katiba zipuuzwe ili kuyapa nafasi mazungumzo ya kisiasa ambayo hayatokani na nguvu za kikatiba wala sheria za Zanzibar "alisema
Shaka amewatolea wito vijana kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika upigaji kura kesho ili hatimaye wananchi wa Zanzibar watekeleze haki ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Aidha alisema tokea uchaguzi wa kwanza mgombea wa CUF Maalim Seif amekuwa akijenga mazingira ya kuonyesha anaibiwa kura zake bila kuonyesha ushahidi.
Shaka alisema kiongozi huyo wa CUF anataka kushika madaraka kupitia huruma ya mazungunzo ya kisiasa na kutaka apuuzie utashi wa sheria na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
"Maridhiano hufanyika baada ya kupita mchakato wa uchaguzi baada ya wananchi kuamua kwa kura zao, ikiwa kuna dosari au hitilafu zozote zinaweza kuzungumzwa na viongozi husika na kufikia makabaliano au mapatano "anaeleza shaka.
Hata hivyo aliwaeleza kuwa iwapo mtu tokea mwaka 1995 amekuwa akilalamika akidai kuibiwa kura, hata kama atashiriki mazungumzo bado ataendelea kushikilia msimamo wake wakujiona mshindi na hatakubali lolote.
Shaka alisema wale wote wanosema kama Zanzibar kuna tatizo linalohitaji ufumbuzi pia wana haki ya kujua kuwa Zanzibar ni nchi yenye madaraka yake ya ndani ikiongozwa kwa taratibu za katiba yake, sheria na kanuni husika za kiserikali.
"Mazungumzo, majadiliano au upatanishi wa kisiasa utokanao na misuguano ya wanasiasa hauwezi kubatilisha nguvu za kikatiba au sheria za nchi husika ,
0 Maoni