Jumapili, 27 Machi 2016

UVCCM TAIFA INAWATAKIA PASAKA NJEMA

Kwa niaba ya Jumuiya ya Vijana wa CCM(UVCCM)

Tuwatakia Sikukuu njema kwenu nyote,

Nawatakia heri ya Sikukuu ya Pasaka, nikiwa nimekaa Kariakoo, maeneo ya Jangwani na Watoto sita wa Mtaani.

Mmoja wa Watoto hawa nilimjua wiki tatu hivi zilizopita.

Nikiwa na Vijana Wenzangu nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, mbele yetu jirani kabisa na lami ya Lumumba road alilala kijana mdogo wa miaka 13.

Akiwa hana ndala na nguo chafu sana, nyuso yake iliashiria njaa Kali sana.

Nikiwa nataka kuendesha Pikipiki kutoka eneo hilo nafsi ilikataa, nilimuamsha kijana huyo alielala juani.

Kijana amka njoo hapa, unaitwa nani? umetoka wapi? Kwanini umelala hapa?

Kijana : Njaa inauma Kaka kaninunulie chakula,
Nilitokea Mwanza Kuja kumtafuta Mama yangu Hortesia niliambiwa yupo Dar Es Salaam, Sina simu yake wala chochote nimekuwa nikilala Mitaani Kariakoo miezi Sita Sasa.

Maswali nilimuuliza mengi sana,
Kifupi majibu ni hayo alionijibu ili ujaribu kupata picha wewe ambae unakula bata Sikukuu hii ama umepanga kula bata.

Nilimpima kijana huyu kwa kumpa pesa ya kula na kumwambia akanunue Ndala, Shati, Suruali na kunyoa Nywele na kesho yake anitafte kwa kutafta simu yeyote ile ata alipie atume ujumbe nitamuona(Nilimpa Business Card yangu).

Kijana alikuwa mtiifu kweli kwa mara ya kwanza ndani ya Miezi Sita alibadili Nguo.

Leo siku ya Pasaka nimekuja kumuona yeye na wenzake sita na kila Mmoja wao ana Historia yake.

Huruma ilikuja Zaidi baada ya wengine kusema wanafanyiwa vitendo vya liwati usiku na watu wazima na wamelia wakiomba wapande gari warudi kijijini wakakae tu na bibi, kwani hawajui wazazi wao walipo.

Mimi na Marafiki zangu tutawasaidia hawa ikibidi waende na Shule kabisa na baada ya Mwaka Mmoja tutatoa Taarifa rasmi ya Maendeleo yao.

Wakati tunakula bata za Sikukuu ujumbe wangu na Ushauri wangu.

Wakati umefika kwa Serikali kuweka Sheria na utaratibu rasmi kwa watu wote wanaozaa ama wanaotaka kuzaa.

Ndugu zangu tatizo hili ni kubwa sana na Dunia tuendayo sasa si ya kuendelea kuzalisha watu tegemezi, wakutegemea wengine kuishi
Wakati wapo vijana wakike na wakiume ambao kazi yao wao kuzaa tu bila kulea.

Binti anashika Mimba lazima amtaje aliempa na wote waandikishwe wata wajibika kumlea Mtoto mhusika ikibidi Serikali imlee Mtoto ila  Baba na Mama wakae Gerezani kama wameshindwa kulea Mtoto wao.

Hii itakomesha kuzaa ovyo na kutelekeza ovyo Watoto mtaani.

Itasaidia pia kukuza kizazi kinacho eleweka katika kujitaftia Ajira na kukipa Elimu ya Bure.

Elimu ya Bure isiwe ndio tiketi ya kufyatua Watoto Vijijini na kuwatelekeza.

Wito wangu kwa Rais.... Iwe wanaotelekeza watoto kwabibi zao, mtaani huku wakipata shida watu hao ni Majipu lazima watumbulie haraka sana.

Tunawatakia pasaka Njema.

Imetolewa leo Machi 27, 2016 na;
Abubakar Asenga,
Mtoto wa Fundi Cherahani,
Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano.
Meseji 0715429738.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu