• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Ijumaa, 15 Aprili 2016

KAIMU KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA SHAKA HAMDU SHAKA AWASILI WILAYA YA NGORONGORO KUHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA

 Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shakha Hamdu Shakha akihutubia wafugaji katika wilaya ya Ngorongoro katika wilaya hiyo

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shakha Hamdu Shakha (wanne kushoto)  akiwasili
katika wilaya ya Ngorongoro ambapo alifanya mkutano wa hadhara na kuzindua
matawi ya chama  katika wilaya hiyo.wakwanza mstari wa mbele ni Mwenyekiti
wa UVCCM Arusha Lengai Ole Sabaya (PICHA NA WOINDE SHIZZA,NGORONGORO)
Share:

Jumatatu, 11 Aprili 2016

WABUNGE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUHAMASISHA JAMII JUU YA FURSA ZA KIBIASHARA ZINAZOPATIKANA AFRIKA MASHARIKI

WABUNGE wa Jumuiya la Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii ili kujua fursa za Kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ameyasema hayo leo Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa wataanza kuhamasisha jamii katika soko la Kariakoo na Soko la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam pamoja na vyombo vya habari mbalimbali.

Makongo amesema kusudi la kuelimisha jamii ili wafanyabishara waweze kufanya biashara katika nchi za Afrika Mashari kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashari Makongoro Nyerere akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji, Miriam Yahaya Usi, Ndarakilo Kessy na Dk.Twaha Tasilima wakiwa katika mkutano huo leo.


Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi (Katikati)akifafanua jambo katika mkutano wa waandishi wa habari na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
Mbune wa Bunge la Afrika Mashariki, Nderakilo Kessy (aliyesimama )akizungumza na waandhishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na wabunge hao kuanza kuhamasisha jamii juu ya Fursa zilizopo katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji akizungumza kuhusiana na Fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashari.

Amesema kuwa frusa zilizopo kwa waalimu wa Lugha ya Kiswahili wanaweza kwenda kufundisha Kiswahili kwenye Nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Afrika ya kati ipo mbioni kujiunga na Umoja huo.

Amesema Lugha ya Kiswahili kwa sasa imeanza kushika karibu nchi zote za Afrika Mashariki na hii ndio fursa Kubwa tuliyo nayo.

 Share:

Ijumaa, 8 Aprili 2016

OLE SENDEKA: LOWASSA ANADANGANYA WATANZANIA KUTAFUTA MASLAHI KISIASA

Ndugu Christopher Ole Sendeka akizungumza leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.
Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili  kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.
 
Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha  shughuli za maendeleo nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi. 


Ndugu Christopher Ole Sendeka   
MSEMAJI WA CCM 
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
                                                     08/04/2016       
Share:

MWENYEKITI WA UVCCM KILIMANJARO ASHINDA KESI YA UDIWANI KATA YA BOMA MBUZI

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Juma Raibu ameshinda kesi ya Udiwani Kata ya Boma Mbuzi, Manispa ya Moshi.
Share:

BREAKING NEWZZZ; ASENGA ABUBAKAR ASHINDA KESI YA PINGAMIZI, AMBWAGA LIJUA LIKALI KESI YA UBUNGE LEO

Aliyekuwa  Mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Kilombero na Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na MawasilUVCCM TAIFA, Ndugu Abubakar D. Asenga.

ASANTE MWENYEZI MUNGU
NAWASHUKURU WANASHERIA WANGU HASA Onesmo Mpenzile.

Leo tumeshinda Mapingamizi ya Mbunge Lijua Likali wa Jimbo la Kilombero alioweka Chini ya Adv. Tundu Lisu akitaka kesi yetu itupiliwe mbali.

Hivyo kesi ya msingi inaendelea kwa kadiri mahakama itakavyo panga na kwa mashahidi elfu 45 tulionao ambao ni wapiga kura wetu tunaimani mahakama itatenda haki na uchaguzi kurudiwa Kilombero.

Mtoto wa Fundi Cherahani.
Asenga A.D
0715429738
Share:

BREAKING NEWZZZ;MABULA AMBWAGA WENJE KESI YA UBUNGE JIJINI MWAZA LEO

Mbunge wa jimbo la Nyamagama,jijini Mwanza pichani akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi wa jimbo hilo na Mahakama kuu ya jijini Mwanza dhidi ya aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CHADEMA,Mh.Ezekiel Wenje.

Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Nyamagana iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (CHADEMA) dhidi ya Mbunge wa sasa wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM) ilikuwa ikiendelea katika mahakama Kuu Mwanza ambapo Ezekiel Wenje alifungua kesi hiyo akipinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yakimpa ushindi Mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula. 

Leo April 8 2016, maamuzi ya kesi hiyo yametangazwa rasmi ambapo Mbunge Stanslaus Mabula ameshinda kesi hiyo, baada ya kubainika upande wa madai hauna ushahidi unaokidhi, kuithibitishia mahakama.

Sikiliza Sauti ya Mbunge wa Nyamagana  Mh.Stanslaus Mabula akizungumza na Wanannchi mara baada ya Uamuzi wa Mahakama kutolewa leo,ambapo yeye ameibuka mshindi dhidi ya aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CHADEMA,Mh.Ezekiel Wenje.  


 Wananchi wakifurahia ushindi wa Mbunge wa CCM Mh. Stanslaus Mabula.
Share:

Alhamisi, 7 Aprili 2016

LEO NI KARUME DAY: KUMBUKUMBU YA MIAKA 44 YA KIFO CHA SHEIKH AMANI ABEID KARUME

 Rais wa kwanza wa Zanzibar  HayatiSheikh Abeid Amani Karume

Leo April 7, 2016 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 44 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi. 

Mzee Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964. 

Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya Muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Mzee Karume alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hapa ndipo alipouwawa Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume miaka 44 iliyopita ndani ya ofisi za Makao Makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja, wakati akicheza bao na marafiki zake. Matundu yanayoonekana ukutani ni ya risasi ambayo muuaji alimimina kabla na yeye kuuwawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa Hayati Karume. Sehemu hii imewekwa uzio maalumu ili kupahifadhi kama kumbukumbu, kwani kila kitu kipo vile vile kilivyokuwa siku hiyo

Wanafunzi wakitembelea mahali alipouwawa Hayati Mzee Karume.
Share:

MWENYEKITI WA CCM ATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM

 Kaimu Mhariri Mtendaji wa Uhuru ublications Limited, Wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Ramadhani Mkoma, akimweleza jambo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaa Kikwete alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Uhuru Publicatiions Ltd  alipotebelea kampuni hiyo leo. Pamoja naye ni Msemaji wa CCM, Cliristopher Ole Sendeka na Mwenyekiti wa Bodi ya Uhuru Media, Adam Kimbisa.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni alipoingia katika Ofisi za Uhuru FM leo. Wengini ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, Adam Kimbisa na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali
Baadhi ya wayanyakazi wa UHURU FM wakiwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipoingia studio wa Uhru FM.
Share:

Jumatano, 6 Aprili 2016

JK AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ITALY LEO

Mwakilishi Maalum wa AU kuhusu mgogoro wa Libya Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italy Dk. Mario Giro leo

Mwakilishi Maalum wa AU kuhusu mgogoro wa Libya Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italy Dk. Mario Giro leo

Msaidizi wa Mwenyekiti wa CCM,Suleiman Mwenda akiteta jambo na  Dk. Jakaya Kikwete Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM.

Msaidizi wa Mwenyekiti wa CCM,Suleiman Mwenda akitoa ufafanuzi wa kilichozungumzwa kati ya Mwakilishi Maalum wa AU kuhusu mgogoro wa Libya Dk. Jakaya Kikwete na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italy Dk. Mario Giro

Msaidizi wa Mwenyekiti wa CCM,Suleiman Mwenda akitoa ufafanuzi wa kilichozungumzwa kati ya Mwakilishi Maalum wa AU kuhusu mgogoro wa Libya Dk. Jakaya Kikwete na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italy Dk. Mario Giro.

NA MWANDISHI MAALUM
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) katika mgogoro wa Libya, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete leo amekutana na Naibu  Waziri wa Mambo ya nje wa Italy Dk. Mario Giro, katika Ofisi Ndogo ya  Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo maalum.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo, Msaidizi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Suleyman Mwenda alisema, Dk. Kikwete amekuwa na mahusiano ya kirafiki ya muda mrefu na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italy Dk. Mario Giro, hivyo Naibu Waziri huyo amefanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya kumjulia hali kama rafiki yake wa muda mrefu.

"Pamoja na kuja kumsalimia kama rafiki wa siku nyingi, lakini lengo hasa la Naibu waziri huyo ni kutaka maelezo juu ya suala la Libya' alisema Mwenda na kuongeza  "Kama mnavyofahamu kuwa Dk. Kikwete ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika (AU) kuwa mwakilishi katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa Libya".

Alisema, Italy inalipa umuhimu wa kipekee suala la Libya kutokana na kwamba nchi hiyo  ni jirani hivyo ina maslahi mapana na ya karibu juu ya suala la amani ya Libya, Dk. Giro ameiwakilisha nchi yake katika kujua hatua ya usuluhishi na  hatma ya mgogoro wa Libya.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri huyo aliambatana na Balozi wa Italy hapa nchini, Luigi Scotto pamoja na Dk. Raffaele De Lutio, Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Italy.
Share:

COMRADE ASENGA ABUBAKAR YUPO LIVE CHANNEL 10


Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano UVCCM TAIFA, Ndugu Abubakar D. Asenga akiwa mzigoni live hivi sasa ndani ya Kipindi cha MADA MOTO ndani ya Chaneli 10.
MADA; AGIZO LA RAIS KWA VIJANA KUFANYA KAZI JE LINATEKELEZEKA?
Share:

JPM NA KAGAME WAZINDUA RASMI DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO NA KITUO CHA HUDUMA ZA PAMOJA MPAKANI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo, mchana huu. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi daraja la kimataifa la Rusumo, mchana huu. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Ujenzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA. Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka. 
 Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
 Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la Rusumo mara baada ya uzinduzi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi  wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
 Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huo
Share:

Jumatatu, 4 Aprili 2016

MWENYEKITI WA UVCCM KILIMANJARO AFANYA ZIARA MOSHI MJINI


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa wa  Kilimanjaro, Ndugu Juma Raibu akihutubia katika mkutano uliofanyika viwanja vya Pasua Sokoni.

Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Moshi Ndugu Joel Makwaia akiwa Jukwani kwenye Mkutano wa hadhara akiongea na Wananchi.

Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Moshi Ndugu Joel Makwaia akisoma taarifa ya Nazi kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa  Kilimanjaro, Ndugu Juma Raibu.


Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Moshi katika viwanja vya Pasua Sokoni

Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Moshi katika viwanja vya Pasua Sokoni

Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Moshi katika viwanja vya Pasua Sokoni

Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Moshi katika viwanja vya Pasua Sokoni

Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu