Jumatatu, 4 Aprili 2016

BREKING NEWS.....ZAINAB KATIMBA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI KUHUSU SERA YA MAFUNZO KWA VITENDO


Dar es Salaam. 02.04.2016.

Mbunge wa viti Maalumu Mhe.Zainab Katimba (CCM) amewaahidi vijana wenzake waliowakilisha taasisi 10 za vijana, kuwa atawasilisha bungeni hoja binafsi juu ya kuliomba bunge kupitisha azimio la kuitaka serikali kuunda Sera ya Mafunzo kwa vitendo ( Internship policy)ili kukabiliana na changamoto ya kukosa uzoefu ( work experience) wanapokwenda kuomba kazi sekta binafsi na sekta ya umma.

Mbunge Zainab Katimba aliyasema hayo katika hoteli ya Grand Villa kijitonyama alipokutana na asasi 10 za vijana zikiongozwa na TYVA, YUNA, YPC, TYC, TAMASHA, ACTIVISTA, FEMINA, YOA, OMT na ENREDO.

Vijana hao kwa pamoja walikubaliana kufuatilia utatuzi wa changamoto za ajira kwa vijana na kupitisha azimio la kuafiki Mbunge Katimba kuwasilisha hoja binafsi katika kuunda sera ya mafunzo kwa vitendo. Sera hiyo itawafanya vijana wa vyuo vya elimu ya juu kupata fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo katika taasisi za umma na binafsi bila vikwazo ambavyo kwa sasa vinawakosesha fursa hiyo.

Pamoja na mambo mengine asasi hizo za vijana zimeunda muungano wa kuchambua na kusimami maswala/maslahi ya  wa vijana bungeni yaani Parliamentary Youth Working group.

Muungano huo wa vijana umedhamiria kufanya uchambuzi wa bajeti ya wizara inayoshughulikia vijana kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Muungano huo unatarajia kukutana na kundi kubwa zaidi la wabunge vijana bila kujali itikadi zao za vyama ili kufanikisha mabadiliko ya sera mtambuka mbalimbali zinazowahusu vijana.

Imetolewa na:

Tanzania Youth Vision Association (TYVA)
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu