Jumapili, 3 Aprili 2016

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM ATIKISA JIJI LA MWANZA

Kaimu Katibu Mkuu wa UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa, Ndugu Shaka Hamdu Shaka (kulia) akizungumza wakati wa Semina, katikati ni Mkuu wa Idara ya Utawala Uvccm Makao Makuu Ndugu Omari Mwanag'walu na Mjumbe wa Baraza la UVCCM Taifa Viti 5 Bara Mtemi Sylvester Yaredi (kushoto).Kaimu Katibu Mkuu wa UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa, Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Uvccm, kulia ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Ndugu Miraji Mtaturu.


Kaimu Katibu Mkuu wa UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa, Ndugu Shaka Hamdu Shaka akipandisha Bendera ya CCM kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi la UVCCM.

Kaimu Katibu Mkuu wa UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa, Ndugu Shaka Hamdu Shaka (watatu kulia) Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana, Ndugu Kheri James (wapili kulia), Mkuu wa Idara ya Utawala UVCCM Makao Makuu, Ndugu Omari Mwanang'walu (watatu kushoto), Mjumbe wa Baraza la UVCCM Taifa Viti 5 Bara, Mtemi Sylvester Yaredi (wapili kushoto) na Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa, Ndugu Rashid Gewa (Kushoto).
Kaimu  Katibu Mkuu  wa UVCCM  Shaka Hamdu Shaka amesema ili kuirudisha jumuiya hiyo katika mkondo mnyoofu wa  usimamizi wa  kanuni za utumishi, miiko na msingi ya  nidhamu, watatumbua vipele vidogo vidogo kabla ya kuyatumbua majipu makubwa ndani ya umoja huo.


Amesema taasisi zote duniani huongozwa kwa mujibu taratibu , kanuni za msingi , kuheshimu  katiba  ili kukuza haiba ya uaminifu, uadilifu na utendaji  bora.


Shaka aliyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na watendaji wa UVCCM ngazi za wilaya na Mikoa ya iliyopo kanda ya ziwa kilichofanyika Mkoani  Tabora na Mwanza.


Alisema katika kufuata misingi na njia sahihi za usimamizi bora wa kiutendaji na kikazi zaidi, utendaji wa pamoja na uwajibikaji ni katika mambo  makuu yanayohitajika katika UVCCM ya sasa.


Aliwakumbusha Kuwa  kila mtumishi katika eneo lake la kazi ajione ana wajibu wa kukisaidia chama Cha Mapinduzi  kufikia malengo yake sambamba na utunzaji wa mali na rasilimali  za jumuiya ikiwemo na utii wa kununi maadili.


"Vipele havijitokezi katika kiwiliwili cha binadamu kama  damu haichafuka, nitatumbua vipele vidogo baadae  nitakamua  majipu makubwa na kusafisha majeraha bila hofu yoyote  kwa lengo la kuimarisha na kujenga jumuiya yenye kuendana na wakati tuliona ili tuendelee kuaminiwa ma vijana walio wengi zaidi"alieleza Shaka


Alisema hadhi na staha ya UVCCM iko katika kiwango cha juu kwasababu tayari  imetoa viongozi wengi ambao wameshika madaraka ya utawala wa nchi katika nafasi mbalimbali za uongozi wa Taifa na medani za utawala wa sasa hivyo ni vyema ari hiyo kuendelezwa na viongozi waliopo sasa.

 
 Kaimu Katibu Mkuu aliwatahadharisha watendaji hao kuwa kila mwanajumuiya, mtumishi na mtendaji yeyote anayefikiri uvccm  ni kichaka cha kuficha uovu , ubadhirifu na ufisadi atajidanganya na daima hatapata nafasi ya kujificha katika  uongozi wa sasa.


"Kila mmoja ajipime, ajichuje na kujitathmini mwenyewe kabla ya hatua za kikanuni hazijachukuliwa dhidi ya mtumishi au mtendaji , kama ulipora , ulishiriki kuvunja kanuni, kufuja mali au kuuza vitega uchumi, hukuna atakayekuhurumia " alisisitiza


Aliwataka watendaji  wa UVCCM toka ngazi za Taifa hadi matawi  kutambua kuwa ni wote wana wajibu wa kutii na kufuata kanuni na katiba pamoja na kuelewa mipaka ya kila mmoja katika kiwango na ukomo wa utendaji wake.


"Kama mtendaji  hujui taratibu au kanuni mbalimbali na miongozo yetu   usijifanye  mwerevu , hujui jambo  hebu uliza ili uelekezwe, kuuliza si ujinga na ukiujifanya kujua wakati hujui unaweza kuvurunda mambo"alisema Shaka huku watendaji wakiwa kimya kumsikiliza kwa makini .


Alisema msimamo wa  Uvccm ambao  umerithiwa toka enzi za TANU na  ASP youth league kabla ya kuzaliwa  Uccm ni dhana ya kiongozi  kuongoza kwa mfano, kukosoa na kuwa tayari kukosolewa pia awe  mzalendo, mtii anayejiheshimu na kuheshimu mwenzake.


Hata hivyo Shaka wakati akihitimisha kufikia mwisho ziara yake ya kukutana na watendaji wa UVCCM ambayo ilianza kanda ya kati  mashariki,, nyanda za juu,  kusini na kuhitimisha akiwa kanda ya ziwa amekutana na kuzungumza na watendaji wa mikoa na wilaya za Mwanza , Geita, Mara na Kagera Shinyanga, Kigoma Katavi, Tabora Simiyu, Rukwa amekamilisha kukutana na watendaji 173 wa wilaya na 32 wa mikoa.

Kwa upande wao watendaji hao wamelezea kuridhishwa na hatua iyo iltakayowaongezea  ari na bidii katika utendaji wao.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu