Jumanne, 31 Mei 2016

SHAKA HAMDU SHAKA; NIMEFARIJIKA, MMENIPA MATUMAINI VIJANA WA IRAMBA


Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka akionyesha umahiri wake wa kunyosha tofari kitaalam zaidi.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka akiwapa ushirikiano mafundi wakati was kupandisha matofali.

Jana 30 Mei 2016 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) ameanza ziara  siku 5 mkoani Singida.  
ziara yake  imeanza katika wilaya ya Iramba kwa kuzindua mashina ya UVCCM zaidi ya 10 na kupata fursa ya kusalimiana na makundi ya vijana kupitia mikutano ya hadhara.
Amesikika akisema: "Nimefarajika sana na mmenipa  matumaini makubwa  kuwa mageuzi ya kimfumo tunayoyakusudia yatokee ndani ya UVCCM yanawezekana, niliwagiza na mmeshuka kutekeleza, mashina ya UVCCM kugeuzwa kuwa mashina ya kuwakusanya  kuwawezesha vijana katika masuala ya ujasiriamali mumetekeleza kwa vitendo kauli mbiu yetu ya siasa na uchumi kwa vijana wakati wake ni sasa , nasema hakuna njia ya mkato ya  kufikia maendeleo ya kiuchumi pia kujikwamua na umasikini  lazima muwahamasishe vijana wajitume kwa bidii kama  mfanyavyo sasa" alisema Katibu Mkuu.
Alimbelea na kukagua mashina ya vijana wa ujasiriamali ya bodaboda useremala , wauza  mafuta ya alizeti, kilimo cha bustani na mifugo.
Katibu Mkuu alishiriki katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Musuna na kushiriki shuhuli za ufyatuaji matofali kwa kushirikiana na wananchi.

Katibu Mkuu aliwatembelea vijana wanasomea Uuguzi katika chuo cha Kiomboi (KNTC) na kupata fursa ya kubadilishana nao mawazo  pamoja na mambo mengine vijana hao walimuelezea Katibu Mkuu changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo ikiwemo ukosefu wa chakula  huku wakila mlo mmoja asubuhi hadi usiku kwenye magenge ya mama ntilie magengeni ambako si salama sana. 
Kukosekana huduma za vyoo chuoni hapo jambo linalowalazimu wajisaidie maeneo ya nje na chuo. 
Kukosekana kwa utaratibu mzuri wa mitaala ya ufundishaji sambamba na ukosefu wa walimu, madawati, vifaa vya kufundishia masomo  ikiwemo kompyuta nk. 
Wanafunzi hao wameeleza kuwa tatizo jingine ni umeme wa uhakika kutokana na kukatika katika ovyo umeme nyakati za usiku jambo ambalo linawakosesha wanafunzi hao kujisomea nyakati za usiku, utaratibu mbovu wa usimamizi katika shuhuli za utawala jambo linalonyesha kama serikali imekitelekeza Chuo hicho, wanafunzi hao wakiongozwa na Rais wa serikali ya chuo hicho  walisimama mbele ya ujumbe wa Katibu Shaka kuelezea kero, madhila, shida na adha zinazowakabili wanafunzi chuoni hapo. 

"Hapa hatufanyi siasa tunatembea ili kuona na kukagua  utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika maeneo ya huduma za jamii na maendeleo ya kisekta yanakwenda sawa au la , kimsingi hatuwezi kuona vijana  wakinyanyasika na sisi tukichekelea,  nakugiza Mwenyekiti UVCCM Mkoa na kamati  ya utekelezaji pia  nakuomba Katibu wa CCM wa Wilaya hii, tokeni mkanitafutie Mkuu wa Wilaya,   Mkurugenzi wa Halmashauri, Mganga Mkuu wa wilaya na  Mkuu wa chuo kokote walipo tukutane hapa kesho asubuhi  ili waje   kujibu hoja zilizojitokeza na watuahidi utatuzi wake katika muda mfupi,  wambieni endapo hawatakuja nitakuja  kuwabeba wanafunzi wote nakwenda kufunga ofisi zao hadi watakapoamua  kutafuta njia za kutatua changamoto zilizopo  . 
nawakumbusha watendaji waliopewa  dhamana ya kusimamia serikali ya  Chama cha Mapinduzi kusimamia wajibu wao na kuwa  sasa Wakati umefika anaetaka kufanya  kazi na Rais Magufuli afanye  anachokitaka Rais na asiyeweza  atupishe kwasababu wakifichwafichwa vijana tutawaumbua .
Kauli ya Katibu Mkuu aliposimama kutaka kusalimiana na wanafunzi wa chuo hicho,  kauli ilipokelewa kwa Shangwe na nderemo 
na wanafunzi hao.
Jioni yake Katibu Mkuu alitembelea shule ya Watoto wenye ulemavu  New Kiomboi na kutoa msaadaa wa chakula ( unga wa ngano, sukari, mchele, mafuta, sabuni za kuogea na magodoro) ili kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabili watoto hao wenye ulemavu na  wale wanaoishi katika mazingira magumu.
Katibu Mkuu amemalizia ziara yake katika wilaya ya Iramba kwa kuzungumza na viongozi wa Chama na jumuiya zake katika ukumbi wa ofisi ya CCM wilaya na kisha kuelekea wilaya ya Mkalama kuendelea na ziara.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu